Wakuu kama yaliyosemwa yametosha, nitaanza rasmi kukusanya points muhimu kuanzia Jumapili, kutoka hii topic ili kuzifikisha kwa baadhi ya wabunge wetu wa taifa, ili zifanyiwe kazi maana binafsi ninaaamini kwamba huu umekuwa mjadala mzito na wenye hoja nyingi za muhimu kutoka pande zote zinazotetea na zinazoshambulia, yote ilikuwa nia ya kuliletea taifa letu mabadiliko yanayolenga uwajibikaji katika sekta zote muhimu za taifa letu,
Kama vile tulivyowahi kutoa mapendekezo kwa ajili ya foreign(Membe), BOT(Balali), Tanesco(Idrisa), Polisi(Mahita), Chenge, Mkapa, Richimonduli, Lowassa, Msabaha, Karamagi, na wengineo wengi, ninaamini nia ilikuwa ni ile ile nayo ni taifa, sidhani kwamba kuna hata member mmoja hapa aliyetoa mchango wake kwa nia ya ubinasfi.
Binafsi ninawashukuru wote waliochangia hii mada nzito iliyoanzishwa na Mkulu MMJ, ambayo pia imetuhakikishia kuwa uhuru wetu wananchi wa kuuliza maswali muhimu kwa taifa letu kuwa hauna mipaka ndani ya sheria za jamhuri yetu, na Jumapili nitaanza rasmi kuchomoa points.
Ahsanteni!