Ramaphosa azimiwa kipaza sauti baada ya kukosoa vikali Israel kuhusu vita Gaza

Ramaphosa azimiwa kipaza sauti baada ya kukosoa vikali Israel kuhusu vita Gaza

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amezimiwa kipaza sauti kwenye mkutano maalumu wa kujadili umuhimu wa kuanzishwa taifa huru la Palestina, baada ya kuelekeza mashambulizi dhidi ya Israel akidai inachofanya Gaza ni mauaji ya kimbari.

Pia, alifananisha mateso ya Wapalestina wanayofanyiwa na Israel na waliyoyapata Waafrika Kusini wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi wa makaburu nchini Afrika Kusini.

Ramaposa alizimiwa kipaza sauti ghafla kwenye mkutano maalumu ulioitishwa jijini New York na mataifa ya Ufaransa na Saudi Arabia, siku moja kabla ya kufanyika mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Akihutubia mkutano huo juzi jijini New York, Ramaphosa alisema suluhisho pekee la mgogoro wa Israeli na Palestina ni mataifa mawili yanalotegemea mipaka ya mwaka 1967. Ambapo mipaka hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuanzisha nchi mbili ya Palestina na Israel, lakini lilianzishwa taifa moja tu la Israel.

Licha ya kutaka kusitishwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka, na kuondolewa kwa vizingiti vinavyozuia utawala wa taifa la Palestina ikijumuisha ukuta wa kutenganisha wa Israel, alilinganisha mateso ya Wapalestina na historia ya ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini.

Katika shambulio lake la hasira dhidi ya Israel, ghafla kipaza sauti chake kilizimwa.

 
Ya Nchi yake kuwapatia maisha Bora citizens wake yamemshinda atayaweza ya Israel.

Viongozi wa Africa ni mizingo TU
 
Ngoja tuone akili za hovyo za kitanzania na unafiki wetu kwenye comments!!
 
Yeye alipaswa kuzungumzia ndugu zake weusi wenzake wanao una/kufa Kila kukicha
Drc Congo
Somalia
Sudan
Chad
Mozambique
Et al
Na sio kujipendekeza kwa race zisizo muhusu hata mm ningekua na access ninge zima na umeme kabisa katika ilo jengo..
Aya njoooni wafuga majini
Cc. Webabu
 
Safari ya ukombozi ni ngumu sana lakini ukijitoa unafanikiwa... Usisikilize nyumbu wanaokatisha tamaa
 
Muda wake uliisha.
anaongea mambo ambayo wote pale wanajua.
Alitakiwa aongee mambo ya kwao huko.
 
Sasa yeye nae ana undugu na wapalestina? Aache watu weupe wauane watakavyo! Ya ngoswe amuachie ngoswe mwenyewe!
If you are silent in the situation of injustice, you are supporting the oppressor. Ukikaa kimya pale haki inapo banangwa na kubagazwa basi utakua umechagua kukaa upande wa mnyanyasaji.
 
Yeye alipaswa kuzungumzia ndugu zake weusi wenzake wanao una/kufa Kila kukicha
Drc Congo
Somalia
Sudan
Chad
Mozambique
Et al
Na sio kujipendekeza kwa race zisizo muhusu hata mm ningekua na access ninge zima na umeme kabisa katika ilo jengo..
Aya njoooni wafuga majini
Cc. Webabu
kah?
 
Huyo Ramaphosa ni mnafiki tu.

Wapalestina waliouawa ni 60,000. Wasudan waliouawa ni 1,00,000. Halafu yeye ana huruma zaidi kwa waarabu waliouawa 60,000, lakini anakosa huruma kwa weusi wenzake 1,000,000 waliouawa na wanaendelea kuuawa. Huu ni unafiki mkubwa.

Ramaphosa anauona ubaguzi wa Wayahudi dhidi ya waarabu, lakini anashindwa kuuona ubaguzi wa waafrika wa nchi yake dhidi ya waafrika wa mataifa mengine ambao wanadhambuliwa na kuuawa nchini mwake.
 
Njemba from Africa inaacha issue za Africa imebeba propaganda za muslims kudanganya kwenye mkutano wa UN issue ambazo zipo on news kiprpaganda kila siku, leo uniambie Israel anafanya Genocide wakati tafsir ya Genocide nafahamu, tokea miezi hiyo zaidi ya 27 imepita Arabs wote wangekuwa wameisha kama ni Genocide,

Anayefahamiama na huyo raisi amifikishie ujumbe kuwa ukiwa muongo unafanana na shetani,

Kuongea fact kuna kazi gani? Una deal vipi haswa na magaidi, zaidi ya unafiki tu, Rwanda na DRC pamemshinda, kwake ni uozo wa Xenophobia
 
Back
Top Bottom