Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,346
Ibara zote 240 za rasimu ya katiba ziko kimya kabisa juu ya suala la ndoa, mahusiano ya kimapenzi na familia.
Je, ukimya huo hautakuwa upenyo kwa watu wanaotetea masuala ya ndoa/mahusiano ya kimapenzi kwa watu wa jinsia moja?
Katika ibara ya 24 (2) na (3), rasimu inatoa haki sawa kwa wote, na kukataza utungwaji wa sheria yeyote itakayowabagua watu.
Nanukuu:
"(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu, mamlaka ya nchi au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika kutekeleza kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.
(3) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake."
Je, vipengele hivi havitatumika na watetea ndoa za jinsia moja, dhidi a sheria yeyote ya ndoa itakayoacha kuwatambua?
Ieleweke kuwa suala la ndoa za jinsia moja limekuwa kama 'utamaduni' katika dini fulani. Pamoja na rasimu ya katiba kueeza kuwa haki za kidini zitalinda pamoja na mambo mengine, maadili ya taifa
ie.. Ibara ya 31 (4)... "Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za nchi".
Lakini neno maadili halijapewa ufafanuzi mahali popote katika rasimu hii, hivyo itakuwa vigumu kukitumia kipengele hiki kukataa ushoga nk...
Ikumbukwe kwamba rasimu hii imetoa ruksa kwa dini na uhuru wa mtu kuabudu na kufuata mambo ya dini husika
Ibara 31 (1)... Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.
Wakuu nyie mnaonaje?... Naomba kueleweshwa kama hii rasimu ina kipengele ambacho kinadhibiti ndoa na mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja...