RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Huu ni upuuzi mwingine, uwasa wa kijinsia hauji kwa ukuwa na idadi sawa ya jinsia bungeni, hao waliopo bungeni kwasasa wamefanya nini kuinsure wanawake wazao wanapata haki zao?
 
Last edited by a moderator:
Vyama vya upinzania hawapo?nani kawawakilisha?

mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa peter kuga mzirai amewawakilisha na amechukua rasimu moja kwa niaba yao na atawagawia vyama vyote na pia ukumbuke kuwa hii ni katiba ya nchi sio ya vyama
 
Safi sanaaaaa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
mgombea binafsi ruksa, kura za rais lazima ziwe more than 50%
 
Yaani wamependekeza serikali 3
Ya shirikisho...
Ya Tanzania bara...
Ya Zanzibar...

Alafu wakajiamulia kutengeneza katiba ya serikali moja (shirikisho) peke yake!!! Sasa hizo mbili wamemuachia nani?!!! Ebo!
Mkuu umerogwa kama unapinga rasmu hii.
 
nimefurahi serikali ya tanganyika imekuja. hongereni watanganyika na wazanzibar
 
Tanganyika is BACK

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
...sipati picha..Dr Slaa rais mteule wa tanganyika alfu rais wa muungano kikwete na rais wa pwani,no no no rais wa zanzibar of which najua itajitenga na pemba awe sefu...
 
Bado nafsi yangu haijaridhika...nilitaka Muungano uvunjwe ili kila mtu achukue chake tubakie na ujirani mwema tu; gharama za serikali tatu, masuala ya ardhi, uraia nk yataleta chokochoko.

Labda tuitumie nafasi ya serikali tatu kama njia ya kuelekea kwenye kuuvunja Muungano.
 
hawawezi kutengeneza rasimu ya tanganyika kwani kuna wa zanzibar kwenye tume
 
Mambo ya muungano
Katiba
Ulinzi na usalama
Uraia
Sarafu
mambo ya nje
Usajili wa vyama vya siasa
Ushuru wa bidhaa zinazotokana namambo ya muungano
Nawauliza mnatafuta utani na Maalim Seif?
 
Suala la rasilimali za taifa halijawa na jibu , rasilimali asili nani anamiliki!

Good question! Nilipoangalia rasilimali za taifa, nimebaki najiuliza, ina maana rasilimali zetu ni hizo tu? Kiswahili ambacho kinazungumzwa na karibu watu milioni kumi bado ni rasilimali ya kujivunia? Hatuna rasilimali za asili kweli?
 
Hata mi najiuliza. Na hizo serikali mbili (Tanganyika na Zanzibar), zitakuwa na mamlaka gani kimataifa?
mpaka katiba mpya kwanza itambue uwepo wa tanganyika ndipo tanganyika itaandaa katiba yake
 
Mkuu hebu msome huyu jamaa haswa hapo kwenye kipengele cha idadi ya majimbo na wabunge, nadhani utapata mwangaza
 
.
Chadema chukueni point hapa kuanzia sasa pigeni campaign kuwa Chadema kikichukua nchi kitaandika katiba ya Tanzania bara itakayofuta wakukuu wa wilaya na mkoa au kama italazimika kuwepo wapigiwe kura kama magavana.
.

Mi bado najiuliza katiba ya Tanzania bara itatengezwa lini. Wananchi wa Tanzania bara watachagua viongozi wao kwa sheria ipi?
 
.
Chadema chukueni point hapa kuanzia sasa pigeni campaign kuwa Chadema kikichukua nchi kitaandika katiba ya Tanzania bara itakayofuta wakukuu wa wilaya na mkoa au kama italazimika kuwepo wapigiwe kura kama magavana.
.
Labda wewe umeijuwa Chadema leo, hoja hii kwa mara ya kwanza iliwasilishwa na Freeman Mbowe bungeni mwaka 2000, mtu yeyote ambaye si mbulula anafahamu vyema kwamba uwepo wa chadema madarakani ndio mwisho wa hili genge la majobless so called RC na DC.
 
HIVI SASA, Ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na TBC1. mgeni rasmi ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE...
KATIBA MPYA KWA TANZANIA YENYE NEEMA
TUFUATILIE

Ulimwona wapi rais katika shughuli hiyo..... Au ulidhamiria nini???
 
Hii itakuwa demokrasia ya Tanzania, tutakipinga hiki kipengele hadi kibadirishwe kabla ya kura ya NDIYO NA HAPANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…