Ramani ya Afrika mwaka 1959

Ramani ya Afrika mwaka 1959

Cesar Saint

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2016
Posts
423
Reaction score
726
Hivi ndivyo Afrika ingekuwa kama mipaka yake ingewekwa kutokana na Lugha na jamii kubwa (Major Ethinic) mwaka 1959

IMG_1619.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana Afrika ingekuwa ndiyo super power kama waafrika tusingekuwa wapumbavu na wapenda madaraka kama tulivyo mpaka sasa. Afrika iliyoungana ni hatari kuliko taifa lolote linalotawala dunia hii mpaka sasa. Ukijumlisha nguvu na eneo wanalotawala watu weusi na waafrika ndilo lenye rasilimali za aina zote, misitu iliyo bora, mafuta mengi, madini aina zote, mito ya kila namna, ardhi inayofaa kwa kila kitu, watu wengi wa kutosha, nk,nk,nk.

Tatizo la watu weusi dunia hii ni kugawanywa na kudanganywa kuwa ukiwa rais wa kanchi kama malawi utafanana na Trump au Xi Jingpin wa China. Naitamani siku Aftika imeungana, tunaweza kuwa na states hata mia na hamsini au mia mbili, lakini Rais mmoja. Federation ya Afrika ikiundwa leo na hawa viongozi wetu wakaiona Afrika kuwa nchi moja, utakuwa mwanzo wa Afrika kuwa Super power ndani ya miaka 50.
 
Tatizo huanzia na kuwa historia ya afrika haifundishwi mashuleni mitaala ya wanaojiita wasomi hukazana na kufundisha utumwa na ukoloni bila kujua hujenga kizazi dhaifu kisichoweza kujisimamia na kujivunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la watu weusi dunia hii ni kugawanywa na kudanganywa

"Kugawanywa na Kudanganywa".

Hebu yafikirie hayo maneno mawili tu kwanza, na hapo utaona upungufu wa hoja nzima unayoitetea.
Hii dhana ya weusi kuwa na udhaifu kila sehemu na kutakiwa waendeshwe na wengine ni jambo la kutisha sana.

Hapa kwetu sasa hivi tunasikia kelele nyingi kuhusu Lissu "kudanganywa' au 'kununuliwa' na mabeberu.

Kelele nyingi zinasikika kuhusu njama za mabeberu (watu wasiokuwa weusi), kutufanyia njama za kuturubuni na vimisaada vyao ili kuzuia maendeleo yetu (tusijitegemee wenyewe) kwa kujiletea maendeleo wenyewe! Na hali wakati huo huo, tunalalamika na kupiga kelele nyingi kuhusu Tundu Lissu anavyosaliti taifa letu kwa kwenda kutuchomea utambi kwa washirika wetu tusipate misaada!

Nadhani unaweza kuona mtiririko mzima wa dhana hii ya kusadikika uliyioweka katika mchango wako kwenye bandiko hapo juu.

Hivi hawa weusi ni viumbe wa aina gani ambao kila mara mambo yao ni lazima yaingiliwe na wengine na sio wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuyasimamia?

Tusipende sana kuwa watu wa lawama kwa wengine bila ya kujipima sisi wenyewe kwanza madhaifu yetu.

Kwa maoni yangu, hali inayomkabili mtu mweusi kwa sasa hivi inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mweusi mwenyewe. Kama elimu tuliyopata tokea kuwa huru haiwezi kutusaidia kutumia vichwa vyetu vizuri na kuamua tunataka nini; na hapo hapo vichwa hivyo tuendelee kuvikodisha kwa hao waliokuwa wanatunyanyasa (wakoloni), tunataka kitu gani kitokee ili tuweze kuvitumia vichwa vyetu vizuri?

KWADO ABIMBOLA, usinielewe vibaya. Sipingi hoja yako, ila nina mtazamo tofauti tu na wa kwako.
 
Haya ona sasa," Gorge Peter, Murdock" anaijua historia ya wafrika kuliko waafrika wenyewe wanavyoijua!

Sijui hicho kitabu kiliandikwa lini(1959)?; lakini mtu unaweza ukajiuliza katika wasomi wote tuliokuwa nao Afrika nzima hakuna aliyeweza hata kujitokeza na kuiandika historia hiyo?

Niseme hapa, inawezekana vipo vitabu vya aina hiyo vingi vilivyoandikwa na wazungu na/au WaAfrika, ambavyo hatujui kuwa vipo! Hiki kinaweza kuwa kimojawapo kati ya vingi? Lakini ni nani anayeifundisha historia hiyo?
 
Ni wazi kuwa historia ya afrika inayofundishwa si kamili bali kuanzia utumwa na ukoloni hata maswali ya watahiniwa wetu kwa sehemu kubwa hulenga humo kipengele cha states ni kidogo sana tukiwa wadogo kulikuwa na maswali kama mzungu wa kwanza kuona ziwa Victoria anaitwa nani? Unajiuliza kwani hili ziwa halikuwa na jina hapo kabla? Hizi historia hasifundishwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kugawanywa na Kudanganywa".

Hebu yafikirie hayo maneno mawili tu kwanza, na hapo utaona upungufu wa hoja nzima unayoitetea.
Hii dhana ya weusi kuwa na udhaifu kila sehemu na kutakiwa waendeshwe na wengine ni jambo la kutisha sana.

Hapa kwetu sasa hivi tunasikia kelele nyingi kuhusu Lissu "kudanganywa' au 'kununuliwa' na mabeberu.

Kelele nyingi zinasikika kuhusu njama za mabeberu (watu wasiokuwa weusi), kutufanyia njama za kuturubuni na vimisaada vyao ili kuzuia maendeleo yetu (tusijitegemee wenyewe) kwa kujiletea maendeleo wenyewe! Na hali wakati huo huo, tunalalamika na kupiga kelele nyingi kuhusu Tundu Lissu anavyosaliti taifa letu kwa kwenda kutuchomea utambi kwa washirika wetu tusipate misaada!

Nadhani unaweza kuona mtiririko mzima wa dhana hii ya kusadikika uliyioweka katika mchango wako kwenye bandiko hapo juu.

Hivi hawa weusi ni viumbe wa aina gani ambao kila mara mambo yao ni lazima yaingiliwe na wengine na sio wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuyasimamia?

Tusipende sana kuwa watu wa lawama kwa wengine bila ya kujipima sisi wenyewe kwanza madhaifu yetu.

Kwa maoni yangu, hali inayomkabili mtu mweusi kwa sasa hivi inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mweusi mwenyewe. Kama elimu tuliyopata tokea kuwa huru haiwezi kutusaidia kutumia vichwa vyetu vizuri na kuamua tunataka nini; na hapo hapo vichwa hivyo tuendelee kuvikodisha kwa hao waliokuwa wanatunyanyasa (wakoloni), tunataka kitu gani kitokee ili tuweze kuvitumia vichwa vyetu vizuri?

KWADO ABIMBOLA, usinielewe vibaya. Sipingi hoja yako, ila nina mtazamo tofauti tu na wa kwako.
Nashukuru sana kwa majibu yako mazuri sana na mawazo yako.
Japo sijafanya utafiti kuhusu watu weusi (waafrika) na mahusiano yao na sayari ya dunia, picha ninayoipata kwa haraka ni kuwa watu weusi mpaka tunaingia kwenye "civilization period -yaani kuanzia 16th century" walikuwa wametapakaa kwenye maeneo tajiri kuliko mahali pengine popote kwenye hii sayari. Yawezekana bado mpaka sasa, tukiingia deep tutawakuta binadamu weusi wanakalia maeneo yenye potential kuliko mahali pengine popote duniani (awezaye ajaribu). Na hapa namaanisha popote watu weusi walipo, siyo lazima Afrika peke yake.

Tatizo la waafrika weusi hasa ni nini? Binafsi nawaona waafrika weusi na aina ya mataifa na muundo tuliyoaminishwa kuwa ndio tunaotakiwa kuwa nao ni tatizo kubwa. (Muundo wenyewe ni Wa marais wanaotawala kama wafalme, wenye nguvu kama za miungu, wanaoweza kuamua chochote, na wanaotaka kufanana na wenzao wazungu kwa kila hali bila kuangalia uhalisia wa mataifa watokayo).

Waafrika tumedanganywa na kudanganyika vilivyo. Tunapaswa kufanya mapinduzi ya kiafrika ya karne ya 21. Tufute mifumo tuliyo nayo ya sasa na tufikiri mifumo mipya inayoweza kutukomboa. Hii mifumo ya wazungu ni namna tu ya kuhakikisha tupo under control na hatufikii potential yetu na hadhi yetu ya kuwa super power.

Binafsi sitakuwa na shida kuwa na mfalme/(au rais) mmoja wa Afrika atakayependekezwa na kuchaguliwa na wawakilishi wa state govermnents (au maseneta) kutoka kila state. Nchi kama Tanzania, inaweza kumezwa na kuwa state 5 mpaka 7. Tukawa na local governments zinazoweza kuwa efficient na ambazo hazitajihusisha na mambo ya nje wala jeshi. Hawa marais wetu wawe tu wawakilishi wa kupanga sera kuu za majimbo ya Afrika na kusimamia mambo makubwa makubwa ya kuifanya Afrika kuwa super power within 50 years.
 
Tatizo huanzia na kuwa historia ya afrika haifundishwi mashuleni mitaala ya wanaojiita wasomi hukazana na kufundisha utumwa na ukoloni bila kujua hujenga kizazi dhaifu kisichoweza kujisimamia na kujivunia

Sent using Jamii Forums mobile app
Tulipaswa kuitazama Afrika kwa kuangalia watu wake na rasilimali zake na potential yake. Haya mambo ya utumwa natamani tungeyafuta kwenye sylabbus. Turudi karne ya 16, tuanzie statez za afrika zilivyokuwa organized, twende kwenye colonization ya afrika ambayo ndiyo imetuma nchi zilizopo sasa. Kwa maana halisi sisi bado tupo colonized, tumeaminishwa kuwa mfumo wa kutawala, elimu, kula, kuvaa, kusali, nk.nk. ni lazima ufanane na ule tulioletewa na wakoloni.

Tukitoka hapo tuwafundishe vizazi vinavyokuja kuhusu new struggle kuelekea kuirudisha Afrika kwenye reli. Kurudisha new Afrika, ambayo inaweza kupangilia na kutumia rasilimali zake (watu-brainpower, ardhi na vilivyopo na tunavyoweza kuitumia kuilisha dunia). Tunapaswa kuja na kitu kipya. Siyo lazima tuige kwa watu weupe.
 
Afrika kuwa super power within 50 years.

Tukubali kutokubaliana kwa hili KWADWO.

Nikipata ki nchi kama ki-Austria pale Ulaya, Ki-nchi kama Korea pale Asia; hata vi-nchi kama Malaysia tu n.k., na watu wake wanadunda vizuri tu na maisha ya kuridhisha, 'utopia' ya kuwa li-super power miaka 50 ijayo hainivutii chochote, na hasa nikijua hiyo ni ndoto ya jinamizi kabisa.

Ethiopia wasipotetereka tena, wamo njiani kuelekea kwenye baadhi ya nchi hizo nilizozitaja.

Pamoja na vurugu zote walizonazo Nigeria, siwezi kuwaondoa kwenye orodha ya nchi zinazoelekea kwenye mwanga katika miaka hiyo 50 uliyoiweka kama mfano.

Tanzania tungeweza sana kama tungepunguza uswahili wetu mwingi na hasa tukaweka mkazo katika elimu yetu iwe imara zaidi. Uwezo wa kutufikisha huko pazuri upo sana. Tuache tu haya mambo mengi ya ubabaishaji tulionao.
 
Nashukuru sana kwa majibu yako mazuri sana na mawazo yako.
Japo sijafanya utafiti kuhusu watu weusi (waafrika) na mahusiano yao na sayari ya dunia, picha ninayoipata kwa haraka ni kuwa watu weusi mpaka tunaingia kwenye "civilization period -yaani kuanzia 16th century" walikuwa wametapakaa kwenye maeneo tajiri kuliko mahali pengine popote kwenye hii sayari. Yawezekana bado mpaka sasa, tukiingia deep tutawakuta binadamu weusi wanakalia maeneo yenye potential kuliko mahali pengine popote duniani (awezaye ajaribu). Na hapa namaanisha popote watu weusi walipo, siyo lazima Afrika peke yake.

Tatizo la waafrika weusi hasa ni nini? Binafsi nawaona waafrika weusi na aina ya mataifa na muundo tuliyoaminishwa kuwa ndio tunaotakiwa kuwa nao ni tatizo kubwa. (Muundo wenyewe ni Wa marais wanaotawala kama wafalme, wenye nguvu kama za miungu, wanaoweza kuamua chochote, na wanaotaka kufanana na wenzao wazungu kwa kila hali bila kuangalia uhalisia wa mataifa watokayo).

Waafrika tumedanganywa na kudanganyika vilivyo. Tunapaswa kufanya mapinduzi ya kiafrika ya karne ya 21. Tufute mifumo tuliyo nayo ya sasa na tufikiri mifumo mipya inayoweza kutukomboa. Hii mifumo ya wazungu ni namna tu ya kuhakikisha tupo under control na hatufikii potential yetu na hadhi yetu ya kuwa super power.

Binafsi sitakuwa na shida kuwa na mfalme/(au rais) mmoja wa Afrika atakayependekezwa na kuchaguliwa na wawakilishi wa state govermnents (au maseneta) kutoka kila state. Nchi kama Tanzania, inaweza kumezwa na kuwa state 5 mpaka 7. Tukawa na local governments zinazoweza kuwa efficient na ambazo hazitajihusisha na mambo ya nje wala jeshi. Hawa marais wetu wawe tu wawakilishi wa kupanga sera kuu za majimbo ya Afrika na kusimamia mambo makubwa makubwa ya kuifanya Afrika kuwa super power within 50 years.
Hapo sawa lakini ujue lazima tuuue sana katika vita itakayo anzishwa hapo Usa. Russia na China hazikuungana kilele mama. mamilioni walikufilia kwa mbali ambao hawakutaka umoja. kwa maana kwamba ni lazima ilikuwa waungane. chukulia mfano Zanzibar vile vijamaa havitaki muungano kabisa siyo wote baadhi Nyerere alifyatua kafara yadamu, ndo maana leo unaona tuna kajimuungano. lakini pia kun vijamaa havitaki hata kwa kuviangalia tu,
 
Nakuelewa sana hoja yako. Msingi wa hoja yako ni viongozi wa Afrika wenyewe. Sidhani kama mtu kama akina Nkurunzinza au Kagame watapenda wawe magavana wa mikoa ya Burundi na Rwanda. Kila binadamu ameumbwa na greed. Ni pale tu atakapodhibitiwa na kuona hakuna namna nyingine ndipo binadamu atakubali kubadilika na kudhibiti kiu yake ya mamlaka, mali, fedha na ukuu dhidi ya binadamu wengine.

Binafsi naona ni afadhali kuwakabili watu wa aina hiyo kwa manufaa mapana ya waafrika ijayo.
 
Kalamu1 tatizo waafrika wanataka kila wakati wasiwe wao ndiyo wenye kubeba lawama linapotokea tatizo. Kwenye ulimwengu nchi nyingi sana ziliwahi kutawaliwa kikatili na watawala wao wa zamani lakini sasa zimepiga hatu makubwa sana ya kimaendeleo.

Katika nchi tano zilizoendelea zaidi Ulimwenguni, yaani Marekani, Uchina, Ujerumani, Japan na Uingereza, zote hizo kwa nyakati tofauti ziliwahi kutawaliwa na watawala wabaya. Wao tofauti na sisi waliona jukumu la kuwaondoa watawala wabaya lilikuwa ni lao.

Mapinduzi ya Ufaransa yalikuja si kwa lengo la kuuondoa utawala wa kifalme kwenye Ufaransa, bali kufanya wafaransa ndiyo wawe wenye kufanya maamuzi wenyewe kwenye maisha yao ya kila siku.

Tatizo Afrika watu wanataka kuwepo madarakani ama kufanya mapinduzi bila ya kuwa na dira ni kwa nini wanayataka madaraka wanayoyatamani. Afrika haina mifano mizuri kabisa ya kuwa na kundi kubwa linalotamani jamii iwe na usawa.

Kwa nini Afrika tusishangae ni kwa nini viongozi tunaowabadilisha wote wanafanana? Kwa nini viongozi wa Afrika huwa tofauti kabla ya kuwa madarakani na wakati wakiwa madarakani? Inakuwaje viongozi wengi wa Afrika huwa hawajali wale wanaowatawala na ni kwa nini wengi wao hutamani kutawala milele?

Hivi kweli tatizo ni viongozi tu ama tatizo ni jamii nzima ya waafrika? Inawezekanaje tukawa na viongozi wabovu katikati ya jamii ya watu waliostaaribika?

Kuna mambo mawili kuhusu Afrika sikubaliana nayo hata kidogo. Kwanza sikubaliani kwamba tupo hivi kwa kuwa tulitawaliwa na wakoloni ambao waliturithisha elimu yao inayotufanya tusiiangalie Afrika Kiafrika. Miaka zaidi ya 60 tangu nchi ya kwanza Afrika kupata Uhuru bado tu tunashindwa kubadili mitizamo yetu kisa tu tulitawaliwa na wakoloni?

Jambo la pili ni Mapinduzi na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Afrika vita vya wenyewe kwa wenyewe na mapinduzi huwa havina mzizi wa kifalsafa kutokea ama kufanyika. Wengi wa waliofanya mapinduzi Afrika wenyewe tena wakawa ving'ang'anizi madarakani.

Hakuna hata vita moja ya wenyewe kwa wenyewe Afrika iliyoanza kwa watu kupishana kifalsafa kuhusu kuliendeleza eneo husika. Hakuna mapinduzi Afrika yenye chanzo cha Kifikra kwanza, bali Mapinduzi mengi yanatokana na wengine kutamani kuwa kama wale walioko madarakani.
 
Hivi kweli tatizo ni viongozi tu ama tatizo ni jamii nzima ya waafrika? Inawezekanaje tukawa na viongozi wabovu katikati ya jamii ya watu waliostaaribika?

LOoo, hilo swali zito hasa ambalo linahitaji fikra pevu kulichambua. Huenda kukawa na siku tukalirejea, hasa tukiwa na wabobezi katika nyanja hizi. Sisi hapa tutapapasa tu kama watu waliogizani.

Kwa ufinyu wa mawazo niliyonayo, ningeanzia kwa kusema kwamba "Viongozi ni sehemu ya jumuia waliomo; lakini pia kutokana na hadhi ya huo uongozi wao ni sehemu mhimu ya ku-'shape' aina ya taifa wanalolijenga. Ni kiungo mhimu sana wanaolielekeza taifa na wananchi wako katika dira maalum waliyonayo viongozi hao.

Sasa sisemi hapa kuwa viongozi hao wanatakiwa wawe na kila kitu vichwani mwao, au mawazo yote yawe ni ya kwao tu; hapana. Lakini viongozi wenye dira huwakusanya viongozi wenzao ndani ya Taifa na kuweka mawazo yao pamoja yatakayoweka mwelekeo wa Taifa lao na jamii yao (wananchi) wanaowaongoza.

Na wala hata sisemi kuwa viongozi hao ni 'perfect',. Watakuwa na mapungufu kadhaa, lakini kiujumla wanakuwa ni viongozi walio na picha kamili wanakotaka kulielekeza Taifa lao.

Mimi sina shaka yoyote kichwani mwangu, kwamba kiongozi kama huyo tuliwahi kumpata hapa kwetu pamoja na uchanga wetu. Mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi wa aina ya picha ninayoiona kichwani mwangu kuhusu hao uliyoyaandika hapo juu.

Na kama hakufanikiwa kulijenga Taifa hilo alilokuwa amelilenga, hilo pia ni jambo linalojadiriwa mara kwa mara; lakini tukumbuke tu hali ya uchanga wetu na mambo mengi yaliyokuwepo duniani wakati akijaribu kuijenga Tanzania aliyokuwa na picha yake kichwani akishirikiana na viongozi na wananchi wote kwa jumla.

Kuna mambo mawili kuhusu Afrika sikubaliana nayo hata kidogo. Kwanza sikubaliani kwamba tupo hivi kwa kuwa tulitawaliwa na wakoloni ambao waliturithisha elimu yao inayotufanya tusiiangalie Afrika Kiafrika. Miaka zaidi ya 60 tangu nchi ya kwanza Afrika kupata Uhuru bado tu tunashindwa kubadili mitizamo yetu kisa tu tulitawaliwa na wakoloni?

Wanaoendelea kuikumbatia na kuitumia dhana hii ni wachovu wa fikra.

Maoni yangu kuhusu uchelevu wetu wa kufikia huko tunakokutamani sote ni kwamba; tusiwe watu wasiokuwa na subira. Tunaweza kutazama mifano mbalimbali ya nchi zilizochukua hatua moja baada ya nyingine hadi kufikia hapo walipo leo.
Kwa nini sisi tunataka leo katika miaka 60 tuwe tumefikia hatua ya Korea Kusini? Tunajua waKorea walikotokea hadi wakafika hapo? Chukulia nchi kama Turkey. Imewachukua muda kiasi gani, pamoja na mizunguko yao miiingi kufikia hapo walipofikia? Kwa nini sisi tunataka leo tuwe kwenye hatua waliyofikia wao katika miaka 60 tu!

Sisemi kamwe kwamba nataka nasi tupitie mizunguko hiyo yooote waliyopitia nchi hizo, na muda waliouchukua kufika huko, La hasha. Kwani nyakati na teknologia zilizopo sasa ni tofauti. Sisi itatuchukua muda mfupi kama tutatuliza mawazo yetu na kuyalenga kwenye maendeleo tunayotaka tuyapate.
Lakini pia kuna upande wa pile wa picha hiyo, nchi kama Haiti, pamoja na kuwa huru miaka zaidi ya 100, wapo hapo walipo. Misri ndio wanaanza kuchangamka sasa, lakini wamechelewa mno!!. Nisingependa Tanzania nasi tuwe kwenye kundi la nchi hizi!

Hapa nataka nitoe mfano wa nchi kama Ethiopia. Kama hawa watatulizana vizuri na kuendelea kwenye kasi waliyonayo sasa hivi, Ethiopia katika miaka kumi ijayo itakuwa ni nchi tofauti sana na hii iliyopo sasa. Huu ni utabiri wangu, na ninaomba Mwenyezi Mungu aniweke nishuhudie utabiri huu.

Tanzania tulianza kuelekea huko, lakini Mh Magufuli nadhani atakuwa amezima breki kidogo kwa sasa. Sijui yajayo baadae.
 
Back
Top Bottom