Rasimu ya katiba: Ikulu itakuwa ya Tanganyika au muungano?

Makao makuu ya Tanganyika yalikuwa Dar es Salaam na yatarudi kuwa Dar es Salaam. Dodoma ni makao makuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaia.
 
Nadhani CHAMWINO ndo kwa rais wa Tanzania, magogoni ni kwetu watanganyika!!!!!
 
Dah!huu ndo utakua mwanzo wa kuanza kuachapana hata kabla marehemu hajafa tumeshaanza kugombania nyumba,maamuzi ya wapi ikulu ya muungano itakuwepo najua yatafanyika kwa umakini mkubwa sana coz nionavyo huyo rais wa muungano hatadumu muda mrefu na muungano huenda ukafa ss wakichukua magogoni sijui itakuaje.
Hii rasimu ishaanza kuteletea balaa
 
Mkuu haya ni baadhi ya mapungufu yaliyopo ndani ya Rasimu,kwa haraka hakuna mahali kumetajwa wapi patakuwa Makao makuu au Ofisi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Warioba na wajumbe wake bado wanakazi ya kufanya.
 
Na jengo la bunge itakuwaje? Lile la Dodoma ni la Muungano, hakuna mjadala hapo, vipi lile jengo la zamani nalo ni la muungano? vinginevyo sasa bunge la Jamhuri ya Tanganyika litarejea Karimjee.
 
Na jengo la bunge itakuwaje? Lile la Dodoma ni la Muungano, hakuna mjadala hapo, vipi lile jengo la zamani nalo ni la muungano? vinginevyo sasa bunge la Jamhuri ya Tanganyika litarejea Karimjee.

JMT bado haina ASSET yoyote. Ardhi yote na vyote vilivyomo TANGANYIKA ni vya Tanganyika kama ilivyo kwa Zanzibar.
Tanganyika itakapofufuka, itabidi turudishiwe kila kitu kinachodaiwe eti cha Muungano. Vingi vilikuwa vya Tanganyika. Zanzibar haijawahi kuwekeza katika ujenzi au ufanikishaji wa chochote. Hata Benki kuu, Viwanja vya ndege, Majengo, Kampuni ya simu TTCL, ya Reli TRL, na vinginevyo. Kama tuna ushahidi wa uchangiaji wa Zanzibar, uwekwe wazi ili Tuweze kupanga umiliki wa share na mengineyo.
Hapa naona dalili ya ugomvi mkubwan mbeleni... Unaoweza kutuingiza katika vita..
Naomba kurekebishwa..
 
Kazi ipo mwaka huu, na kile chuo cha UDOM kitakuwa ni cha muungano au itakuwaje?
Na jengo la bunge itakuwaje? Lile la Dodoma ni la Muungano, hakuna mjadala hapo, vipi lile jengo la zamani nalo ni la muungano? vinginevyo sasa bunge la Jamhuri ya Tanganyika litarejea Karimjee.
 
Wanajf mie nashangaa kuona wazazi wa muungano ambao ni tanganyika na zanzibar walizaa mtoto tanzania na baada ya kizazi hicho mzazi mmoja tanganyika jina lake likafa na jina la mzazi wa pili likaendelea kuwepo lakini cha ajabu zaidi mtoto aliyezaliwa akawa na nguvu kuzidi wazazi wake, na mbaya zaidi hata wazazi wenyewe wanamwogopa huyu mtoto ni balaa hata eti ''hasiguswe'',. Je bandugu hii ndo malezi gani kwa huyu mtoto na je majirani watawachukuliaje hawa wazazi kwa malezi haya?
 
Mkuu nilifikiri Dodoma ni makao makuu ya Jamhurti ya Muungano (na sasa shirikisho), kwa hiyo seriksli ya shirikisho itakuwa Dodoma. Tanganyika itabaki Dar es Salaam isivyo amliwe vinginevyo.
 
Kuongeza serikali ni kuongeza matatizo, kigharama, kuleta ma cliques na ma personality conflict kutokana na ma ego etc
 
Sisi hatunahaja na magogoni tunataka mamlaka kamili ya znz basi na si hadithi za mambo saba ya muungano...chuweni majengo yote wazanzibar we want our sovereignty back..... On this an option is on the table
 
Hivyo vilivyojengwa ndani ya muungano ni vya tz ni kodi za pande zote ni vyetu sote.
Lkn znz kwanz twataka nchi kamili yatakuja kujadiliwa yanazungumzika lkn znz sovereign has
no compromise
 
Umesahau
Nembo ya Tanganyika ndo hii ya muungano, jee itakuwaje ?
Wimbo wa taifa la tanganyika ndo huu wa muungano jee itakuwaje ?
Bendera ya muungano ndo hiyo ya tanganyika jee itakuwaje ?
 
mawazo yangu yako hv,ikulu ya magogon ibaki kwa tanganyika na ikulu ya muungano ijengwe mpya.
 
safari hii makao makuu ya serikali yawe zanzibar na wizara zote za muungano zihamie zanzibar
 
kama ningekuwa na ushawishi wa kisiasa ningeshauri ikulu ya serikali ya muungano ikajengwa zan zibari nasi tubaki na tuliyokabidhiwa na mkoloni
 
Kama vipi ya muungano iwe katikati,yaan baharini.
Sasa hapo inabidi tununue meli kuuuuuubwa!rais wa muungano awe anakaa katikati ya tanganyika na znz kama baharia vile.

Mawazo yangu tu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…