Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Status
Not open for further replies.

Icadon, ahsante wa Uzalendo wako wa dhati. Inaonekana na wewe huna nia ya kufunga magoli ya vikeki (sijui Wamarekani wameutoa wapi huu msemo wa ku score brownie points!)

Watu walishaanza kudhani kuna majibu ya ukahika hapa na kwamba sijui ninachokisema. Angekuwa mwingine umempa jibu hilo angefanya tafrija ya dhihaka. Niliwahi kukubali kosa hapa JF watu wakashtuka mno. Wakaniita 'Juha kama Jiwe.' Hapa nika take a chance baada ya kujiuliza mara tatu tatu. Lakini ndivyo nilivyo, nikaona niseme tu

Nakusaluti.
 

Mwnkjj;

Tumesha jadili yote hayo. Tukaenda mpaka kwenye sheria za 1970 zinazo toa maana ya maneno yaliyo tumika kwenye sheria ya 1996. Ukipata muda pitia pitia matundiko ya nyuma kidogo, kurasa mbili tatu hivi.
 
1. Icadon

Ahasante kwa maelezo yako,
Naomba nikuulize nini hasa kazi ya wale agents wa TISS pale BOT na kwenye mabenki mengine na kwenye mashirika yote ya umma?

2.
Sina uhakika.

Full stop!


Mkuu Icadon, Ubarikiwe tu mkuu, yaaani I love Jambo Forums!
 
Kwanza heshima zenu wakuu kwa uzalendo mnaoonekana kuwa nao na pia mnavyoonekana kuelewa na kutueleza kazi za Idara ya Usalama wa Taifa na kufikia kutaka RO ajiuzulu kwa kuwa muonavyo ninyi hakutekeleza kazi hizo. Ni vizuri mkatueleza pia kazi za mshororo wa mfumo mzima wa serikali na uongozi wa nchi ili muweze kuhitimisha ni nani ajiuzulu na kwa sababu ipi kwa kuangalia tu yale mnayoyajuwa ya uwaziri wa Chenge, EPA, Richmond, ANBEN, Mtera etc. Wengi kama si nyote mnajinadi kuwa si wana usalama, sasa kama hivyo ndivyo manajuwaje kama haya mafichuo yote yanayotokea yakifuatilia pia mambo ya hapo nyuma, kabla ya RO si matokeo ya kazi ya idara hiyo.

Matatizo yaliyorithiwa kutoka awamu za nyuma hususani ile ya tatu si siri. Je usalama ulifanya nini kuyazuwia wakati huo hata yafikie kujiri leo? Ninashindwa kuelewa vile wazalendo wa hali ya juu hivyo wasivyoweza kupambanisha haya na kukiri mabadiliko na badala yake kuweka mbele "kujiuzulu" kwa RO bila ya kutudhihirishia kutohusika kwake katika kudhihirisha mabaya haya. Sidhani kuwa matarajiyo yao ya dhati ni kutaka yeye na timu yake nzima ya usalama wa taifa iingie hapa kujigamba vile wanavyoyafuatilia mambo haya na vile walivyoyafikisha hapa tulipo kuweza kujuwa hujuma zinazofanywa na kutowa njia na wepesi wa kuzifuatilia.

Kumsakama RO wakati mafisadi wanafichuka badala ya kusaidia kufichuwa mafisadi hao pamoja na kuwavuta mikanda wajiuzulu na warudishe walichochukuwa aidha kwa hiari yao au kwa nguvu ya dola inatia hisia za kupoteza lengo. Mafisadi wana mbinu nyingi na haya ya radar, EPA na mengi makubwa siyo ya awamu hii. Kama RO ni tishio wa mafisadi basi kwao wao kujiuzulu RO ingekuwa ni afueni kwao na pengine ndio nia za mjadala huu. Mwenye macho haambiwi tazama.
 
Kukuonyesha kwamba nia yangu ni majadiliano ya kujengana nitasema kitu ambacho ni wachache hapa JF, na labda hakuna, anaweza kukisema: Sina uhakika.


Mimi nakusifu na kukupongeza kwa kuwa muwazi maana watu wengine muda mwingine hupindisha habari ili washinde mada.

Ila kutojua hili labda ndio chanzo cha kumuona huyu bwana yuko sahihi.Na hapa there is nothing personal about RO ila ukweli ni kwamba usalama wako vitengo vyote vya pesa na ndio maana muda mwingi si lazima kwa wao kuomba kibali kujua account ya mtu hapa nchini.Na hii inatumika duniani kwote na ndio maana wahalifu wengi walio alert uchimbia hela zao sio bank.
RO unachoweza kutetea ni kwamba si mzembe taharifa yeye inawezekana anafikisha /file tena anaweza kwenda moja kwa moja kwa rais kuruka waziri au kiongazi yeyote aliye juu yake,ila act inasema yeye si mtekelezaji.
Ila kama Kiongozi ukiona mambo yanaenda kinyume na kiapo(maslahi ya nchi) unajiuzuru si lazima uwe wewe umekosea ili ujiuzuru.Juzi juzi General mmoja muhimu marekani kajiuzuru kwa kuona mambo yanaenda sivyo .
 

Kuhani,

Kwa mtaji huu wa uhaba na mapungufu ya Sheria hii ya mwaka 1970 unatuambia wazi kuwa Serikali itaendelea kuruka vihunzi vya uwajibikaji kwa kutumia maana ya maneno na vipengele vya sheria na katiba?

Sisi tunachidai ni kuwa yeye kama Afisa Mkuu mtendaji wa Usalama wa Taifa alipokuwa London, je hakutumika na Serikali au kuipa Serikali ushauri wa ki-usalama (Radar ni kitu cha Usalama) kuhusiana na manunuzi haya ya Radar?

Ikiwa alijua wazi kuwa kuna mpango (mkuu wa Usalama wa kituo ambako bidhaa inanunuliwa na sia ajabu alikwenda angalia utengenezwaji) wa Serikali kununua Radar, na hata kusikika kwa mabishano katika Bunge la Uingereza kuhusiana na Ununuzi huu, je kwa nini alikaa kimya? Kama hakukaa kimya alimshauri nani na ni nani huyo aliyepuuzia ushauri wa Usalama wa Taifa?

Then linakuja suala la Chenge. Tayari tunajua SFO walikuja omba kabrasha la Chenge, jee Ikulu na Usalama wa taifa ulikaa kimya bila kufanya uchunguzi wao na kumpa Rais dondoo kuwa hali ni mbaya? je SFO walikuja Tanzania baada ya Lowassa kuanguka au uchunguzi ulianza siku nyingi? maana hakieleweki kuwa Waziri anayechunguzwa kama Serikali ilijua anachunguzwa mapema kwa tuhuma za ushiriki katika rushwa ya Radar alipewa nafasi ya kuendelea kuwa waziri wa wizara nyeti kama miundo mbinu ambako ameendeleza Libeneke na kuharibu ATCL!

Nadharia unayoleta hapa ya kusema yeye RO ana kinga kisheria kwa kuwa si jukumu lake kulinda maslahi ya Taifa au Usalama wa Taifa, naikataa maana katika Katiba ya Tanzania kipengele 27 kuhusiana na sheria ya ulinzi wa mali ya taifa kwa mujibu wa Sheriaya 1984, 15/6 na kuzingatia kuwa kila kiongozi na afisa wa Serikali anayeapishwa huapa kuitii na kuilinda katiba ya nchi, RO kama Afisa usalama wa Tanzania na Raia anawajibika kulinda maslahi ya kiuchumi ya Taifa kwa mujibu wa Katiba.


Ama ukifuatilia sheria ya Uhujumu uchumi ya mwaka 1984 kifungu cha 21.. inazungumzia ni nani ana jukumu la kuendesha upelelezi.

 
Mutu na Mchungaji, nilitaka niwashukuru kwa response zenu lakini Mkuu FMES atasema ni mimi ndio yule yule Mutu na Rev. Kishoka najishukuru mwenyewe. Kuna siku niliambiwa mimi ni 'Shetani karudi kugombana Nyani ngabu.' Sijui Shetani ndio nani jamani, mavete wa JF mnisaidie!

Anyway, ahsanteni sana ndugu zangu. Nilidhani mjadala ndio umeisha tena na wanaotaka Rashid Othman ajiuzulu wamechukua ushindi na vile na hivi.

Lakini, kama Icadon alivyo onekana kukubali -huyu jamaa nitakuwa namuheshimu sana - kazi za idara ya usalama hazijulikani. Na hata kama ni kweli ni kazi yao kuzuia hujuma za uchumi, bado kuna walio na majukumu ya karibu zaidi na hiyo kazi -TUKUKURU na Tume ya Maadili - ambao ndio haswa ilibidi waanze kuwajibishwa.

Hivyo, bado nadhani RO hapa hana hatia.
 
lakini Mkuu FMES atasema ni mimi ndio yule yule Mutu na Rev. Kishoka najishukuru mwenyewe.

1. Mimi sikukutaja jina kuwa ni wewe unayeandika na kujijibu na kujipa thanx, ahsante kwa kuniambia kuwa kumbe ni wewe!

2. Rev Kishoka, tumetoka mbali sana na ninamfahamu kwa karibu sana mkuu, yeye sio wewe, NO!

3. Ahsante kwa kunifahamisha kuwa wewe ndiye Mutu, unajua kwenye criminology, wanasema the more you talk ni the more unajsiema wewe ni nani, hasa unapojaribu kukanusha tuhuma ambayo in the first place haikulengwa kwako!

Sasa back to the ishu maana kama nilivyosema huko nyuma mimi sio the subject hapa kama unavyotaka wachangiaji wengine waamini, the ishu ni kujiuzulu kwa mkurugenzi wa usalama, now kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake kama anavyotakiwa kwa mujibu wa sheria,

JF hatujawahi kuwa on the wrong side of the glass, kuna wakati tulisema Mama Meghji, atoke tena mkulu wangu MMJ, alimtetea kama wewe mkuu unavyotetea huu ubovu, matokeo nafikiri unajua huyo mama yupo wapi, hapa hakuna personla wala beef na kiongozi yoyote, isipokuwa ni taifa tu, miaka miwili sasa imekuwa ni mafisadi tuu enough!
 

Lets say kuwa argument yako ni ya kweli, sasa hebu explain inakuwaje tena mafisadi hao hao wanaotutuma kumsakama RO ili waibe vizuri, wanapotukamata na kutaka kuifunga hii forum?

Halafu kwa nini Lowassa, alihangaika sana kujibishana na Mwanakijiji, iwapo ni mtu aneyetumwa na mafisadi kumtaka RO ajiuzulu? Sasa mwenye macho nafikiri haihitaji kuambiwa aone mwenye nia ya kuvuruga mjadala huu kwa niaba ya mafisadi, exactly ni nani? au?
 
Wana JF baada ya kupitia nyuzi hii kwa undani naona kitu kilekile kinajirudia, siwezi kuamini hata kidogo kuwa TISS hawakujua wizi wa fedha za EPA, kwa sababu wengine hao tunaowaita waheshimiwa nao ni members wa TISS, inawezekana kuwa hata Chenge pia ni member wa TISS. Kuna possibility kubwa kuwa huenda nao wamo kwenye EPA (prove me wrong), kwa hiyo tukisema kuwa TISS wameshindwa kazi, wakati kwa upande fulani wao wenyewe walikuwa part ya EPA, this does not stick in my mind. Pamoja na udhaifu wote walionao, siwezi kuamini kuwa Issue ya Radar, EPA, Richmond, ITCL na nyinginezo ziliwapita pembeni, naamini kuwa wao pia walikuwa na mkono kwenye issue.
Unaweza kujiuliza ni kwanini TISS ilijaribu sana kufanya hoja ya EPA isiingie bungeni? On whose interest? For sure not in the interest of our National security, and not in the interest of our nations prosperity.
Sasa hivi ufisadi mbele kwa mbele na kulindana mbele kwa mbele, kwenye baraua ya Zakia alieleza kuwa walitumia jina la TISS kutuibia pesa, ma-agent wa TISS pale BOT for sure walisaidia kufanikisha hilo.
The point i want to make is we need to redefine the wholse meaning of Usalama wa taifa, isiwe confined kwenye usalama wa CCM na viongozi wa serikali, iwe mpaka kwenye usalama wa nchi na uchumi wa nchi. Sasa hivi manners, morals and ethics za TISS ziko at lowest level, labda kwa baadhi ya wafanyakazi wake wa ngazi ya nchini, lakini juu kunasikitisha sana!
 
Wana JF baada ya kupitia nyuzi hii kwa undani naona kitu kilekile kinajirudia, siwezi kuamini hata kidogo kuwa TISS hawakujua wizi wa fedha za EPA


Mkuu Heshima mbele,

Huko kwenye EPA bado tuko njiani tutafika huko, hatuna haraka ishu moja baada ya nyingine, tulianza na Richimonduli, Lowassa, Msabaha, Karamagi, Meghji, Balali, pole pole mkuu tunawajia mafisadi kwa karibu, sasa Chenge, this is an-easy one litaisha very soon, and then tuta-move on huko kwingine, mkulu mmoja aliniambia majuzi kuwa by the time tumefika term ya pili, sijui kama watabaki wote!
 
FMES
Inatia moyo kama kweli wanashughulikia issue hizi, lakini kushughulikia kusiishie kuwafanya watu wajiuzulu tu na kuendelea kulindwa, wanatakiwa kufikishwa mahakamani. Sasa tunapoona kuwa haya mambo yanaishia hewani kwa watu kujiuzulu tu ndio inashangaza kidogo, tunashindwa hata kuwaamini hao walioko madarakani, kitendo cha mkuu wa kaya kumu-include Chenge kwenye Baraza la mawaziri kinaacha viulizo vingi sana. Na hata anaweza kuongea kwa jeuri kubwa kuwa "vijisenti" na bado ni waziri, na mawaziri wengine wanasema hawajaanza uchunguzi dhidi yake, yaani wamempa two years headstart, sasa hapa sijui kama kweli atashikwa! inatia shaka sana!
 

Duh not a good guess mimi ni mimi ,inawezekana ladba kuna watu wana mchezo huo anyway don't make a big deal wewe unajua si mimi thats all.Nachoweza mshauri system admin check mac address ili awaseme wenye mchezo huu kama mtu anatumia pc moja kufanya mchezo huu atajulikana.Hata ku ban mtu mkorofi anaweza mac address maana hata akibadili jina kibano kipo palepale.
 
TISS imetajwa kuhusika na wizi wa EPA wamekaa kimya; leo wametajwa kuwa ofisa wao ameshiriki katika sakata la Kubenea wamekaa kimya.

Kuhusu masuala ya ufisadi kufichuka siyo kazi ya Usalama wa Taifa wamefanya hivyo. Sitaki kuamini kuwa ni Usalama wa Taifa walioibua suala la Richmond, sitaki kuamini ni wao wamefunua mambo ya Kagoda; siyo wao waliofunua masuala ya Rada!!!

Siyo Usalama wa Taifa. Wao wanafuata tu, hawaanzi. Na hilo ndilo kosa la Othman na timu yake nzima. Nasema hivi kwa ujasiri kwa sababu baadhi ya watu waliohusika kufunua suala la Rada, Richmond ninafahamu juhudi zao zilianzia wapi, and I can tell you confidently, it was not Usalama wa Taifa.

Hivi unafikiri kuwa tumelipa zaidi ya Bilioni 21 kwa dalali wa Rada usalama wa Taifa walikuwa wanajua? Hivi unafikiri Usalama wa Taifa wanajua fedha za mawaziri zilizofichwa huko Jersey na Cayman Islands? .. hapana hawajui wao wanataarifiwa tu wakati wajuao wapo.
 
BI SENTI 50 JEE? au huyu anatumia ajenda ili watu wafungiwe? sina cha kusema wewe ndio kila kitu.
Mwambie anitaje senti 50.



What has CHADEMA done you? U seem to be very allergic with them. Au kibarua kiliota nyasi wakati fulani sababu ya hoja zao? Punguza matusi basi na hasira za zamani jamani. Jenga hoja, usihamanike

Asha
 

Ukiinyoshea CHADEMA kidole kimoja ujue vinne umevinyoosha CCM aka Chama Cha Mafisadi, kijiwe cha wasanii wakina Chenge, Lowassa, Karamagi, Mramba, Mkapa nk

Asha
 
Tanzania Tanzania Nchi yangu Niipendayo sana inanipa wakati mgumu sana katika maamuzi yangu binafsi ninapoifikiria Tanzania.

Tanzania Tanzania Nihurumie Mpenzi Tanzania!!!


Mnyonge Mnyongeni Ilaaaaaaa sasa akiitambua haki yake Hakika utampaaaaaaaaa TU
 

Mwanakijiji,

Nimekuwa nikifikiria kuwa michango yako ni ya uzalendo na inajaziishwa na uzalendo. Tafadhali niwezeshe niendelee na fikra hizo hizo, tafadhali andika yale unayoyajuwa kwani kuamini kwako na kutokuamini kwako si muhimu bali cha muhimu ni wewe kutueleza unayoyajuwa, uliyona hakika nayo hasa tukichukulia pia kuwa wewe ni mwanahabari. By the way, kuhusu radar fuatilia WB iliishinikiza vipi Serikali mwaka 2002 kuwa haikuridhika na ununuzi huo na tafuta na uelewe BM alijibu vipi. Hao wajuao ilikuwaje wakae kimya hadi WB ilonge na daada ya kulonga ipigwe kiini macho.
 
Nimewahi kuuliza mara nyingi sana watu wengi sana hapa TZ pia niliwahi kumuuliza rafiki yangu mmoja ambaye ni usalama wa taifa. nilimuuliza swali hili hivi usalama wa taifa ni nini? nikamuuliza tena kazi yao ni nini? nikaendelea kuuliza watu wanatakiwa kuwa usalama wa taifa wanatakiwa kuwa na taaluma zipi? nikamalizia kwa kumuuliza mimi nikitaka kuwa usalama wa taifa nifanye application wapi? kati ya mwaswali yangu yote hakunipa jibu hata moja..
Jamaa alikuwa akitoka na kagari kake kazuri anakaa bar hadi saa nane za usiku.. asubuhi anaenda kwenye kaofisi fulani sikujua hata anafanya nini.. ila ana nyumba 2 gari kama 3... nikiangalia kwa makini anafanya nini sioni kwa kweli....

Sawa nakubali nchi lazima ilwe na watu wa usalama wa nchi na moja ya kazi zao kubwa ni kuangalia usama wa raia na mali zao..pia kuangalia kama kunamafusadi wanaotaka kuifilisi nchi yetu.
Kinachonishangaza mimi usalama wa taifa letu wanawalinda mafisadi.. ndio wanakula na mafisadi.. ndio wananshauri raisi awachague mafisadi..

Nami naongana na Invisble RO ajiuzulu Yes Aachie ngazi.. la sivyo atambie amefanya nini
 
Sawa nakubali nchi lazima ilwe na watu wa usalama wa nchi na moja ya kazi zao kubwa ni kuangalia usama wa raia na mali zao..pia kuangalia kama kunamafusadi wanaotaka kuifilisi nchi yetu.

Msesewe;
Unajua ni kazi yao au ungependa iwe kazi yao?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…