Rapcha anajua lakini maana ya freestyle?

Hao madogo wanakalishwa hata na Cannabino (Conboi) anawaficha kabisa kiuandishi.
 
We boya kweli, hakuna mtu ambaye alikuwa anaifanya freestyle ionekane nyepesi kama Ngwair. Alipoibuka Chidi walau akaleta upinzani ila still alikuwa anampa respect.
Hawa madogo wa kizazi cha Young Lunya hawawezi kukuelewa.
 
Mzee mwenzangu hawa watoto wanazingua,sema nini dizasta na mbeya boi chuma wapumzishe,hawa ni kizazi hiki lakini wana kitu fulani cha kusikilizwa
 
Huwa nacheka sana zile nonsense za kudai eti Dizasta ni mkali, these kids don't know shit.
Kwa hawa madogo wa sasa,Dizasta ni mkali mzee,labda ukimfananisha na nguli wa kale,ila kwa kizazi chake huwezi kutomtaja dizasta,labda kama unajambo nae lingine
 
Limetokea wimbi la ivi visanii vya Sasa

Kuandika nyimbo mnazi record mnasiita freestyle

Au ndiyo hamjui maana ya mitindo huru?


Bongo freestyle walikuwa KING ZILAH na NIKKI MBISHI

wengine acheni izo mnajivua nguo
Ukipata time mfuatilie Cado kitengo
 
Limetokea wimbi la ivi visanii vya Sasa

Kuandika nyimbo mnazi record mnasiita freestyle

Au ndiyo hamjui maana ya mitindo huru?


Bongo freestyle walikuwa KING ZILAH na NIKKI MBISHI

wengine acheni izo mnajivua nguo
Unauhakika wanaziandika? Just because zimerocordiwa hainamaana sio freestyle
 
Wasanii wenzie wana-salute Ngwair alikuwa kitu ingine, ukikaa na Majani kawarecordia wengi ila Ngwair ni special kwake.

Wasanii walikuwa wanaandaa mashairi yao, anachukua beat kuifanyia mazoezi mda, alafu One call kwa Ngwair aje studio, mzee akitimba ni kupita na vocal tu.R.I.P Master Ngwair
 
Ngwair overrated na wauza unga na wala unga

Saigon tu alikuwa ana rap vizuri kuliko mashauzi ngwair
naunga mkono hoja,mangwea alikuwa overrated sana kuzidi uwezo wake na hii inatokana na kupambwa na kupewa promo na media.media ikikupamba as long as una uwezo mdogo utaonekana mkubwa,same apply to marioo huyu dogo kakuzwa sana ila muda utaongea maana speed ya kuporomoka itamshangaza yeye mwenyewe na fans wake na mwisho wa siku akiangalia jina lilivyokuwa kubwa na mafanikio kidogo aliyopata ataishia kuwa mtumia madawa ya kulevya kama ilivyokuwa kwa mangwea.MUDA UTAONGEA
 
Acha chuki binafsi. Hadi Yesu anarudi hatatokea kama ngwea Tanzania. Madawa ni inshu binafsi ya mtu. Wasanii wote wakubwa na wakongwe wanauogopa hadi mzimu wa ngwea hadi leo. Maana jamaa ukimshirikisha kama msanii unajitambua labda umpe chorus ila ukimpa verse kashakufunika. Ngwea hajawahi kushika peni kuandika mistari. Sikiliza mahojiano ya KR na juma Nature usikilize wanachoongea. Muulize prof j kwenye wimbo wa Una, yeye mwenyewe anakiri kuogopa kumpa verse ngwea akaona ampe chorus, Fid Q kama tunavyojua alifuta verse, chid benz alivunja chupa akampiga marehemu baada yakuzidiwa kuchana, King zilla( RIP) studio aliishiwa pumzi akabaki anaropoka uamerika mwingi (you know) usio na maana. Ngwea ukimshirikisha kwenye RNB anauwezo wa kubadilika nae anaendana na RNB sikiliza ngoma zake na Steve RNB. ASikiliza freestyle aliyopiga XXL Miaka ile clouds FM akiwa na Quick ROCK na izzo bussiness ngwea anapewa topic anaflow kuhusu topic aliyopewa. Albums alizotoa ngwea ni miongoni mwa album bora kutokea. Kwenye hizo album hajarudia nyimbo za watu. Vijana kubalini ukweli, freestyle ya sasa msanii ukimwita radio station tofauti lazma atarudia mistari tu aliyochana radio iliyopita, kitu ambacho ngwair alikua hafanyi ujinga huo.
 
Ngwair alikuwa na mshairi mepesi sana
Ngwair got Swagz... Jamaa alikuwa anafreestyle with Swagz kitu ambacho hakuna Emcee yoyote Kwasasa anafanya.


Freestylers WA sasa hivi MTU anarap kama anafukuzwa ilimradi atoe maneno Tu.

Hebu cheki hizi
 
Yani Albert Mangwair kwamba alikuwa overrated....


Nyie madogo mna laana ndio maana nashangaa sasa hivi madogo mnahangaika kitaa Hamna mbele walA nyuma
 
Marioo is overrated big time, hilo nakubaliana nalo sana.
 
Albert Keneth Mangwea my favourite Artist of all Time

Bongo hakuna msanii nilimkubali na ntaendelea kumkubali km Albert Keneth Mangwea


Uwezo alio nao Ngwea upande wa rap Music kwa bongo sijawahi kuona

Idea za nyimbo zake mpaka leo zimebaki za kipekee sana

Huyu jamaa alibarikiwa sana upande wa sanaa ya rap music


Continue to rest in peace Cowbama
 
Ngwea kwa wakati wake ndio alikua mkali..
Lets talk now kwa ishu ya mitindo huru (freestyle) fundi wao. Ni toxic
Kwanini ni toxic maana anaenda na hadhira vizuri na anazingatia nini mashabiki wanataka.
Kuhusu midamuuu(kitengo) anajua ila awezi kwenda na hadhira maana anatukana mno
Raptcha na ma young wote freestyle hawawezi hata kidogo ila punchlines wapo vizuri
Ukitaka kulinganisha nani mkali kati ya cado na ngwea kwa freestyle utakua una shida maana ni watu wawili tofauti kwa wakati tofauti..
Assume ngwea angekua hai mpaka leo kwa mtiririko ule angemkalisha cado au toxic..
Sio mnabisha humu wakati hamfatili Bato zinavofanyika. Kuna watu wanatembe freestyle sio poa.
Muulizeni unju alichofanya na cado..
Muulizeni cado alichofanywa na toxic
Muulizeni toxic alichofanywa na stan wa ryms

Ngwea alikua best kwa kipindi chenu hiko.
Now zama hizi ata angekuepo kwa ishu ya freestyle asingegusa hawa madogo... Naongelea freestyle sio punchlines
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…