RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

mikataba ichapwe kwenye magazeti.

tutmie kiswahili mashuleni
 
wameongeza mzigo wa wabunge wanawake. inamaana hakutakua tena na mchuano kati ya wanaume na wanawake? kwa nini hao wanawake wasiwawekee nafasi za mikoa badala ya jimbo? tutakuwa na wabunge zaidi ya 600, gharama zimepungua? aafu mbona mambo ya rais kuteua bado yapo? kuna utofauti gani na katiba ya sasa? ikitokea rais mwingine kama jk asiyesikiliza ushauri wa tume na kuteua hawara zake tutakuwa tumeepuka nini?

hii ni rasimu ya muungano imependekeza bunge liwe na wabunge 75... 50 bara, 20 visiwani na 5 walemavu wateule wa rais. Majimbo 25 kwa bara na 20 kwa visiwani na kila jimbo litakuwa me na ke. Tusubr katiba ya bara itasemaje.
 
Mi nadhani wamejitahidi vya kutosha. Kinachotakiwa ni kuboresha rasimu hii. Nin imani kubwa kuwa katiba nzuri ya Muungano itapatikana. Baada ya katiba ya muungano kupatikana nadhani haitakuwa shida kupata katiba za washirika wa muungano. Mungu ibariki Tanzania
 
HIVI SASA, Ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na TBC1. mgeni rasmi ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE... KATIBA MPYA KWA TANZANIA YENYE NEEMA

TUFUATILIE

Usanii mtupu,wamependekeza serikali ya shirikisho lakini sasa hayo mambo waliyoyaweka ya mungano hilo shirikisho litatokea wapi?
 
Sijui kama wenzangu mmeiona hiyo, maana sijasoma maoni ya wachangiaji wote.Kuhusu muundo wa muungano labda wajumbe wa tume wamekosea au makusudi wamependekeza serikali za shirikisho la Jamuhuri ya muungano,serikali za jamuhuri ya Zanzibar na Serikali za Tanzania bara. Na hili mimi ni naliunga mkono mia kwa mia, ila tatizo hili jina TANZANIA BARA silihafiki kabisa kwa kuwa huu muungano wa sasa ni wa nchi mbili ambazo ni TANGANYIKA NA ZANZIBAR. Kwa hiyo napendekeza hili Jina TANGANYIKA LIBAKI KAMA LILIVYOKUWA kabla ya tarehe 26 APRILI 1964.
 
Serikali yetu ya Tanganyika wazanzibar basiiii.. Sasa muende kufanya kazi kwenu...wabunge walioko bungeni sasa basi imetosha, sasa mtakuja wachache kwenye bunge la jamhuri ya muungano. Mpeleke mambo yenu kwenu sasa...

waache wakaanze kazi mapya. tunawatakia heri..........
 
Katika michakato na mapambano ya kisiasa na ya kitabaka,aghalabu huwepo mikingamo juu ya mawazo na matarajio.Kutokana na ukweli huo,si rahisi,na kwa kwa kweli haitarajiwi,pande zinazopambabisha fikra na mawazo kukubaliana ama kutokubaliana katika kila jambo.Sasa,kama tutaitazama Rasimu ya Katiba kwa jicho la kisiasa ,kwa maana ya tofauti za wazi za kiitikadi na kifalsafa,kinadharia,kimtazamo na kimwelekeo,kadiri zinavyowatofautisha washiriki wa kisiasa kimatendo na kimazoea,haitastaajabishi hata kidogo,kuona wanachama,wapenzi na viongozi wa vyama mbalimbali wakiipokea rasimu hiyo kwa hisia na mitazamo tofauti.
Yawezekana kabisa baaadhi ya wanachama,wapenzi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi watapendezwa na kuchukizwa na maudhui ya baadhi ya Ibara fulani za Rasimu ya Katiba,mathalani,''uwepo wa mgombea binafsi'' ama hata ''muundo wa Muungano''.Hali hiyo hiyo,inatarajiwa kujitokeza kwa wanachama,wapenzi na viongozi wa vyama vya UPDP, CHADEMA, NLD nk., katika maeneo hayo na mengine.Hii ni kweli kwa kuwa,mosi,tunayaelewa na kuyatambua mapendekezo na misimamo ya baadhi ya vyama vya kisiasa hapa nchini na pili,tunaelewa na kutambua kuwa hoja za kisiasa katika kipindi cha kati ya 2010 na 2013,kutokana na sababu zinazoeleweka bayana,zilichukua nafasi kubwa katika uwanja wa kisiasa kadiri ya agenda ya Katiba Mpya na kufanya mapendekezo na misimamo ya makundi mengine yaliyopo katika jamii hapa nchini,kama vile tabaka la wafanyakazi na wakulima,wavuja jasho,kutokupata usikivu stahiki ingawa hii si lazima imaanishe kuwa maoni ya tabaka hili muhimu hapa nchini yamezingitiwa ama hayakuzingatiwa.Hali hizo kwa kweli zilitarajiwa na kwa hakika kutaraji vinginevyo ni jambo lisiloshawishi akili na lisilokubalika kimantiki.Hiyo ilitarajiwa kwa kuwa mchakato wa kupata rasimu na hatimaye katiba mpya hauwezi kuzingatia maoni ya wadau wa kisiasa pekee ingawa ushiriki wao hauwezi kupuuzwa.
Ishara ya kutia moyo imejitokeza wazi nayo ni kwamba mara baada ya maudhui makuu ya Rasimu ya Katiba kuwekwa bayana wadau mbalimbali,hasa wa kisiasa,wanaonyesha kufurahia na papo hapo kutofurahia baadhi ya maudhui ya Ibara za Rasimu hiyo.Hii ni hatua muhimu kwa kuwa hatimaye Katiba Mpya ni nyenzo ama taasisi ya kusimika na kuimarisha mwafaka wa Kitaifa,utakaozingatia maslahi mapana na ya muda mrefu ya watu wa taifa letu bila kujali tofauti zinazojitokeza katika itikadi,falsafa,imani,nadharia,maslahi,matamanio na matarajio miongoni mwa wananchi.
 
Mkuu, hiyo ni kama kiini macho!
Mapambano bado sana kama kweli mnataka katiba mpya itakayokuwa na maslahi kwa watanzania wote.
Ngoma ndo kwanzaaaaaaaa imeanza!
Bado mbichi sana aisee

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sasa tutakuwa na viongozi full wa Tanganyika huru.. Hatuhitaji tena mseto kwenye Tanganyika yetu..
Slaa Rais zitto makamu, mbowe waziri mkuu, tundu lisu mwanasheria mkuu, lema Mambo ya ndani, Abdalla safari sheria na katiba, Ally banaga kazi vijana, silinde tamiseni, lema mambo ya ndani, Nasarri sayansi na Teknolojia... Suzan elimu ...
 
Kwa maoni yangu nimefarijika kwa kiwango cha kutosha na imani yangu kwao imerejea. Nawaomba sasa wasiichakachue wale wanaoitwa makada watiifu walochukua nafasi zao katika mabalaza....
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone
Ww hujasoma ile rasimu wala hujasikiliza hotuba ya warioba, kiswahili kipo kwenye tunu za taifa na ni lugha ya taifa...bunge litajadili mambo yote mhm ya nchi na kuna serikali tatu, mikataba itajadiliwa kwny serikali ya tanzania bara na ya znz
 
Nasikitika watu humu wanachangia wasivyovielewa, mambo mengi mnayodananama humu yameaemwa na warioba
 
Nendeni kwenye ile thred ya rasimu ya katiba acheni kudanganyana hapa
 
Nampongeza warioba, nampongeza kikwete naipongeza ccm, naeapongeza watanzania, tz tunayoitaka ileeeeeee!!!!!!
 
Back
Top Bottom