RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa


Kwani hatuwezi kuwa na Katiba ya watanzania bila ya ushiriki wa Tundu Lisu???? watanzania tuko milioni 40, usituambie rubbish hapa
 
Kitu kingine ni suala la ushoga! Nadhani wangeweka kipengele cha familia....
Familia iwe kwenye katiba...
 
Si tumeambiwa wahariri wamegawiwa? Waache uvivu si waiweke hapa? Manyerere Jackton wewe si ni Mhariri, tuwekee hapa
 
Last edited by a moderator:
tuwe wapole kwani kwenye hadidu rejea za tume kuna kipengele cha kuhakikisha rasimu tajwa inawafikia wananchi,leo ni uzinduzi tu.tuvute subra

mkuu umesahau kuwa upo Tz ambapo mambo mengi yapo vizur kimaandishi kivitendo hakuna utekelezaji,! So sina hakika kama hyo rasimu itawafikia hata nusu ya Wtz. Wakuu ikipatikana irusheni huku pls
 
haya ni mawazo yako siyo ya wazanzibar subiri wazanzibar watoe maoni yao.

Waz'br maoni yao walikwisha yatoa kwenye tume,ni mamlaka kamili,kinyume na hapo hapaeleweki.
 
Naomba ufafanuzi kuhusu wakuu wa mkoa/wilaya watakuwepo? Wanapatikanaje? Madaraka ya rais sijaona yamepunguzwaje. Kura za ushindi wa urais inakuwaje endapo aliyenda ana ushindi mdogo upande moja kwenye serikali ya shirikisho?
 

Hii tume imekuja na takataka tu eti mgombea akifa chama husika kitrue tu mtu!? Wataanza kuuana CCM! Achukuliwe mshindi wa pili!
 
Inatia matumaini

Yericko Nyerere Hapa naona tumepigwa changa la macho, vyeo vya kupena vitaendelea kuwepo inavyoelekea

 
kuna vetting ya wanaoteuliwa na Rais bungeni
 
Naunga mkono muundo wa serikali tatu lakini siungi mkono jina la "Tanzania Bara".
Tunataka jina la Tanganyika.......!!
Kwa nini tukubali kupoteza identity yetu wakati wenzetu wanailinda na kuipigania ya kwao??!!
Watanganyika tusikuballi ujinga huu!!!
 

Nakubaliana na wewe! paangaliwe upya hapa. Hvi vichwa vya tume ya walioba hawakuliona ili? any wanayomengi now time for them to look at it.
 
No comment on this for I know is just another silly constution!
 
HIVI SASA, Ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na TBC1. mgeni rasmi ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE... KATIBA MPYA KWA TANZANIA YENYE NEEMA

TUFUATILIE

Mimi kona ambayo sijaridhika nayo ni hao majaji wanaoteuliwa na raisi sikupenda sana nilitaka iwepo kamati maalumu ya mahakama iwateue.
Kitu cha pili ambacho nataka kiingizwe kwenye katiba ni mikataba yote inayosainiwa ya kuuza nchi iwe na maslai katika nchi kwa asilimia 80 na kuwepo na chombo maalumu cha kuikagua ufanisi wake na pia mikataba hiyo yote isiwe ya siri ianikwe kwa watanzania wote waisome na kuielewa.
Nawasilisha.
 
Muungano uvunjwe, uvunjike! Kama mke hakutaki (pamoja na kuwa na sura mbaya, masikini hohehahe hana kitu, mdini, mkabila) mpe talaka yake aondoke vinginevyo atakulisha sumu

Hapa inabidi Tundu Lissu avuliwe ubunge kwanza ndo move ya katiba itaenda smooth
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…