Rashid Makwiro (Chid Benz) hali yake ni tete kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya

Wa kumsaidia Chidi ni yeye mwenyewe. Asitegemee mtu sababu sisi watu ni wanafiki. Akiamua mwenyewe atapona. Nimeshuhudia watu waliofika Hali mbaya zaidi ya hapo lakini.sasa wamepona na Hali ni nzuri ya kumshangaza kila mtu. Chaguo ni lake yeye mwenyewe.
 
SERIKALI ISIMDEKEZE CHID BENZ AU RAY C. WAKAMATWE ASWEKWE CELLO.
HUKO WATAONESHA WANAPO NUNUA HIZO NGADA NA ATAACHA AKISWEKWA MIAKA 3 KWA KOSA LA MADAWA YA KULEVYA!
NA WENGINE WATAOGOPA.
Hivi unadhani serikali haiwafahamu wauza unga.? Kila waziri akiteuliwa Kwenye hiyo wizara hupiga kelele mwanzo apate umaarufu kisha hukaa kimya kama hajui...
Ushawahi mwona mwingulu anahangaika na wauza unga..
Some time huwa nawaza labda ni moja ya chanzo cha mapato ya ndani.. Tumbua tumbua yooooote.. Hakuna Drug Lord hata mmoja
 
Daaaaaaaah me naona apigwe sindano ya sumu tuuu akapumzike.... Ye mwenyewe kashachoka kuishi inaonekana
 
Rapa Nikki Mbishi amedai Chid Benz hafai kusaidiwa sababu ya ujeuri wake na walishamsaidia kabla ya Babu Tale kumpeleka Sober House ila akashindikana
Mama yake mwenyewe amehangaika nae amemshindwa so ni bora akaachwa nature ichukue mkondo wake
 
Swala la chid Benz linahitaji kucomittment kubwa sana sio la kujaribu tu na kuacha kama kina Babu Tale walivyofanya[emoji48]
 
"Chid Benzi "anatushangaa tunavyomshangaa

NI zaidi ya kujikuta juu ya kitanda na msichana unayempenda kuliko wote duniani. Ni zaidi ya kutazama bao la ushindi la timu yako katika dakika za majeruhi katika mechi muhimu. Yote haya hayazidi starehe ya kubwia unga.

Sahau kuhusu bia, sigara, Sahau kuhusu kila starehe. Inatajwa kuwa hakuna starehe kama unga. Na sasa Watanzania wanaendelea kumshangaa mtu anayeitwa Chid Benz. Mwanamuziki hodari wa kizazi hiki katika zile staili za vijana za muziki wa kufokafoka.

Chid anateketea. Mwili wake kwa sasa ni kama mahindi ya shambani yaliyoliwa na nzige. Mwili wake ni kama kama gari lililoungua likaisha. Amebaki mifupa tu. Unaweza kupishana naye bila ya kumfahamu kama bado kichwani unatembea na taswira ya yule Chid Benzino mwenye mashavu manene, miwani usoni, na taulo shingoni.

Wasichofahamu watu wengi ni ukweli kwamba wakati sisi tukiendelea kumshangaa Chid, kumbe yeye ndiye anatushangaa zaidi sisi. Anatushangaa kwanini hatuungani naye katika starehe yake tamu. Anatushangaa kwanini hatupo katika safari yake ya kubembea.

Kwanini anatushangaa? Ninesema hapo juu hakuna starehe tamu zaidi ya unga. Kitu cha muhimu hili ni kutoonja starehe yenyewe. Ukionja hautabaki. Hata Chid si ajabu zamani alikuwa analaani wala unga. Kosa kubwa alilifanya katika kuonja tu. Ukionja ni vigumu kutoka katika mtego.

Ni hapo ndipo lilipo tatizo la Chid na watumiaji wengine. Kikubwa wanachotakiwa kukifanya kuachana na unga hawawezi kukifanya. Kitu cha kwanza kabisa ni kuukana utamu wake. Kuukana utamu wake ni kama kuikana nafsi yako. Hapa ndipo ilipo vita kubwa ya kuacha.

Kwanza inabidi uone mapungufu makubwa ya unga lakini kama ukilegeza moyo kamwe hauwezi. Kwa mfano, leo Chid hajioni mchafu, hajioni amekonda, hajioni amepoteza nuru. Utamu wa unga umezidi akili ya kujitafakari (self assessment). Ikifika hapo kazi inakuwa nzito zaidi.

Kumpeleka Chid katika vituo vya matibabu (rehabilitation centres) ni kupoteza muda mpaka pale moyo wake utakapoanza kujifanyia self assessment kuwa amepotea, anahitaji msaada na anachukia unga. Akifika hapo atashinda vita.

Chukulia kwamba familia yako imekuomba mtoke out na uwape muda wa kuwa na wewe. Wanaweza na tabia yako ya kupenda mpira kuliko wewe. Unawakubalia walichokuomba. Lakini wanakupeleka katika hoteli ambayo watu wanatazama mpira. Lazima moyo wako utakuwa unafuatilia kwa karibu matokeo huku mwili wako ukiwa mezani na familia.

Kitu cha aina hiki kinaitwa addiction. Ndipo alipofika Chid. Kama ambavyo wewe unashangaa kwanini mtu hapendi mpira au muziki, basi na ndivyo Chid anavyotushangaa kwanini na sisi wengine hatupendi unga. Alipofikia yeye na sisi wengine wote tumefika ingawa sisi tuna starehe tofauti na yeye.

Kabla ya matibabu kitu cha msingi kwa Chid ni kukutana na mwanasaikolojia wa kumshawishi aelewe kwamba kitu anachokiona kitamu kumbe sio kitamu. Nani anaiweza kazi hii? Ni kazi ngumu. Ndio maana washkaji zake walipompeleka Bagamoyo alitoroka na kuendelea na starehe yake kwa sababu hakuwa tayari kuona utamu wake unaitwa uchungu.

Mwisho wa Chid? Sitaki kuingilia kazi ya Mwenyezi Mungu lakini mwisho wake unatabirika kiurahisi zaidi pengine kuliko mwisho wa watu wengi tunaomshangaa. Sisi tuna siku zetu za ahadi na tunaweza kuondoka mapema hapa duniani kuliko yeye, hata hivyo tutaondoka kwa vifo visivyotabirika.

Chid anaweza kufuata njia za akina Whitney Houston tu. Watu wengi wa aina yake huwa inatokea tunawaokota mtaroni au chumbani wakiwa wametangulia Mbele ya haki. Inatokea huwa wanajidunga kupitiliza, au kuliko miili yao inavyoweza kuhimili uzito wa dawa aliyotumia siku hiyo. Kwa kiingereza cha matumizi ya unga wanaita overdosing.

Hili sio la kuombea lakini maisha ya kufichana yamepita zamani jamani. Kama tunahitaji lisitokee basi ni kwa Chid mwenyewe kumjua adui yake na kupambana naye. Adui wa Chid sio unga. Adui wa Chid ni akili yake mwenyewe. Unga upo tu, lakini mbona wengi hatutumii?

Ana bahati mbaya ameangukia katika starehe ambayo inammaliza. Sisi wengine tuna matatizo kama yake ya kuendekeza starehe lakini bahati nzuri huwa hazitumalizi. Starehe ya kubishana nani zaidi ya Lionel Messi na Ronaldo haiwezi kutumaliza kwa urahisi.
 
Hiyo commitment ya kuhanga na huyo jamaa ataweza mzazi wake tu ila sio mtu mwingine.

Kumsaidia mtu ambaye hayupo tayari kuacha hayo madude ni kazi sana , Nina mjomba wangu mpaka leo familia imemsusa yupo TAZARA pale anapiga debe na anakula ngada kama kawaida. Tulimpeleka sober house ya zanzibar huko tukishirikiana na mama zangu ila akajifanya kawa chizi kule hivyo akawa analeta vurugu wakatupigia simu na barua ya rufaa kuwa tumepeleke muhimbili kitengo cha wenye magonjwa ya akili. Tulimpeleka daktari alivyofanya mahjiano naye tu akasema huyu hana tatizo la akili na kweli alivyorudi nyumbani akatulia ila alikuwa anasumbua kwa kupenda kuvuta sigara kila mara.
Siku nyingine ukikaa naye anasema anajuta kwa nini alijiunga na hii tabia ya uvutaji wa ngada mpaka mimi huwa ananishauri nisije kuthubutu kwani inamadhara makubwa sana.
Ila baadae akaona nyumbani kwangu kama anabanwa sana akatoroka sasa hivi anapolala anapajua yeye mwenyewe na hivi hana mama ndugu zake wote wamemsusa yupo TZARA pale stand ya Mbagala anapiga debe.

So kwa Chid kwa sababu mama yake yupo wacha tumuombee huyu mama aishi muda mrefu zaidi ili amsaidie mtoto wake lakini kutegemea wahisani kumsaidia itakuwa ngumu sana.
Swala la chid Benz linahitaji kucomittment kubwa sana sio la kujaribu tu na kuacha kama kina Babu Tale walivyofanya[emoji48]
 
Chid Benzi anatushangaa tunavyomshangaa

Na Edo Kumwembe
NI zaidi ya kujikuta juu ya kitanda na msichana unayempenda kuliko wote duniani. Ni zaidi ya kutazama bao la ushindi la timu yako katika dakika za majeruhi katika mechi muhimu. Yote haya hayazidi starehe ya kubwia unga.

Sahau kuhusu bia, sigara, Sahau kuhusu kila starehe. Inatajwa kuwa hakuna starehe kama unga. Na sasa Watanzania wanaendelea kumshangaa mtu anayeitwa Chid Benz. Mwanamuziki hodari wa kizazi hiki katika zile staili za vijana za muziki wa kufokafoka.

Chid anateketea. Mwili wake kwa sasa ni kama mahindi ya shambani yaliyoliwa na nzige. Mwili wake ni kama kama gari lililoungua likaisha. Amebaki mifupa tu. Unaweza kupishana naye bila ya kumfahamu kama bado kichwani unatembea na taswira ya yule Chid Benzino mwenye mashavu manene, miwani usoni, na taulo shingoni.

Wasichofahamu watu wengi ni ukweli kwamba wakati sisi tukiendelea kumshangaa Chid, kumbe yeye ndiye anatushangaa zaidi sisi. Anatushangaa kwanini hatuungani naye katika starehe yake tamu. Anatushangaa kwanini hatupo katika safari yake ya kubembea.

Kwanini anatushangaa? Ninesema hapo juu hakuna starehe tamu zaidi ya unga. Kitu cha muhimu hili ni kutoonja starehe yenyewe. Ukionja hautabaki. Hata Chid si ajabu zamani alikuwa analaani wala unga. Kosa kubwa alilifanya katika kuonja tu. Ukionja ni vigumu kutoka katika mtego.

Ni hapo ndipo lilipo tatizo la Chid na watumiaji wengine. Kikubwa wanachotakiwa kukifanya kuachana na unga hawawezi kukifanya. Kitu cha kwanza kabisa ni kuukana utamu wake. Kuukana utamu wake ni kama kuikana nafsi yako. Hapa ndipo ilipo vita kubwa ya kuacha.

Kwanza inabidi uone mapungufu makubwa ya unga lakini kama ukilegeza moyo kamwe hauwezi. Kwa mfano, leo Chid hajioni mchafu, hajioni amekonda, hajioni amepoteza nuru. Utamu wa unga umezidi akili ya kujitafakari (self assessment). Ikifika hapo kazi inakuwa nzito zaidi.

Kumpeleka Chid katika vituo vya matibabu (rehabilitation centres) ni kupoteza muda mpaka pale moyo wake utakapoanza kujifanyia self assessment kuwa amepotea, anahitaji msaada na anachukia unga. Akifika hapo atashinda vita.

Chukulia kwamba familia yako imekuomba mtoke out na uwape muda wa kuwa na wewe. Wanaweza na tabia yako ya kupenda mpira kuliko wewe. Unawakubalia walichokuomba. Lakini wanakupeleka katika hoteli ambayo watu wanatazama mpira. Lazima moyo wako utakuwa unafuatilia kwa karibu matokeo huku mwili wako ukiwa mezani na familia.

Kitu cha aina hiki kinaitwa addiction. Ndipo alipofika Chid. Kama ambavyo wewe unashangaa kwanini mtu hapendi mpira au muziki, basi na ndivyo Chid anavyotushangaa kwanini na sisi wengine hatupendi unga. Alipofikia yeye na sisi wengine wote tumefika ingawa sisi tuna starehe tofauti na yeye.

Kabla ya matibabu kitu cha msingi kwa Chid ni kukutana na mwanasaikolojia wa kumshawishi aelewe kwamba kitu anachokiona kitamu kumbe sio kitamu. Nani anaiweza kazi hii? Ni kazi ngumu. Ndio maana washkaji zake walipompeleka Bagamoyo alitoroka na kuendelea na starehe yake kwa sababu hakuwa tayari kuona utamu wake unaitwa uchungu.

Mwisho wa Chid? Sitaki kuingilia kazi ya Mwenyezi Mungu lakini mwisho wake unatabirika kiurahisi zaidi pengine kuliko mwisho wa watu wengi tunaomshangaa. Sisi tuna siku zetu za ahadi na tunaweza kuondoka mapema hapa duniani kuliko yeye, hata hivyo tutaondoka kwa vifo visivyotabirika.

Chid anaweza kufuata njia za akina Whitney Houston tu. Watu wengi wa aina yake huwa inatokea tunawaokota mtaroni au chumbani wakiwa wametangulia Mbele ya haki. Inatokea huwa wanajidunga kupitiliza, au kuliko miili yao inavyoweza kuhimili uzito wa dawa aliyotumia siku hiyo. Kwa kiingereza cha matumizi ya unga wanaita overdosing.

Hili sio la kuombea lakini maisha ya kufichana yamepita zamani jamani. Kama tunahitaji lisitokee basi ni kwa Chid mwenyewe kumjua adui yake na kupambana naye. Adui wa Chid sio unga. Adui wa Chid ni akili yake mwenyewe. Unga upo tu, lakini mbona wengi hatutumii?

Ana bahati mbaya ameangukia katika starehe ambayo inammaliza. Sisi wengine tuna matatizo kama yake ya kuendekeza starehe lakini bahati nzuri huwa hazitumalizi. Starehe ya kubishana nani zaidi ya Lionel Messi na Ronaldo haiwezi kutumaliza kwa urahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…