Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mkuu ahsante sana kwa kuanzisha hii nyuzi.Katika mkutano wake na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Rasimu ya Katiba leo Tarehe 03 Juni, 2013, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alimalizia hotuba yake kwa kusema kuwa "Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya www.katiba.go.tz."
Nimejaribu kuingia kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili niweze kujipatia nakala ya Rasimu hiyo lakini mpaka sasa sijafanikiwa kuiona. Wenzangu mmefanikiwa kupata nakala kwenye hiyo tovuti?
Nimeona baadhi ya watu wanatoa tathmini zao aidha kwa kusikiliza au kusoma hotuba ya Jaji Warioba ambayo ina kurasa kama 10 hivi. Lakini kwa mujibu wa Manyerere Jackton, Rasimu nzima ina kurasa 133 za A4.
Alichokisema Warioba ni summary ya rasimu siyo rasimu yote.
Ni jambo la kushangaza sana watu wanaanza kuchangia kwa kuangalia skeleton.
Mfano suala la Uraia limetajwa halikufafanuliwa sasa mtu anawezaje kuchangia suala hilo.
Ningewaomba watu wasikimbilie ku-define hii skeleton hadi rasimu yote itakapopatikana.
Sijaipata katika web yao kama kuna aliyeipata afaya maarifa kuwasiliana na Invisible itupwe hapa maana web za tz zina matatizo sana.