Rasimu ya katiba mpya imeruhusu ndoa za jinsia moja?

Kwani unadhani kila kitu kitaingizwa kwenye katiba? Maana ya ndoa ni nini kwa utaratibu/sheria/miongozo ya sasa?Muunganiko wa watu wawilie...wenye umri....jinsi tofauti. Kwa maana nyingine kuna msisitizo wa umri na jinsi (sio jinsia)

Mkuu kama hujali hebu pitia post # 19 hapo juu alafu utumbie ni kwa nini nchi nyingine hilo suala limeongelewa?
 
Mkuu Magobe, asante kwa mchango.. Lakini kwa uelewa wangu kitu kinachoitwa "utamaduni na mila za kitanzania" ni dhana ya kufikirika zaidi. Haijaandikwa mahali popote (kama papo naomba unipe reference), na hakuna mamlaka yeyote ya kitaifa inayotunza kitu hicho.
Zipo tamaduni na mila ya mamia ya koo na makabila Tanzania, ambazo hutofautiana sana. Mathalani, ukekeketaji wa wanawake ni sehemu ya mila kwa baadhi ya makabila Tanzania.
Kule Mara, wakurya wana mila ambayo inaruhusu mwanamke kuoa mwanamke mwenzake, wanaita Mmba Ntobu (Najua nimelikosea hilo jina, naomba Mwita Maranya aje anisahihishe). Je, kesho wewe ukiwa katika mamlaka fulani, ukaletewa ushahidi kuwa mdada ameolewa na Mmama fulani kama Mmba Ntobu, hivyo status yake ni married, utaamuaje?
Kwenye kabila langu (may be ukoo wetu), kuna mila inaruhusu kuoza marehemu, nk...

Kule nchini Malawi, miezi kadhaa iliyopita walikuwa na debate ya ndoa za jinsia moja, na kwa kiasi fulani ikapelekea raisi Joyce Banda kulaumiwa. Lakini mi nadhani tatizo lilianzia kwenye katiba yao ambayo kwenye Ibara ya 22, inaongelea familia lakini haikubainisha ulazima kuwa ndoa ni mwanaume na mwanamke. Nainukuu:

(3) All men and women have the right to marry and found a family

Katiba hiyo ya Malawi ilikumbuka tu kuongelea kuhusu umri:

(8) The State shall actually discourage marriage between persons where either of them is under the age of fifteen years

Tulishuhudia nchini Uganda watu wakiandamana kudai haki ya kutambuliwa kwa ndoa za jinsia moja. Kigezo walichokuwa wanatumia kuwa katiba haijakataza ndoa hizo, wakirerefer Ibara ya 31 ya katiba yao ambayo inasema, nanukuu:

(1) Men and women of the age of eighteen years and above have the right to marry and to found a family and are entitled to equal rights in marriage, during marriage and at its dissolution

Hata hivyo serikali iliweza kuwadhibiti kwa kutumia kifungu kidogo cha 3 ambacho kinasema, nanukuu:
(3) Marriage shall be entered into with the free consent of the man and woman intending to marry

Hata hivyo, bado huko uganda suala hilo limekuwa na utata hadi sasa

Nchini Kenya, katiba kielelezo (rasimu ya katiba) ilipigwa chini katika kura ya maoni, nayo ilikuwa plain kuhusu suala la familia na ndoa. Makundi mengi ya kidini yaliipinga rasimu ile kwa kigezo hicho. Walipokuja kutengeneza rasimu nyingine ambayo ndiyo ilipitishwa na sasa inatumika kama katiba ya nchi hiyo, waliliweka suala la ndoa na familia very clear.
Katika Ibara ya 45 katiba ya Kenya inasema, nanukuu:
(1) The family is the natural and fundamental unit of society and the necessary basis of social order, and shall enjoy the recognition and protection of the state
(2) Every adult has the right to marry a person of the opposite sex, based on the free consent of the parties.

Kwa mantiki hiyo mkuu, suala la ndoa na familia kwenye katiba, sio la kuacha tu hewani kwani baadae litaleta migongano.

Labda niombe mawazo ya watu wengine humu kina Mzee Mwanakijiji EMT, gfsonwin, Kongosho,
Roullete na wanaJF wengine wote...
Mkuu Painlife in Tanzania, hebo toa pia mawazo yako hapa...

"Utamaduni na mila za Kitanzania" inajumuisha pia mafundisho yao ya dini (maana dini ni sehemu ya utamaduni). Ukisema utamaduni wa Wakurya unaruhusu ukeketaji, unakuja kuona pia kwamba kwa mafundisho ya wale wanaoabudu katika imani fulani, inakataza kufanya kitu kama hicho. Utakuta pia haki za binadamu ambazo tumeridhia kuzifuata zinakataza. Ukisoma post yangu hapo juu wakati nakujibu nilianisha vifungu ambavyo vinaonesha kama kitu kama hicho kikitokea kitakuwa kinapingana na Katiba Mpya katika maeneo kadhaa. Niliyataja kama:

1) tunu za taifa
2) mila na desturi za Kitanzania
3) malengo makuu ya Katiba
4) haki na wajibu muhimu
5) kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.

Ina maana, ukisema ushoga na usagaji - ni kinyume na tunu za taifa ambazo zimeainishwa kama utu (human dignity), uadilifu (morality, morals) nk, ni kinyume na
desturi na mila za Kitanzania (yaani, desturi na mila hizi ni zile ambazo hazipingani na Katiba, sheria zilizopo, haki za binadamu na imani za dini), ina maana ni kinyume na malengo makuu ya Katiba, ina maana ni kinyume na haki na wajibu muhimu na zaidi sana ni kinyume na kukuza... heshima ya taifa. Yote haya yameanishwa katika Rasimu ya Katiba. Zamani kule Ukerewe, mapacha wakizaliwa ilikuwa ni bahati mbaya, hivyo walikuwa wanatupwa wanawekwa kwenye vyungu vikubwa na kuachwa wafe au waliwe na fisi porini. Sehemu yenyewe inaitwa "Nyamayungu". Hii huwezi kuiita mila maana inapingana na mambo mengi sana katika jamii. Pia hata leo mtu akifiwa na mke au mume "ili kumaliza kifo" ni lazima alale na mume/mke mwingine na hiyo ikishafanyika mfiwa ananyolewa nywele ili nywele mpya zianze kuota kuonesha maisha mapya (ya kale yamepita). Hii ni kwa mantiki kwamba tendo la ndoa ndilo linaolowezesha uhai uwepo na hivyo (mbegu za kiume kumwingia mwanamke) zinaonesha ku'resist' kifo/kupambana na kifo na hivyo kufanya propagation of the human race. Sasa hii mila si mila nzuri hasa ukizingatia kuwa kulala na mtu mwingine unaweza kupata ugonjwa wa zinaa/HIV/Aids na unazini (kinyume na maadili ya dini) nk. Kwa maneno mengine, atakaye kuja na hoja ya kuhalalisha ushoga lazima awe mtu wa pekee sana kuweza kuwafanya Watanzania wakubaliane naye.
 
Asante...
 
Ibara hiyo inatakiwa tuipinge ni hatari kwa vizazi vyetu.
 
Tuko ,
'Maadili' (kama ilivyo kwa tamaduni kwa ujumla) yanabadilika. Miaka 30 iliyopita ilikuwa ni "kukosa maadili" kwa mwanamke kuvaa suruali! Lakini leo hii hali ni tofauti sana. Ukitizama hata suala hili la ushoga, leo hii linafanywa kwa uwazi zaidi kuliko zamani (unaweza kusema kuwa leo hii "linavumilika" zaidi kuliko zamani!). Kwa hiyo, kwa katiba kutoku define neno maadili nadhani ni sawa ili kuzipa nafasi social dynamics za wakati husika kutoa definition yake kwa wakati husika ("kila zama na kitabu chake"!).

Hii habari ya haki za mashoga ni tata sana. Hasa kwa kuwa mara nyingi tunaojadili suala hilo na kulitolea maamuzi tupo "straight" na hivyo kwa kiasi fulani pengine tunashindwa kuwa objective au kuona upande wa pili.

Najaribu kujiuliza tu, hivi ni kweli (kisayansi) mtu anaweza kuzaliwa "shoga" (with homosexual orientation)? Kama ni kweli wapo waliozaliwa hivyo je "haki zao" zinaweza kulindwa vipi kikatiba? Wanayohaki ya kuishi sexually kwa kufuata namna "orientation" yao inavyotaka kama vile sisi tulio "straight" tunavoishi? Pengine hii ingetosha kuwa mada tofauti kabisa lakini katika kuitizama rasimu katiba yetu ni muhimu pia suala hili likatizamwa/likajadiliwa.
 
rasimu ya katiba mpya haijaruhusu ndoa za jinsia moja kwa sababu hii ni rasimu ya kwanza kwa hiyo haijagusa vitu vyote vilivyopendekezwa. Kwa hiyo tusubiri rasimu ya pili tuone kama itazungumzia suala hilo.

rasimu haiwezi kuingiza kila kitu imeaangalia vile vya msingi ambavyo vinaweza kuleta mikingano endelevu...tuisome rasimu tuisome
 
Ibara hiyo inatakiwa tuipinge ni hatari kwa vizazi vyetu.
Hata kama hiyo ibara itabaki, mi nadhani kuwepo kipengele (kama kilivyo katika katiba ya nchi nyingine eg Kenya) kinachosema marriage ni baina ya watu wa opposite sex. Rasimu ya kwanza kule Kenya ilikaa kimya, lakini Misikiti na Makanisa yakashupalia hadi kipengele kile kikaongezwa...
 
Tuko ,
'Maadili' (kama ilivyo kwa tamaduni kwa ujumla) yanabadilika. Miaka 30 iliyopita ilikuwa ni "kukosa maadili" kwa mwanamke kuvaa suruali! Lakini leo hii hali ni tofauti sana. Ukitizama hata suala hili la ushoga, leo hii linafanywa kwa uwazi zaidi kuliko zamani (unaweza kusema kuwa leo hii "linavumilika" zaidi kuliko zamani!). Kwa hiyo, kwa katiba kutoku define neno maadili nadhani ni sawa ili kuzipa nafasi social dynamics za wakati husika kutoa definition yake kwa wakati husika ("kila zama na kitabu chake"!).

Hii habari ya haki za mashoga ni tata sana. Hasa kwa kuwa mara nyingi tunaojadili suala hilo na kulitolea maamuzi tupo "straight" na hivyo kwa kiasi fulani pengine tunashindwa kuwa objective au kuona upande wa pili.

Najaribu kujiuliza tu, hivi ni kweli (kisayansi) mtu anaweza kuzaliwa "shoga" (with homosexual orientation)? Kama ni kweli wapo waliozaliwa hivyo je "haki zao" zinaweza kulindwa vipi kikatiba? Wanayohaki ya kuishi sexually kwa kufuata namna "orientation" yao inavyotaka kama vile sisi tulio "straight" tunavoishi? Pengine hii ingetosha kuwa mada tofauti kabisa lakini katika kuitizama rasimu katiba yetu ni muhimu pia suala hili likatizamwa/likajadiliwa.
Nakubaliana na wewe mkuu, lakini kwa hili la ndoa za jinsia moja, nadhani tusiiachie nature. Kesho kutwa utakuwa hakimu mahali, mara unaambiwa unatakiwa uidhinishe kiapo cha ndoa ya wanaume wawili... Mi sitaweza...
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Nashukuru kwa mchango chanya ni kweli kabisa baada ya katiba kupita kuna sheiria nyingi pia zitafanyiwa maerekebisho. Naamini kuwa sheria ya ndoa hata kama itakuwa na marekebisho lakini haiwezi kuruhusu ndoa ya jinsia moja.. Unajua sheria mara nyingi inaweza kuwa na maana zaidi ya moja ukiangalia kwa kina utaona kuwa hata hapo unaweza ona ndoa moja inaweza kutetewa kwa ibara hiyo ya 24 (3) lakini itakuwa inawaumiza wa upande wa pili yaani mimi na wewe ambao tunaona kuwa hawa wanatudhalilisha sisi wanaume.. Hata ile ibara ya 16 ya ktiba tliyo nayo ukiisoma utaona kabisa hata mtu wa jinsi hii inaweza kumtetea...
 
Labda niombe mawazo ya watu wengine humu kina Mzee Mwanakijiji EMT, gfsonwin, Kongosho, Roullete na wanaJF wengine wote...
Mkuu Painlife in Tanzania, hebo toa pia mawazo yako hapa...

Sijui mjadala wenu umeanzia wapi lakini nakubaliana na Magobe T kuwa huwezi kuweka "each and everything" kwenye katiba.

Hata ukiangalia nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani na Afrika ya Kusini ambazo zina probably the most advanced constitutions siyo kila kitu kimewekwa kwenye hizo katiba zao.

Indeed, watu wengi sasa wanataka kuishi in a free, unregulated world. Sometimes, too much laws doesn't do us any favour. Kama kila mtu akiamini na kuheshimu haki yako ya kuwa na familia na wewe ukiheshimu pia haki za hao watu, then hakuna haja ya kuwa na sheria ya kulinda hiyo haki kwa sababu haitakaa ivunjwe anyway.

Badala ya ku-judge matendo yetu based whether they are lawful or unlawful tu-base zaidi kwenye whether our actions or omissions are right or wrong.

Juzi nilikuwa nasoma article moja ambapo tajiri mmoja katika ku-avoid kulipa tax kubwa alichukuwa karibia nusu ya faida yake na kukipa chama kimoja cha siasa. Hapo hakuvunja sheria yoyote kwa sababu tax avoidance siyo kinyume na sheria.

Hata hivyo, wananchi na vyombo vya habari walikuja juu na kudai kuwa, though it was legal, it was was not a right thing to do. Badala ya kukwepa kulipa kodi, the right thing to do was to pay full tax for his profits.

Usisahau kuwa originally sheria zilianzishwa kwa ajili ya kulinda watawala na walichonacho. Sidhani kama mambo yamebadilika sana.
 
Mkuu, I get your point. Then miaka michache ijayo tutegemee watu wanavuka mpaka toka Kenya, Uganda, Burundi and all surronding countries wanakuja Tanzania "kufunga ndoa" kisha kurudi ma kwao.
(I will be the last person to tolerate that I guess)...
 
Mkuu, naona unajitahidi kuwa as strict as the Pope...lol. Any way... Tupo kwenye zama za kiliberali. Ngoja tuone viongozi wetu wa dini wanarespond vipi hapa Bishop Hiluka njoo humu...
Masanilo, njooni mumpe mwongozo muumini wenu huyu...
 
Last edited by a moderator:
Tuko,
SMU na EMT wanamichango mizuri kwa kile ninachotaka kusema.
Kwa kuongezea rasimu imejaribu kukwepa migogoro ya kikatiba inayoweza kujitokeza.

Kumbuka hii ni rasimu ya muungano. Unapoweka kipengele cha dini kunaweza kuwa na tatizo huko mbeleni.Zanzibar kama wanavyodai ni taifa la kiislam, sasa mshirika wa muungano akiweka sheria zake za ndoa kwa mziangira yake hapo huoni kuna ukinzani na katiba ya muungano.

Pili, Ukishaweka kipengele cha ndoa hapo umeingiza dini. Na kama ulivyoona rasimu imejaribu kukwepa suala la dini kuwa ndani. Kwahiyo uki define ndoa utaishia kwenye mambo mengine ambayo yana migogoro.

Tatu,dunia inabadilika. Leo unaweza ku-define ndoa, miaka mitano likatokea kundi lenye interest nyingine.
Mathalan, CUF ambao ni waliberali wakaongoza Zanzibar na kufuata misingi ya ideology ya chama chao huoni kutakuwa na mgogoro wa kikatiba.

Nne, utakapo define ndoa hapo unaongelea dini, lakini kumbuka kuna ndoa za asili ambazo nazo itabidi uzitafutie avenue kwasababu huwezi kuwa na katiba ya waislam na Wakristo ukaacha makundi mengine
ya jamii. Ukishawaalika watu wa asili, atheist, pagans n.k. huwezi kuwaweka kando waliberali.
Kutakuwa na mgogoro tu

Tano, Kila serikali mshirika atakuwa na mamlaka ya kuamua mambo kulingana na mazingira yao hivyo ni bora katiba kuu ikatoa nafasi hiyo.

Ndivyo ambavyo watu wanajiuliza kwanini ardhi haikuingizwa. Kwa mtazamo ni kuwa ukishafanya ardhi suala la katiba ya muungano hapo utakuwa umenyima nafasi washiriki wa muungano.
Sheria ya muungano itaathiri pande zote, je washirika watakubaliana na hilo?
Ni heri liwe nje kwa kila mshirika kuamamua matumizi ya ardhi yake
 
Mkuu nashukuru kwa mchango mzuri. Lakini kama ulivyoona, rasimun hii imetoa uhuru wenye mipaka katika mambo ya dini. Ibara nzima ya 31 inaongelea uhuru wa dini. Hata hivyo wanaweka mipaka katika ibara ndogo ya nne, nanukuu:
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za nchi.

Kwa hiyo unaona kuwa uhuru wa dini utasimamiwa na "utaratibu ulioanishwa kwenye sheria za nchi". Nadhani hili ni muhimu kwa sababu ikija dini leo na kusema wao wanakula watu, au wanakula maiti, au maiti wanazitupa barabarani nk, sidhani kama uhuru huo wa dini utavumuliwa. Sasa ni katika dimensions hizo hizo kwa maoni yangu, naona suala la kuingiliana kinyume na maumbile lizuiwe katika katiba.
Mkuu, katiba za nchi nyingi za JIRANI ambazo kwa kiasi kikubwa tunafanana kitamaduni zina hicho kipengele. Why not us?
 
Tuko nakuelewa kabisa, na rasimu imesema kama ulivyosema. Ukiisoma kwa umakini utaona inajaribu sana ku-limit isiingie kwa undani katika mambo ya imani. Kwavile jamii ina watu wenye imani tofauti, rasimu imejaribu kulieleza kwa uchache ili kuzuia yasijetokea hayo ya watu kula wengine.

Kuhusu kipengele cha kupiga marufuku, nadhani wanachelea kwa mifano ya nyuma.
Hakuna aliyekuwa anaamini kuwa ujamaa utaanguka na hata ukawekwa katika katiba. Leo tunajua kuwa ni kipengele kilichokufa miaka mingi kikabaki kama alama.

Unakumbuka kuhusu IMF? Maandamano n.k. leo wamepiga kambi Dar na ofisi kabisa
Unakumbuka white paper na vyama vingi, leo kila kona ni chama cha siasa.

Sasa kwahili nadhani wanoiona hatari ya huko mbeleni kujikuta katika wakati mgumu.
Hata hivyo ukanza kuwazuia hao, basi waislam na wakristo watasema na upaani upigwe marufuku halafu wakimaliza wanahamaia kwa atheist na Baada ya hapo wanapiga marufuku jando na unyago.

Tuko, unajua masuala ya imani ni complicated. Ukishaanza ku-define na kuingia ndani basi unakaribisha hali isiyo nzuri.
Naona tyaache mambo mengine kama yalivyo. Sikubaliana lakini naangalia dunia in different perspective
 
Mkuu, I get your point. Then miaka michache ijayo tutegemee watu wanavuka mpaka toka Kenya, Uganda, Burundi and all surronding countries wanakuja Tanzania "kufunga ndoa" kisha kurudi ma kwao.
(I will be the last person to tolerate that I guess)...

Would you also be the last person to tolerate kama Watanzania nao watakuwa wanavuka mipaka na kwenda Kenya, Uganda, Burundi and all surrounding countries kuoa/olewa?

Au unadhani kuwa Watanzania nao hawatavuka mipaka na kwenda kuoa/olewa nje ya nchi? Kuna ubaya wowote wakivuka mipaka?

Kwanza nini maana ya familia? Ni kufunga ndoa na kisha kurudi ulikotoka?

Kuwa na haki ya familia ni lazima ufunge ndoa?

Hata hivyo, haki ya kuwa na familia nimeitolea kama mfano tuu.

Vipi ningesema haki ya kusikilizwa au freedom of expression?

Katiba iweke misingi ya taifa, lakini siyo kubeba kila kitu.

There are fundamental constitutional principles which should be included in a constitution. But not all principles are constitutional.

Principles nyingine kama the right to be heard, not to be bias in decision-making are principles of natural justice. Whether or not you include them into the constitution, won't make a difference. Bado zitaendelea kutambuliwa kama principles of nutural justice rather than constitutional principles.

On the bottom, hakuna haja ya kuweka kwenye katiba, kwa mfano, idadi ya wizara katika serikali, limit ya safari za Rais nje ya nchi simply because tuna wizara nyingi au Rais wetu anasafiri sana.

Ni Rais na washauri wake kujihoji kama it is right or wrong kuwa na wizara nyingi au kuwa na ziara nyingi nje ya nchi.
 
Ndio. Sura ya nne, sehemu ya kwanza kifungu cha 45. Inazungumzia haki za makundi madogo katika jamii. Makundi madogo katika jamii kwa kimombo ni "minority groups". Kwa definition minority groups" ni pamoja na mashoga. Ukitaka kuamini angalia katiba za wenzetu hasa za ulaya na hata afrika kusini katiba zao zinataja "the rights of minority groups" ambao wanatasfiriwa ni pamoja na mashoga. I stand to be corrected.
 
Kwa wale wenye mwelekeo wa Kikristu, naomba niwakumbushe kwamba ni kosa kumbagua mtu hata kama ni homosexual. Kama homosexuality ni dhambi, basi tunapashwa kuichukia hiyo dhambi na siyo huyo mdhambi.

Definition ya NDOA lazima iwekwe kwenye katiba. Na NDOA ni kati ya mwanamke na mwanamme. Kwa msingi huo, there is no such thing as NDOA ya jinsia moja. This is plain verbal engineering
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Watu wengi wamesema, hata wale ambao wamezaliwa wakiwa na vinachocheo vya mwili (homones) zenye ushoga, endapo mtu anagundulika mapema ni rahisi. Pia hata wale ambao wameshaanza kufanya hilo tendo, inawezekana kubalidilia. Nakuwekea links hapa: Some Gays Can Go Straight, Study Says - ABC News
[URL Pia unaweza kusoma hapa, ambapo wengine wanadhani haiwezekani, http://wiki.answers.com/Q/Can_a_person_change_from_gay_to_straight. Well, kimsingi inabakia kusema kuwa iwepo kinasaba (gene) au kisiwepo, suala la sexual orientation linaweza kudumazwa/kuhamasishwa kupitia mazingira zaidi kuliko kinasaba chewenye (nadhani) [/URL] Najaribu kujiuliza tu, hivi ni kweli (kisayansi) mtu anaweza kuzaliwa "shoga" (with homosexual orientation)? Kama ni kweli wapo waliozaliwa hivyo je "haki zao" zinaweza kulindwa vipi kikatiba? Wanayohaki ya kuishi sexually kwa kufuata namna "orientation" yao inavyotaka kama vile sisi tulio "straight" tunavoishi? Pengine hii ingetosha kuwa mada tofauti kabisa lakini katika kuitizama rasimu katiba yetu ni muhimu pia suala hili likatizamwa/likajadiliwa.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom