RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Majimbo yaunganishe/yapunguzwe na wachaguliwe wabunge wa Muungano ambao hawazidi 150. Tupunguze gharama za kuhudumia bunge - ni kubwa mno kwa sasa. Nawakilisha maoni yangu

Tume imependekeza wabunge 75, Tanganyika 50 Zanzibar 20, walemavu 5, wewe unataka kupunguza gharama kwa kuongeza wabunge kuwa 150.
 
*Waziri/katibu awe ana apply hyo kazi na c kuteuliwa na prez
*usalama wa taifa ufutwe maana upo kwa ajili ya ccm uundwe ambao strictly kwa taifa tu n' not kulinda ccm
 
wabunge wawili kila jimbo labda majimbo yapunguzwe sana kimsingi hakuna nchi inaweza ku finance huu ujinga.
 
idadi maalum ya wizara..
This can't be fixed maana kila serikali ina prioritiews zake, wengine wanapenda kuweka mining na energy pamoja, next inaweza kuamua kuziachanisha etc. Sijui kama kuna nchi imeweka a fixed number.
 
watz wote kuwa na siku maalum kwa kila mwaka kumhoji rais kuhusu ahadi zake!

wagombea urais kufanyiwa mdahalo, sasa tupo kidijitali zaidi hivyo hilo ni muhimu sana!
 
This can't be fixed maana kila serikali ina prioritiews zake, wengine wanapenda kuweka mining na energy pamoja, next inaweza kuamua kuziachanisha etc. Sijui kama kuna nchi imeweka a fixed number.


Marekani Rais hawezi ongeza wizara au punguza bila kuomba ruhusa ya bunge
au kuvunja na kuunga wizara fulani

Tanzania right now as we speak kuna waziri asie na wizara maalum..
 
Napinga kwa akili na hekima niliyokirimiwa na Mungu wangu jaji mkuu kuteuliwa na Rais! Kuna ujanja hapa...eneo ili lifanyiwe kazi na wahusika. Katiba mpya iweke bayana nini chakumfanya Rais anayeenda kinyume na katiba.

Then ndio eti anakuja kuwa bosi wa tume huru!
 
Binafsi naona kama hii rasimu imejikita zaidi kwenye upande wa siasa zaidi na kuna mambo mengine naona kam ahayakupewa kipaumbele mathalani Mfumo wa Elimu, Afya, Utalii na nyanja nyinginezo zisizohusika moja kwa moja na siasa

Naunga mkono hoja yako mkuu
 
Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye
kamati za Bunge.
Kwa walioelewa hapo naomba wanisaidie, inakuwaje Mawaziri wasihudhurie vikao vya bunge? Nani atakuwa anajibu maswali ya wabunge bungeni?
Kuhusu viti maalumu wangefanya iwe ni % flani ya wabunge wote, na wasitokane na vyama vya siasa na ikiwezekana wapatikane kwa kuomba hizo nafasi. Maana asilimia kubwa ya hawa wa sasa ni mizigo tu huko bungeni.
Kingine ni kuhusu kugombea urais na makamo wake, kwa sasa ni lazima kama rais katokea bara makamo atokee Z'bar, kwa upande wa mgombea binafsi itakuwaje? Atamchagua makamo wake baada ya kushinda au watagombea wote kwa pamoja?
 
Sauti ya umma kuhusu rasilimali zao, naona akina bush, xi ji , obama wanazitaka kwa udi na uvumba! hz rasilimali zitaleta machafuko nchini ukitazama kwa kina ndio kiini cha mgogoro uliopo kati ya serikali na wananchi na ndio turufu kubwa ya upinzani
 
Pia kuna suala la kuwa na spika wa bunge aliyechaguliwa, labda na wananchi asiye na mafungamano na chama chochote cha siasa kati ya vilivyo bungeni.

Suala la spika,rasimu inasema spika na naibu wake wasiwe wabunge,wala viongozi wa chama!ila mchakato wake wa kuwachagua ndio hawajauweka bayana

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Binafsi kwa haraka haraka mapendekezo ya tume ninayaunga mkono isipokuwa madaraka ya raisi lazima yafyekwe.
Sikubaliani na pendekezo la kiongozi wa mhimili wa serikali kumteua kiongozi mkuu wa muhimili wa mahakama. Raisi afanye mambo mengine kama kuteua mawaziri na manaibu wao lakini si kumteua jaji mkuu.
Nakubaliana nao kwamba raisi ateue wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama lakini sikubaliani na pendekezo la raisi kuteua wabunge watano hata kama ni walemavu, hilo ninalipinga.
Uwekwe utaratibu wa kisheria kuwawezesha walemavu wenyewe kuchagua wawakilishi wao wenyewe, vingineyo walemavu watakosa wawakilishi wanaojua shida zao watakaotetea maslahi yao.
Sasahivi kuna mbunge mmoja wa ccm Margreth Mkanga anatajwa kwamba anawakilisha walemavu lakini sijawahi kumsikia akiwasemea walemavu hata mara moja.
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone

Hujamsikiliza warioba haya yote yamo
 
Marekani Rais hawezi ongeza wizara au punguza bila kuomba ruhusa ya bunge
au kuvunja na kuunga wizara fulani

Tanzania right now as we speak kuna waziri asie na wizara maalum..
Oh, you mean hana ruhusa ya kuongeza wala kupunguza bila kuomba ruhusa bungeni? Maybe that.
but kusema leo hii constitution i-fix a number of ministry in the constitution itakua ngumu (IMO)
 
IGP aombe kwenye tume ya ajira asiteuliwe na rais

Kutakuwa na tume ya ulinzi na usalama ambayo ndiyo itakayomshauri rais kuhusu uteuzi viongozi wote wa ulinzi na usalama!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom