RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Tumebimefanya kazi nzuri ila hapo kwenye Wabunge wawili kila jimbo hapana hatuwezi kukubaliana na upuuzi wa namna hii, hii ni katiba kwa miaka 50 ijayo isiandikwe kuwasaidia kina Sophia Simba kurudi Bungeni na kuwaachia watoto zetu urithi mbaya kana kwamba tulikuwa mazezeta. Nasema no wabunge wawili kwa jimbo moja.
 
More updates mlio karibu na redio na runinga
 
Hapo kwenye red tuipinge hii idea kwa nguvu zote, nani ataingia gharama kuwalipa lundo lote la wabunge hawa comedy show? idadi ya wabunge wa sasa inatosha sana.

mkuu Matola mimi mwenyewe jambo hili siliafiki hata kidogo,mbunge mmoja anatosha sana,kama wameweza kutoa viti maalumu kwa nini wanatuletea tena huu mzigo mwingine?ni nini mantiki ya kuwa na wabunge wa jinsia zote ktk kila jimbo?ni ktk harakati za kutafuta usawa au ni nini?na je usawa unatafutwa kwa kufanya km sisi tunavyotaka kufanya?we have to be very keen here na sio kukurupuka.
 
Last edited by a moderator:

Well said,binafsi sioni sababu ya kuwa na wabunge wawili kwenye jimbo moja eti kwa kigezo cha kubalance gender! Gharama zisizo za msingi,vile vile bado wamekumbatia ugonjwa mbaya sana wa madaraka makubwa ya raisi
 
Tume imepitisha serikali tatu yaani Tanganyika,zanziber na muungano. Rais kapunguziwa mamlaka,mambo ya muungano yamepungua toka 22 na kubaki saba tu.viti maalum wanawake vimefutwa na Wabunge wa kuteuliwa na rais wamepunguzwa toka kumi hadi 5 na watakaoteuliwa na Rais wanapaswa wawe Walemavu tuuuu. Tume huru ya katiba
 
Rasimu inapendekeza serikali tatu. Katiba ya Tanganyika wapi, na/au lini itatengenezwa?
 
Haya kama nilivyowatabiria miezi kadhaa zilizopita serikali imefufuka.

Acheni ujinga, Tanganyika imerudi bila katiba......wenzenu Zenji wana katiba na hii ya Warioba ni rasimu ya Tanzania, ya Tanganyika iko wapi
 
Kwa muono wangu kwa mapendekezo ya Tume ya Katiba juu ya aina ya Muungano kuwa wa Serkali 3 yaani serkali ya zanzibar, serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano yaliyotokea kule USSR yatajirudia hapa Tanzania tena ndani ya miaka 10 endapo pendekezo hilo litapitishwa. Binafsi suluhisho ya Muungano ni Serkali moja tu lasivyo Uvunjwe period.
 
Makamu wa raisi naye anapongeza ujinga... Watu wanapendekeza serikali tatu, alafu hawatoi muongozo kuwa serikali mbili kati ya hizo zianzeje?!!!
 
Mi nadhani hii tume ilazimishwe kutengeneza katiba za Tanzania bara na Zanzibar haraka sana, tena kwa gharama zao wenyewe. Haiwezekani watumie hela yote kufanya upuuzi kama huu!!!

Mkuu mimi pia nimepata utata kuwa hizo katiba zingine zitatoka wapi hususani Tanzania bara! Maana walau zanzibar wana pakuanzia,bado sijaelewa kabisa ngoja nivute subira
 
Htimaye Tanganyika yetu tuliyoiuza muda mrefu sasa tumeipata,sasa ni wakati wa kuwekana sawa.
 
serikali yenye mamlaka na itakayofahamika kimataifa ni ile ya shirikisho.
 
vipindi vya ubunge ni 3 urais je mbona hajasema
 
Ndiyo nini hicho? Serikali ya shirikisho, ya muungano na ya zanzibr, ndiyo mfumo gani huobwa utawala? I thought tutakuwa na serkali ya Tanganyika, ya zanzibar na ya muungano?
 
Rasimu inapendekeza serikali tatu. Katiba ya Tanganyika wapi, na/au lini itatengenezwa?

Mi ndio najiuliza sasa 2015 Tanzania bara tutajichaguliaje viongozi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…