Rashid Makwiro (Chid Benz) hali yake ni tete kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya

Babutale where are you?

Wabongo wanafiki sana toka lini mtu kakaa sober house only one month, kesharushwa studio?!?

Wimbo haujahit babutale kala kona..mxiuuu
Acha kuropoka,

Chid katoroka sober house, Tale amezira amesema hawezi kumsaidia tena mtu aliyetoroka sober house.

Sasa hivi ni zamu yako tunaomba umsaidie.
 
Hapana,huyo sio Chid Benz ninayemfahamu mimi,yaani kuanzia rangi ya Ngozi mpaka sura,kichwa chake, bila kisahau kile kichogo chake kwa nyuma kilivyokaa, NAKATAA KWA NGUVU ZOTE KWAMBA HUYO SIO CHID NENZ na ningependa pindi mwenyewe akiona hii post akufungulie Kesi ya udharirishaji na Jamii Administration watoe ushirikiano ukamatwe
 
Hebu pitie na hii video mje mfute comments zenu, mtoe ushauri wa maana

Hiyo video nimeiangalia kwa makini bado nakataa huyo sio CHID BENZ, na nitamtafuta mwenyewe kisha nitatupia hapa jukwaani, weka video inayomuonyesha sura yake vizuri, nakuhakikishia mtoa mada endapo itathibitika taarifa yako ya uongo nitahakikisha kesi ya UCHOCHEZI unaipata, maana nina wasi wasi umetumwa, hiyo sauti tu ya kuchana jamaa anaonekana anamuiga CHID BENZ
 
Haihitaji huruma ya mtu no yy kukaa na kujiangalia anatoka WAP na non mwisho wake so vingine
 
Ninachojifunza ni kuwa serikali yetu hii haiwezi kupambana na mafisadi na wauza unga. Inaishia kutisha watumishi tuu, lakini wale wezi halali bado wapo hukohuko kwenye chama na ubunge, na wauza unga wote wamesharudi mitaani. Ni yaleyale, mtu keshatuliza mzuka, nothing will ever change.
 
Chid Benzi anatushangaa tunavyomshangaa

Na Edo Kumwembe
NI zaidi ya kujikuta juu ya kitanda na msichana unayempenda kuliko wote duniani. Ni zaidi ya kutazama bao la ushindi la timu yako katika dakika za majeruhi katika mechi muhimu. Yote haya hayazidi starehe ya kubwia unga.

Sahau kuhusu bia, sigara, Sahau kuhusu kila starehe. Inatajwa kuwa hakuna starehe kama unga. Na sasa Watanzania wanaendelea kumshangaa mtu anayeitwa Chid Benz. Mwanamuziki hodari wa kizazi hiki katika zile staili za vijana za muziki wa kufokafoka.

Chid anateketea. Mwili wake kwa sasa ni kama mahindi ya shambani yaliyoliwa na nzige. Mwili wake ni kama kama gari lililoungua likaisha. Amebaki mifupa tu. Unaweza kupishana naye bila ya kumfahamu kama bado kichwani unatembea na taswira ya yule Chid Benzino mwenye mashavu manene, miwani usoni, na taulo shingoni.

Wasichofahamu watu wengi ni ukweli kwamba wakati sisi tukiendelea kumshangaa Chid, kumbe yeye ndiye anatushangaa zaidi sisi. Anatushangaa kwanini hatuungani naye katika starehe yake tamu. Anatushangaa kwanini hatupo katika safari yake ya kubembea.

Kwanini anatushangaa? Ninesema hapo juu hakuna starehe tamu zaidi ya unga. Kitu cha muhimu hili ni kutoonja starehe yenyewe. Ukionja hautabaki. Hata Chid si ajabu zamani alikuwa analaani wala unga. Kosa kubwa alilifanya katika kuonja tu. Ukionja ni vigumu kutoka katika mtego.

Ni hapo ndipo lilipo tatizo la Chid na watumiaji wengine. Kikubwa wanachotakiwa kukifanya kuachana na unga hawawezi kukifanya. Kitu cha kwanza kabisa ni kuukana utamu wake. Kuukana utamu wake ni kama kuikana nafsi yako. Hapa ndipo ilipo vita kubwa ya kuacha.

Kwanza inabidi uone mapungufu makubwa ya unga lakini kama ukilegeza moyo kamwe hauwezi. Kwa mfano, leo Chid hajioni mchafu, hajioni amekonda, hajioni amepoteza nuru. Utamu wa unga umezidi akili ya kujitafakari (self assessment). Ikifika hapo kazi inakuwa nzito zaidi.

Kumpeleka Chid katika vituo vya matibabu (rehabilitation centres) ni kupoteza muda mpaka pale moyo wake utakapoanza kujifanyia self assessment kuwa amepotea, anahitaji msaada na anachukia unga. Akifika hapo atashinda vita.

Chukulia kwamba familia yako imekuomba mtoke out na uwape muda wa kuwa na wewe. Wanaweza na tabia yako ya kupenda mpira kuliko wewe. Unawakubalia walichokuomba. Lakini wanakupeleka katika hoteli ambayo watu wanatazama mpira. Lazima moyo wako utakuwa unafuatilia kwa karibu matokeo huku mwili wako ukiwa mezani na familia.

Kitu cha aina hiki kinaitwa addiction. Ndipo alipofika Chid. Kama ambavyo wewe unashangaa kwanini mtu hapendi mpira au muziki, basi na ndivyo Chid anavyotushangaa kwanini na sisi wengine hatupendi unga. Alipofikia yeye na sisi wengine wote tumefika ingawa sisi tuna starehe tofauti na yeye.

Kabla ya matibabu kitu cha msingi kwa Chid ni kukutana na mwanasaikolojia wa kumshawishi aelewe kwamba kitu anachokiona kitamu kumbe sio kitamu. Nani anaiweza kazi hii? Ni kazi ngumu. Ndio maana washkaji zake walipompeleka Bagamoyo alitoroka na kuendelea na starehe yake kwa sababu hakuwa tayari kuona utamu wake unaitwa uchungu.

Mwisho wa Chid? Sitaki kuingilia kazi ya Mwenyezi Mungu lakini mwisho wake unatabirika kiurahisi zaidi pengine kuliko mwisho wa watu wengi tunaomshangaa. Sisi tuna siku zetu za ahadi na tunaweza kuondoka mapema hapa duniani kuliko yeye, hata hivyo tutaondoka kwa vifo visivyotabirika.

Chid anaweza kufuata njia za akina Whitney Houston tu. Watu wengi wa aina yake huwa inatokea tunawaokota mtaroni au chumbani wakiwa wametangulia Mbele ya haki. Inatokea huwa wanajidunga kupitiliza, au kuliko miili yao inavyoweza kuhimili uzito wa dawa aliyotumia siku hiyo. Kwa kiingereza cha matumizi ya unga wanaita overdosing.

Hili sio la kuombea lakini maisha ya kufichana yamepita zamani jamani. Kama tunahitaji lisitokee basi ni kwa Chid mwenyewe kumjua adui yake na kupambana naye. Adui wa Chid sio unga. Adui wa Chid ni akili yake mwenyewe. Unga upo tu, lakini mbona wengi hatutumii?

Ana bahati mbaya ameangukia katika starehe ambayo inammaliza. Sisi wengine tuna matatizo kama yake ya kuendekeza starehe lakini bahati nzuri huwa hazitumalizi. Starehe ya kubishana nani zaidi ya Lionel Messi na Ronaldo haiwezi kutumaliza kwa urahisi.
serikali ikamate wauza unga maana hawa ndo wanaoharibu taifa la leo ba kesho hasa vijana
this is why mataifa kama china wanaua wauza madawa ya kulevya kwa sababu ni bora kumwondoa mmoja anayesupply ambaye kumpata inawezekana kuliko kupoteza a lot of resource dealing with hawa watu wa mwisho
 
Mbona vijana wengi wanatumia? Huyo ni nani mpaka awe kichwa cha habari?muache aendelee kutumia...kwa sababu yanapatikana...ndio maaana anatumia......
 
Hivi kama Chidi kwa afya ile anajua pa kununua madawa, polisi kweli hawajui anayeuza? Tanzania hakuna vita dhidi ya madawa ya kulevya!
 
Chid Benzi anatushangaa tunavyomshangaa

Na Edo Kumwembe
NI zaidi ya kujikuta juu ya kitanda na msichana unayempenda kuliko wote duniani. Ni zaidi ya kutazama bao la ushindi la timu yako katika dakika za majeruhi katika mechi muhimu. Yote haya hayazidi starehe ya kubwia unga.

Sahau kuhusu bia, sigara, Sahau kuhusu kila starehe. Inatajwa kuwa hakuna starehe kama unga. Na sasa Watanzania wanaendelea kumshangaa mtu anayeitwa Chid Benz. Mwanamuziki hodari wa kizazi hiki katika zile staili za vijana za muziki wa kufokafoka.

Chid anateketea. Mwili wake kwa sasa ni kama mahindi ya shambani yaliyoliwa na nzige. Mwili wake ni kama kama gari lililoungua likaisha. Amebaki mifupa tu. Unaweza kupishana naye bila ya kumfahamu kama bado kichwani unatembea na taswira ya yule Chid Benzino mwenye mashavu manene, miwani usoni, na taulo shingoni.

Wasichofahamu watu wengi ni ukweli kwamba wakati sisi tukiendelea kumshangaa Chid, kumbe yeye ndiye anatushangaa zaidi sisi. Anatushangaa kwanini hatuungani naye katika starehe yake tamu. Anatushangaa kwanini hatupo katika safari yake ya kubembea.

Kwanini anatushangaa? Ninesema hapo juu hakuna starehe tamu zaidi ya unga. Kitu cha muhimu hili ni kutoonja starehe yenyewe. Ukionja hautabaki. Hata Chid si ajabu zamani alikuwa analaani wala unga. Kosa kubwa alilifanya katika kuonja tu. Ukionja ni vigumu kutoka katika mtego.

Ni hapo ndipo lilipo tatizo la Chid na watumiaji wengine. Kikubwa wanachotakiwa kukifanya kuachana na unga hawawezi kukifanya. Kitu cha kwanza kabisa ni kuukana utamu wake. Kuukana utamu wake ni kama kuikana nafsi yako. Hapa ndipo ilipo vita kubwa ya kuacha.

Kwanza inabidi uone mapungufu makubwa ya unga lakini kama ukilegeza moyo kamwe hauwezi. Kwa mfano, leo Chid hajioni mchafu, hajioni amekonda, hajioni amepoteza nuru. Utamu wa unga umezidi akili ya kujitafakari (self assessment). Ikifika hapo kazi inakuwa nzito zaidi.

Kumpeleka Chid katika vituo vya matibabu (rehabilitation centres) ni kupoteza muda mpaka pale moyo wake utakapoanza kujifanyia self assessment kuwa amepotea, anahitaji msaada na anachukia unga. Akifika hapo atashinda vita.

Chukulia kwamba familia yako imekuomba mtoke out na uwape muda wa kuwa na wewe. Wanaweza na tabia yako ya kupenda mpira kuliko wewe. Unawakubalia walichokuomba. Lakini wanakupeleka katika hoteli ambayo watu wanatazama mpira. Lazima moyo wako utakuwa unafuatilia kwa karibu matokeo huku mwili wako ukiwa mezani na familia.

Kitu cha aina hiki kinaitwa addiction. Ndipo alipofika Chid. Kama ambavyo wewe unashangaa kwanini mtu hapendi mpira au muziki, basi na ndivyo Chid anavyotushangaa kwanini na sisi wengine hatupendi unga. Alipofikia yeye na sisi wengine wote tumefika ingawa sisi tuna starehe tofauti na yeye.

Kabla ya matibabu kitu cha msingi kwa Chid ni kukutana na mwanasaikolojia wa kumshawishi aelewe kwamba kitu anachokiona kitamu kumbe sio kitamu. Nani anaiweza kazi hii? Ni kazi ngumu. Ndio maana washkaji zake walipompeleka Bagamoyo alitoroka na kuendelea na starehe yake kwa sababu hakuwa tayari kuona utamu wake unaitwa uchungu.

Mwisho wa Chid? Sitaki kuingilia kazi ya Mwenyezi Mungu lakini mwisho wake unatabirika kiurahisi zaidi pengine kuliko mwisho wa watu wengi tunaomshangaa. Sisi tuna siku zetu za ahadi na tunaweza kuondoka mapema hapa duniani kuliko yeye, hata hivyo tutaondoka kwa vifo visivyotabirika.

Chid anaweza kufuata njia za akina Whitney Houston tu. Watu wengi wa aina yake huwa inatokea tunawaokota mtaroni au chumbani wakiwa wametangulia Mbele ya haki. Inatokea huwa wanajidunga kupitiliza, au kuliko miili yao inavyoweza kuhimili uzito wa dawa aliyotumia siku hiyo. Kwa kiingereza cha matumizi ya unga wanaita overdosing.

Hili sio la kuombea lakini maisha ya kufichana yamepita zamani jamani. Kama tunahitaji lisitokee basi ni kwa Chid mwenyewe kumjua adui yake na kupambana naye. Adui wa Chid sio unga. Adui wa Chid ni akili yake mwenyewe. Unga upo tu, lakini mbona wengi hatutumii?

Ana bahati mbaya ameangukia katika starehe ambayo inammaliza. Sisi wengine tuna matatizo kama yake ya kuendekeza starehe lakini bahati nzuri huwa hazitumalizi. Starehe ya kubishana nani zaidi ya Lionel Messi na Ronaldo haiwezi kutumaliza kwa urahisi.
Umeongea kama watu 1000 eddo
 
Starehe ya unga ni sawa na mtu uko ndani ya ndege sasa umeachiwa unaelea angani, tabu ukifika chini unagusa ardhi kwa kishindo, kishindo kwa mbwiya unga ni pale unga umeisha mwilini sasa anahitaji kuweka dose ingine.
 
Back
Top Bottom