Yaani wamependekeza serikali 3
Ya shirikisho...
Ya Tanzania bara...
Ya Zanzibar...
Alafu wakajiamulia kutengeneza katiba ya serikali moja (shirikisho) peke yake!!! Sasa hizo mbili wamemuachia nani?!!! Ebo!
Mkuu naelewa. Ninachoona mimi ni kuwa huu mchakato wa katiba umefanywa ovyo kabisa ili 2015 ama tusiwe na uchaguzi, au tutumie ile ile katiba ya zamani.
Hebu jiulize; Mwaka 2014 hii katiba ya shirikisho ikikamilika, je 2015 Watanganyika tutapiga kura kuchagua viongozi wetu kwa kutumia sheria ipi? Tutatumia katiba ipi? Hiyo katiba itatengenezwa lini? Tume ya kutengeneza hiyo katiba itaundwa na nani? Endapo "Tanganyika" hatutafanya uchaguzi 2015, Je tutachagua raisi wa shirikisho na wa Zanzibar? Baada ya hapo Tanganyika itakuwa inaongozwa na nani (Kumbuka serikali ya shrikisho itahusika na mambo 7 tu)?
Nina wasiwasi kama ulielewa vizuri, hii ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naiman itabd tuwe na katiba ya nchi yetu ya Tanganyika. Humo tutakuwa na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wa Tanganyika, wabunge hawa 75 ni wa Bunge la JMT. Bunge la Tanganyika pia litakuwepo kujadili mambo ya Tanganyika km vile ZNZ walivyo na Baraza la wawakilishi..
Madaraka ya rais ndiyo yaliyasababisha nchi kuwa masikini japo tuna rasilimali nyingi. Tukitaka katiba yenye ufanisi katika mageuzi ya kiuchumi ni lazima madaraka ya rais yapunguzwe.
Kuhusu wabunge kuwa wawili katika kila jimbo huu ni uvivu wa kufikiri. Tanzania hatuhitaji kutoa hisani kwa watu wasio walemavu kwa gharama kubwa namna hiyo. Wabunge wapambane wake kwa waume na mwisho wa siku apatikane mshindi mmoja kuwakilisha jimbo.
.
Wewe unapendekeza iweje.
Wamewaachia wale ambao hawana katiba yao ili nao siku zijazo watengeneze katiba yao.
Ni kweli!Kwa ujumla wamefanya kazi nzuri sana, niwapongeze sana kwa uchambuzi makini pamoja na vikwazo walivyopambana navyo ila wamefanya kazi njema, mapungufu hayakosekani ndio maana itajadiliwa tena na bunge la katiba ili kuiweka sawa.
2015 tutafanya uchaguzi wa rais wa Tanganyika na Tanzania, ila katiba yetu itakuwa ipi sasa, zanzibar wenzetu wana katiba!
mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa peter kuga mzirai amewawakilisha na amechukua rasimu moja kwa niaba yao na atawagawia vyama vyote na pia ukumbuke kuwa hii ni katiba ya nchi sio ya vyama
wewe ni pimbi kweli? hujui kama zanzibar ina katiba yake? katiba ya tanzania bara itatengenezwa na watanzania bara wenyewe. sasa wewe unataka mambo ya bara yajadiliwe na wazanzibar? ebo
Tanzania bara hatuna katiba.2015 tutafanya uchaguzi wa rais wa Tanganyika na Tanzania, ila katiba yetu itakuwa ipi sasa, zanzibar wenzetu wana katiba!
Wabunge wa sasa ni wajumbe pia katika bunge la katiba. Ninaamini kabisa wataipinga hoja ya kuwa na bunge lenye wabunge 75, kwani wengi wao bado hawajalipa mikopo ya hela walizotumia kwenye kampeni
Hapo nafikiri labda hujapaelewa vizuri, mimi nafikiri wana hoja ya maana kwamba, kama Mbunge akifariki basi hakuna haja ya Uchaguzi ili kuokoa gharama, basi mrithi wake atatoka Chama kile kile tu, hivyo ina maana Chama chake watateua tu, badala ya uchaguzi kufanyika, kwa maana nyingine tunapaswa tuchague Sera za Chama na SIO mtu!
Mkuu hata mie naona hii ya serikali tatu yawezekana imechomekwa tu ili kwenye mabaraza ikataliwe wapate sababu ya kuendelea na serikali mbili maana haitamkwi TANGANYIKA ki uwazi ila wamechomela Tanzania bara kwa nini???????Kwa kweli mapendekezo mengi ya tume ni mazuri mno ila sina uhakika kama huko kwenye mabaraza ya katiba kama watayapitisha kama yalivyo mana huko kutatangulizwa maslahi ya ccm mbele.
duh kwa mantiki hiyo rais wa Tanganyika na wa Zanzibar watakuwa na mamlaka ya ndani ya nchi zao tu ila yule wa shirikisho ndiyo anakuwa overall kimataifaserikali yenye mamlaka na itakayofahamika kimataifa ni ile ya shirikisho.
Makamu wa raisi naye anapongeza ujinga... Watu wanapendekeza serikali tatu, alafu hawatoi muongozo kuwa serikali mbili kati ya hizo zianzeje?!!!