RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Katika mkutano wake na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Rasimu ya Katiba leo Tarehe 03 Juni, 2013, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alimalizia hotuba yake kwa kusema kuwa "Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya www.katiba.go.tz."

Nimejaribu kuingia kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili niweze kujipatia nakala ya Rasimu hiyo lakini mpaka sasa sijafanikiwa kuiona. Wenzangu mmefanikiwa kupata nakala kwenye hiyo tovuti?

Nimeona baadhi ya watu wanatoa tathmini zao aidha kwa kusikiliza au kusoma hotuba ya Jaji Warioba ambayo ina kurasa kama 10 hivi. Lakini kwa mujibu wa Manyerere Jackton, Rasimu nzima ina kurasa 133 za A4.
Mkuu ahsante sana kwa kuanzisha hii nyuzi.

Alichokisema Warioba ni summary ya rasimu siyo rasimu yote.
Ni jambo la kushangaza sana watu wanaanza kuchangia kwa kuangalia skeleton.

Mfano suala la Uraia limetajwa halikufafanuliwa sasa mtu anawezaje kuchangia suala hilo.

Ningewaomba watu wasikimbilie ku-define hii skeleton hadi rasimu yote itakapopatikana.

Sijaipata katika web yao kama kuna aliyeipata afaya maarifa kuwasiliana na Invisible itupwe hapa maana web za tz zina matatizo sana.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Naona kuna msamiati mpya. Washirika wa Muungano. Kina nani hawa?
Halafu hiki kipengele kimekaaje?
Tume pia, inapendekeza haki mpya ziingizwe kwenye Katiba ikiwa ni pamoja na haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki za Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu na Kujifunza, Haki ya kupata habari, Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari na kadhalika.

Soma manifesto ya waliberali "The Liberal Agenda for the 21st century" utaelewa vizuri.
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone

Mikataba kujadiliwa bungeni ni suala la kuwekewa kipao mbele kwa maslahi ya taifa maana hii mikataba inayosainiwa kisiri inatugarimu vizazi hadi vizazi
 
Hakuna kitu hapa, yani wakuu wa wilaya na mikoa sio swala la muungano na hawajatoa mapendekezo yao, sasa kwanini walituuliza?
Je la serekali za mitaa ni la muungano? mbona wamelitolea ufafanuzi?
 
Ni kweli!
ukiona mtu anapinga, ujue anawaza zaidi kuhusu hatima ya chama chake kuliko utaifa.Sijui atakapohama itakuwaje.
Naona kuna wengine wanasema hakuna jipya, hawajui kama haya mapendekezo yametokana na maoni ya wananchi na sio mtu mmoja.

Big up mkuu. Upo sawa kabisa. Nlichogundua hapa jf kuna wengi wanawaza hatma ya vyama vyao na sio hatma ya taifa letu. Huo ni upofu wa mawazo na maono ya mbali
 
Nimemkumbuka "Hutaki Unaacha",alitabiri ujio wa serikali tatu kwenye katiba mpya, Dr.Slaa kuwa Rais wa Jamuhuri,Lowasa Kuwa wa Tanganyika na Shaini Zenji.
 
Utawala majimbo ungeifanya tanzania kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda. Majimbo yatagawanya raslimali za taifa katika vipande vipande
Hoja hii ni dhaifu, kwa upande wangu naona wanahalalisha raslimali za nchi hii ziendelee kubaki Dsm na kwa katiba mpya ambayo haina sera ya namna raslimali zitakavyogawanya wale WA mikoa ya pembezoni Maisha yataendelea tu kwa magumu
 
This can't be fixed maana kila serikali ina prioritiews zake, wengine wanapenda kuweka mining na energy pamoja, next inaweza kuamua kuziachanisha etc. Sijui kama kuna nchi imeweka a fixed number.

Kenya mbona imeweka na imeweza!
 
Marekani Rais hawezi ongeza wizara au punguza bila kuomba ruhusa ya bunge
au kuvunja na kuunga wizara fulani

Tanzania right now as we speak kuna waziri asie na wizara maalum..

Inajulikana kama kutengenezeana kula
 
Wanajf,
moja kati ya vitu vilivyopendekezwa kuwepo kwenye rasimu ya katiba na tume ya warioba ni kufutwa kwa viti maalum the utaratibu uwe kwamba wanachaguliwa kutoka kwenye majimbo kama wawakilishi wa wanawake,
kama ilivyo utaratibu wa sasa kuwapata hawa wabunge kwa asilimia kubwa ilitegemea ni jinsi gani unawafurahisha mabwana zako(wakubwa wa vyama) na wala si wananchi maana wao hawakuwa na maamuzi kwenye kukufanya kuwa mbunge!

Lakini kwa sasa wananchi wana maamuzi katika kuchagua hawa wabunge(wanawake) kwa hiyo ushawishi wao ndo utawafanya wachaguliwe na wananchi,
tukiongelea kwa chama kama CCM kuwafurahisha mabwana na wapiga kura at the same time ni kitu kigumu sana,
sasa swali langu ni kwamba tutegemee kuona mabadiliko gani kwa hawa wabunge ambao kwa sasa wengi wao ni wale wa (ndiooooo, namsifu sana rais, namsifu sana waziri, naunga hoja mkono mia kwa mia wakati amoerodhesha matatizo kibao e.t.c)??????
Tukizingatia kuna suala la kuruhusiwa mgombea binafsi kwa maana kwamba hata kama chama hakitakuteua bado una chance ya kugombea kama mgombea binafsi na kama wananchi wamekukubali then utapita!

So tutegemee nini bungeni kwa sasa kwa hawa wabunge?
Je wataanza kutetea kwa nguvu zote maslahi wa wananchi hata kama watawakera wakubwa wa chama????? Wakiwa wanajua kabisa kwamba hata wakitoswa watgombea kama wagombea binafsi?
 
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.
Mimi nilidhani jimbo lichague Mbunge mwenye uwezo wa kuwakilisha bila kujali jinsia. Sasa haya mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya ni kuongeza gharama za matumizi ya fedha za umma bila sababu.
 
Nakuunga mkono rais asihusike kuteua majaji, tume ya utumishi ya mahakama ichague majina mawili ama matatu na yaingizwe bungeni kisha yapigiwe kura! Biashara ya rais kuteua wakuu wa mihimili mingine ya dola ni hatari kwa taifa letu!
 
Wa kwanza ni watanzania. Wamesikiwa,wamefikiwa.Wa pili ni Mchungaji Christopher Mtikila. Baada ya safari ndefu ya kimapigano kisheria,sasa Tanzania inakaribia kuwa na Wagombea Binafsi katika kila ngazi ya uongozi. Pia,Serikali ya Tanganyika inarudi.Hongera Comrade Mtikila!

Mshindi wa pili ni CHADEMA.Rasimu ya Katiba mpya inaakisi uwepo wa 'Majimbo' na kupunguza ukubwa wa Serikali hasa Baraza la Mawaziri.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilishaanza 'kupractice' suala hili. Kutakuwa na Majimbo 25 tu Tanganyika na 10 tu Zanzibar.

Mshindwa wa kwanza ni Zitto Z.Kabwe. Anaenguliwa rasmi kwenye mbio za urais 2015 kwa kukosa sifa za kiumri.Rasimu yataka mgombea urais awe na miaka isiyopungua 40.Mwaka 2015, Zitto atakuwa na miaka 39! Ubunge alishaaga,itakuwaje? Ataibukia kwenye uwaziri?

Mshindwa wa pili ni CCM na Serikali yake.Kama chama tawala tulikumbatia Serikali mbili;kukataza mgombea binafsi;kupinga vikali matokeo ya Urais kuhojiwa Mahakamani na kuwa na Mawaziri zaidi ya 50. Jaji Joseph Sinde Warioba ametuacha marikiti. Amependekeza uwepo wa mambo yote tuliyoyapinga kama CCM tangu Muungano ulipoasisiwa.

Washindwa wa tatu ni wazanzibari.Kwa Rasimu hii,badowazanzibari wamepigwa kumbo.Ni dhahiri kuwa Zanzibar haitafurukuta kama Serikali yenye mamlaka kamili mbele ya Serikali ya Shirikisho la Tanzania. Hawatakuwa na mamlaka kamili wanayoililia kila uchao.

Hatahivyo, hii ni Rasimu tu. Itajadiliwa na kupitishwa na ngazi mbalimbali. Yaweza kubadilika hata yote.Au kubaki kama ilivyo nakukataliwa na wananchi kwenye kura ya kuipitisha kuwa Katiba mpya.

Naendelea kuipitia Rasimu hii ili niyaone mema mengine.Mpira ndio kwanza unaanza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Soma manifesto ya waliberali "The Liberal Agenda for the 21st century" utaelewa vizuri.

Gays n lesbian! Haki za makundi madogo kwenye jamii! Wange specify to kuliko kuficha mambo..

we have a long way to go!

Infact,ukitaka kula lazma uliwe kidogo! Source......hahahaha!
 
Back
Top Bottom