Mkuu Copenhagen
Kuna hili la Velar toleo jipya la 2018 ambalo vitasa vya milango yake vinafunguka kama wataka kuweka CD ndani.
Ila hili la Velar limetengenezwa kistadi pia kwani ukizima injini yake basi huwei kulisukuma kwa kuondoa "handbrake".
Lipo katikati ya Evoque na Sport kwa muundo wake.
Nadhani limewalenga wezi wa magari wakijaribu kuipa wasiweze kuliondoa.
Lakini ukiangalia bei zake zinatofautiana sana wakati Vogue inaanzia pauni 79000, hili la Velar linaanzia pauni 44000.
Hivyo kwa wapenzi wa Land Rover hasa hizi za sport wataweza kuangalia tofauti hiyo ya bei.