Mimi naona hili swala linahitaji busara na uvumilivu, hapa JF asilimia kubwa tunatumia fake ID meaning kwamba kila mtu analinda identity yake na Jamii Forums ina jukumu kubwa pia la kulinda Identity za wanachama wake kwa sababu za kiusalama
Ningeomba tuheshimu hilo, wengi hatufahamiani bali tunakutana tu kwenye mijadala na tunaiacha hapa,linapotokea swala la msiba wa mwanachama ningeomba Jamii foruma iweke utaratibu wa kutangaza mwanachama aliefariki lakini swala la kuwachangisha wanaJF naona kama halijakaa sawa unless kuwe na mfuko unaoratibiwa na JF au moderators
Wale wanaofahamiana nje ya Jamii forum ni vizuri mambo ya nje ya JF yakaishia nje ya JF ili kulinda heshima na usiri wa muhusika, suala la msiba ni la kifamilia pamoja na ndugu wa karibu na marafiki walioshibana na sio suala public, kwa hiyo ningeomba wale marafiki wa karibu wa marehemu washirikiane bega kwa bega na ndugu pamoja na familia lakini tusifike mahali tukaoverreact au kubishana kwa sababu ya hili jambo.kumbuka kila mtu ana jisi anavyochukulia mambo ukizingatia kwamba haya ni mambo ya mtandaoni
Wale watakaoguswa kuchangia watachangia lakini naomba
Maxence Melo hili suala uliangalia mara mbili na utoe mwongozo kama itatokea in future kwa sababu sioni kama limekua handled properly, kuna mapungufu mengi
Hapa jukwaani tuendelee kubaki kama tulivyo na hakuna haja ya kureveal Identity ya mtu au sensitive information misiba inapotokea.
Natoa pole sana kwa wafiwa na ninaomba tuungane kwa watakaoguswa kuchangia