RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Twende pamoja wazee, suala la wabunge 75 (50 bara, 20 znz na tano walemavu) ni kwa serikali ya muungano (shirikisho) na suala la wabunge wanawake kila jimbo maana yake orodha ya juu hapo ni nusu kwa nusu (usiniulize hao 5 wa walemavu watagawika vipi) mipaka ya majimbo hayo itaamuliwa baadae

Muhimu ni kuwa mipaka ya majimbo ya sasa kwa maana Bara na visiwani kwa serikali za Tanganyika na Zanzibar itaamuliwa pia na serikali husika kwenye katika zao baadae. Hoja yangu hapa ni kuwa kwa huku bara bado tutakuwa na majimbo zaidi ya 200 hayo utaratibu wake utaamuliwa na serikali ya Tanganyika huko mbeleni. Angalizo ni kuwa hiyo formula ya viti vya akina mama kwa upande wa serikali ya Tanganyika tutaamua wenyewe ama kubaki na formula ya sasa au ku adopt formula ya muungano yaani pasu kwa pasu.

Ninachokiona mimi ni mzigo mkubwa wa serikali 3 mabunge matatu, marais watatu, mabaraza ya mawaziri matatu shughuli pevu
 
Rasimu hii haijakidhi matakwa ya Watanzania. Ni ukweli usiopingika kuwa mchakato wa kukusanya na kuaandaa rasimu ulibakwa na walio madarakani. Zaidi ya mwaka mzima wanafanya kazi na kulipwa mamilioni ya shillingi harafu wanakuja na rasimu ambayo imewacha watanzania wakijiuliza lipi jipya hapa?Japo kenya wamepata katiba mpya kwa kumwaga damu, katiba yao ilikidhi matakwa na mahitaji ya kenya kwa miaka 50 ijayo. Tanzania aibu tupu... katiba hii mpya haiwezi kutosegeza hata miaka 2 mbele. Inakuwaje rais apewe nafasi 5 za kuteua wabunge? Haki hii ni ya watanzania kuchagua na lengo ni kuondokana na vyeo hivi vya kuteuliwa. Mambo ya uraia katika nchi nyingi duniani yameandikwa ndani ya katiba kwa kuwa ndiyo sheria mama. Warioba vipi tena? Anasema eti itungwe sheria ya uraia? Hopeless guy and his team. Hatuna katiba mpya maana haiwezi kupita kwenye kura ya maoni, wameacha mianya mingi wakati watanzania walitoa maoni yao. Vipi kuhusu, TAKUKURU, CAG, AG, DPP, raslimali zetu, mambo haya yanatakiwa ya ainishwe kwenye katiba. Katiba isipo yatamka nani atayasimamia?I'm very dissappointed in Warioba and his team. Wametuaibisha watanzania, kumbe nao wanafikiri kwa tumbo.
mkuu tuliza munkali hayo ni baadhi tu ya mambo ukipata rasimu nzima ndo utoe maoni hayo bt abt maliasili mikata yote itajadiliwa na bunge inshort
 
Mkuu bado katiba ya tanganyika kwani hili si bunge la jamhuri? Bado lile la Tanganyika nalo litakuja na mambo yake...
 
YA ZAMANI


///////////////////////
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo


MAPYA
/////////////////////////

  1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  3. Uraia na Uhamiaji
  4. Sarafu na Benki Kuu
  5. Mambo ya Nje
  6. Usajili wa Vyama vya Siasa
  7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.



NOTE: NECTA OUT

 
Hii Rasimu kwa ujumla ni kiini macho.
Eti Raisi anateua Jaji Mkuu na Makamu wake, halafu hao hao ni wenyeviti wa tume huru. Nonsense! Halafu wamechelea kusema nyadhifa za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ziondolewe, hapa kuna mkakati mchafu. Siwaamini hawa jamaa wa CCM aisee. They have a secret agenda. Hapa uchambuzi makini unatakiwa sana. Hili ni eneo limetapakaa wanajeshi wastaafu, kuna ubabe, vurugu, ujanja ujanja, vitisho, ulaghai mwingi, ukachero na kila aina ya uchafu. Raisi wa CCM angependelea sana kubakia na madaraka ya kuwateua hawa jamaa. Humo ndimo ushindi wa kuchakachua kura unakopikwa na kutokea. Hilo ndilo bomba la maji taka chini, nina maana siasa taka chafu na zenye kunuka ndimo zinakopitishwa. Nasema yale majukwaa ya Katiba yaanze mara moja kumpasha Jaji Warioba.
Wasifanye watu wajinga. Kwanini watu wasipeleke maombi ya kazi na ikafanyika Public vetting kumpata Jaji Mkuu na Makamu wake??????? Nini kinataka kufichwa hapo?? Ili wakishachakachua hata mgombea Uraisi aliyeshindwa kwa kuchakachuliwa kura asiweze kushinda kesi. siyo??? Hapana tunataka rasimu itakayo turejeshea matumaini.
Na je Tanzania bara ni nchi gani hiyo? Jina Tanzania lilitokana na nini?? Siyo Tangayika na Zanzibar??? Sasa iweje leo kuwe na serikali tatu, moja iitwe Zanzibar (imerejeshewa jina original) na Tanganyika isiwepo??? Tunaambiwa tuifute Tangayika vichwani au?? Hapa hapaeleweki kidogo, eti Tanzania Bara (Tanzania Mainland Government right?), why not Tanganyika Government?
 
katiba ni nzuri ila pale walipo anza kusema haya ni masuala ya muungano tu nadhani hawakutenda vema
 
wanataka usawa ndo huo,sio mtu anapongeza tu na kusifu ujinga ukifatilia kumbe ndo walewale
 
Acha upuuzi, anakuwa tayari ameletewa qualifying... yeye anakuwa appoint mmoja kati ya watata etc... there is no issue with this guys,,, tujadili vitu vyenye maana.

Kwani kwa sasa majaji wanapatikanaje?
 
Bora kuwa na mzigo wa serikali 3 angalau unaeleweka, kuliko kiinimacho tulichokuwanacho awali.
 
Hii rasimu ya katiba ni useless
Maana kama inapendekeza serikali tatu, lakini haitoi rasimu ya serikali mbili kati ya hizo, sasa ina kazi gani?!!!

Hivi umesoma hadi darasa la 4 nini? kama hujui uwe unauliza kwanza. Tume inafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ambayo inaipa mamlaka ya kuratibu na kusimamia MABADILIKO YA KATIBA YA MUUNGANO na sio katiba ya bara wala ya zenji... hizo serikali mbili unazosema [ bara na zenji]... haina mamlaka hayo. labda badili sheria uipe mamlaka hayo. hizo katiba zingine zitashugulikiwa na serikali za ushirika kwa taratibu zao za ndani pindi zitakapoundwa na endapo rasimu hii ya katiba itakubalika na watanzania. lakini Upende usipende, katiba hizo za washirika [ya bara na ya zenji] lazima zisipingane na misingi mikuu ya katiba ya muungano ambayo ndio kaka mama na baba yao. period.
 
sijaipenda kwenye vipengere hv

......tume huru ya uchaguzi
......uteuzi wa majaji.
......wakuu wa vyombo vya usalama watakavyopatikana.

nimeipenda kwenye vipengere hv

........serikari tatu
........mgombea binafsi
........kutokuwepo kwa uchaguzi mdogo.
 
Wakuu imetolewa au bado? Sababu hii sio official........ Sasa kina kamata wanakula wapi 2015
 
Kinga ya rais waiondoe, hasa kwa hawa mafisadi.
 
Hapa mimi bado naona hakuna tume huru ya uchaguzi maana bado raisi anahusika katika uteuzi.
Pia rais bado madaraka yake hayajapunguzwa hata tone sasa sijui inakuwaje au warioba kaogopa kumgusa bosi wake wakati sisi tumetoa maoni??
 
Nafikiri kutakuwa na wabunge wengi,yaani kila jimbo liwe na wabunge wawili? Mh Nahitaji kusaidika ili nielewe.
 
Yaani hawa wamekula pesa za walipa kodi wa nchi hii..wanakuja na usanii huu!
Usanii mtupu, raisi ateue jaji mkuu! mbunge akifa wa chama chake achukue nafasi!!!!! Sio mshindi wapili!!!
 
Back
Top Bottom