Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Icadon,
Hawa jamaa wanahitaji reform za hali ya juu. Wao wanafikiri kujua Kung-Fu na Judo ndio ujanja.
Si ajabu wengi wao hata kutumia Computer na internet hawajui!
Icadon, sheria ya TISS inasema wapi kuhusu kuwa na wafanyakazi wa TISS kwenye balozi zetu?
Makala tayari ipo kwenye "Editorial" ya KLHNews..
Mhandisi,
Hawako hapa kujifunza na kujirekebisha! Wako hapa kutafuta nani kasema nini kuhusu Serikali, anakaa wapi na kamsema yupi wa Serikali!
Wamekaa mkao wa wambea kazi kuchukua habari na kusema ohh "vijana wana matusi" nope!
Kwanza ujinga wao na urahisi wao kutabirikia mtaounoa jinsi CCM inavyofanya kazi. Walipokwenda Butiama, unasikia wanasema Tutachapa maadniko ya Nyerere! Hii ilikuwa baada ya watu kukata ishu kuhusu Fikra na legacy ya Nyerere.
Kwenye mkutano wa Rais wa mwisho kwa Taifa, katujubu kihakika JF kuhusu Comorro ili aonekane analofanya ni la maana.
Mbona hawajajibu haya ya Ufisadi? Mbona hawajesma lolote kuhusu maafa yanayotuzingira?
Labda uniambie wale vijana wadogo wakiwasilisha nondo kwa wakubwa na zikifika kwa RO, zinakwama! Then it is justifiable for us to say RO has to go!
Sikutaka kuanzisha thread lakini tangu wiki iliyopita nimekuwa nikiomba hizi threads ziunganishwe ili tuwe na mtiririko mzuri wa habari
Nimeona bora niwarahishie kazi
RASHID OTHMAN ndiye Boss wa Usalama
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=169&highlight=TISS
Usalama wa Taifa wapo likizo?... Je, Waziri wa Intellijensia ni nani?
The Spies who loved me...AG, TISS, TAKUKURU, POLISI
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=10207&highlight=TISS
Taifa lilipotekwa Nyara, Usalama wa Taifa walikuwa wapi?
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=11575&highlight=TISS
Rashid Othman: Umeshindwa Kuhakiki Usalama wa Taifa, Jiuzulu !
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12174&highlight=TISS
GEORGE KAHAMA na ANDY YOUNG wamegombana?
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8264&highlight=TISS
Mashushushu kazini kuua waandishi?
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12160&highlight=TISS
Usalama wa Taifa (TISS) kumejaa wezi na mafisadi
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8997&highlight=TISS
Usalama wa Taifa
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9246&highlight=TISS
VETTING na BACKGROUND CHECKS serikalini
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=5519&highlight=vetting
Mkjj, kudos kwenye makala ndio nimemaliza kuisoma, by the way if my memory serve me correct RO alisema ataanzisha utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari..tunaendelea kusubiri.
Kwa hiyo RO ajiuzulu kwa vile hajakutana na waandishi wa habari?
Kama umefuatlia habari vizuri hao SFO walipata ushirikiano wa serikali kumuhoji Chenge kama RO anahusika asingetoa ushirikiano nao na lazima vijana wake walikuwa bega kwa bega na SFO, hadi sasa sijajua kwanini unalalamika kuhusu Rada na RO.
Wakuu kama yaliyosemwa yametosha, nitaanza rasmi kukusanya points muhimu kuanzia Jumapili, kutoka hii topic ili kuzifikisha kwa baadhi ya wabunge wetu wa taifa, ili zifanyiwe kazi maana binafsi ninaaamini kwamba huu umekuwa mjadala mzito na wenye hoja nyingi za muhimu kutoka pande zote zinazotetea na zinazoshambulia, yote ilikuwa nia ya kuliletea taifa letu mabadiliko yanayolenga uwajibikaji katika sekta zote muhimu za taifa letu,
Kama vile tulivyowahi kutoa mapendekezo kwa ajili ya foreign(Membe), BOT(Balali), Tanesco(Idrisa), Polisi(Mahita), Chenge, Mkapa, Richimonduli, Lowassa, Msabaha, Karamagi, na wengineo wengi, ninaamini nia ilikuwa ni ile ile nayo ni taifa, sidhani kwamba kuna hata member mmoja hapa aliyetoa mchango wake kwa nia ya ubinasfi.
Binafsi ninawashukuru wote waliochangia hii mada nzito iliyoanzishwa na Mkulu MMJ, ambayo pia imetuhakikishia kuwa uhuru wetu wananchi wa kuuliza maswali muhimu kwa taifa letu kuwa hauna mipaka ndani ya sheria za jamhuri yetu, na Jumapili nitaanza rasmi kuchomoa points.
Ahsanteni!
Bro, unaweza kutoa ka muhtasari wa hizo hoja muhimu unazopeleka huko mbele?
ndio maana aondoke afuatane nao huko wanakotumbua fedha za Taifa hili. How can an intelligence agency be unintelligent?
Unajua sikua nataka kweli muhtasari wa kilicho jadiliwa hapa. Wote tumeisoma mada, tumechangia, na bado tunaweza kuisoma. Hasa, nilicho maanisha bila kukitamka ni hiki:
Kulikuwa kuna mawazo yanayopingana sana hapa. Na wewe ulikuwa una hisia kali katika upande fulani wa huu mjadala. Sasa unaposema unapeleka mawazo yetu kwa wakuu najiuliza unaenda kusema nini kuhusu huu mjadala? Utavutia ngozi kwako? Au utasema tumefikiri hivi, na kwa upande mwingine tumefikiria vile. Na huyo mkubwa atakuuliza kwa hiyo mnashauri nini kama kuna pande mbili, au saba?