RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Ccm wamegundua 2015 hawana lao..ndo maana wameacha vipengele vingi vya kuwalinda.
 
Mimi bwana kero yangu ni ya kijinga sana. Yaani nakereka ninaposikia hilo neno Zanzibar. Sababu ya kukerwa na hilo neno ni kuwa kimsingi Zanzibar ilikufa kama ilivyokufa Tanganyika, hebu cheki Warioba anaponikera anaposema "baada ya yote hayo tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa serikali tatu, yaani; serikali ya shirikisho, serikali ya Tanzania bara na serikali ya mapinduzi Zanzibr" sasa najiuliza kama zamani hii tunayoiita Tanzania bara iliitwa Tanganyika kwanini hiyo wanayoiita Zanzibar isiitwe Tanzania visiwani? Kama hawawezi kuua hilo jina muungano si ufe tu?
 
Mimi bwana kero yangu ni ya kijinga sana. Yaani nakereka ninaposikia hilo neno Zanzibar. Sababu ya kukerwa na hilo neno ni kuwa kimsingi Zanzibar ilikufa kama ilivyokufa Tanganyika, hebu cheki Warioba anaponikera anaposema "baada ya yote hayo tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa serikali tatu, yaani; serikali ya shirikisho, serikali ya Tanzania bara na serikali ya mapinduzi Zanzibr" sasa najiuliza kama zamani hii tunayoiita Tanzania bara iliitwa Tanganyika kwanini hiyo wanayoiita Zanzibar isiitwe Tanzania visiwani? Kama hawawezi kuua hilo jina muungano si ufe tu?
Mzee wa ngano sisi wanzibar ndio tunvyotaka muungano ufe tuuu hatuoni maslahi yoyote ya muungano, mwambieni baba yenu warioba hatutaki tena kutawaliwa kila chenye mwanzo kina mwisho uyo muanzilishi wa muungano nyerere, kafikia mwisho wake what about muungano, uvunjwe kila mtu awe na serikali yake asilazimishe.
 
Nanukuu kutoka kwenye rasimu mpya ya Katiba
"KILA JIMBO LA UCHAGUZI LITAKUWA NA WABUNGE WAWILI MMOJA MWANAUME NA MWINGINE MWANAMKE"
Swali langu ni Je, Mishahara yao na gharama zao zitalipwa kutoka wapi?
Si ndio tutaendelea kuminywa hadi tukione cha mtemakuni katika nchi yetu wenyewe?
Kwani neno "Mbunge" lina maana gani kiuhalisia?
Kuna umuhimu wa kila Jinsia kuwa na uwakilishi wake bungeni kwa kila jimbo?
La hasha, watu wamekaa na kuona Ajira imekuwa tatizo la kudumu hata kwa "wake zao" wakaona waweke nafasi za kazi chache kwa "watu wachache" ili kuwe na unafuu......
Sitegemei kulala kwa sasa napitia kifungu hadi kifungu, Mungu wa Mbinguni awabariki sana!
 
Narudia tena Kabla ya tarehe 26 Aprili 1964 kulikuwa kuna nchi iliyokuwa ikiitwaTanganyika na si Tanzania bara. Msikubali kupotoshwa.
Hilo mkuu binafsi limeniuma sana, nilitegemea kuliona jina la nchi yangu yangu ya asili lakini wameniletea jina lilelile linalonikwaza sana!
 
Nakuunga mkono ndugu! Hata mie kipengele hicho nilikiwekea nyota! Plus hiki .... "Kuhusu Mahakama inapendekezwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (Supreme Court) Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama." Nafikiri ibakie tu iyo tume ya Utumishi wa mahakama ipewe nguvu zote. Na kazi ya uteuzi iwe wazi kwa public, kama ilivyo Kenya kwy katiba yao mpya. Wanafanyiwa interview wakati umma wote unaona. Tuachane na hii dhana ya watu kufanya kazi wakimuogopa mtu mmoja aliyewaweka kazini. Ifike hatua watu wa sehemu nyeti kama iyo waone wanawajibika kwa wananchi sio kwa mtu mmoja
 
mbona unaonekana huna unachojua,viti maalumu hakuna isipokuwa viti maalum vitakuwa kwa wenye ulemavu,wananchi wanauwezo wa kumfukuza mbunge kama wataona hafai,mbunge wa kuchaguliwa akifa kama alitokana na chama hakuna uchaguzi chama kitapendendeza mwingine,kama alikuwa ni mgombea binafsi uchaguzi mdogo utakuwepo.

vilaza wengine bana......kazi kumeza tu!......toa maoni usiwe mdandiaji tu
 
Rasimu imeacha mambo ya msingi mengi tu kubainisha kwa maoni yangu
1. Rasilimali za Nchi (Ardhi na Madini, Mafuta, gesi) haina budi kutamka bayana umiliki na faida zake
2. Mawaziri kutokuwa wanasiasa hili lazima liwe open bila chenga
3. Sioni mantiki ya kutaja umri wa Rais pasipo kutaja kiwango cha elimu yake; kwa kifupi hatutarajii kuwa na Rais au watendaji wakuu ambao ni 'undergraduate' (kujua kusoma na kuandika) ikiwa directors tu lazima wawe postgraduates
4. Imetaja kiswahili kama tunu ya taifa kwa maana inaleta umoja, lakini ilikuwa itaje wazi Kiingereza ni Lugha ya kufundishia katika level zote za elimu na pia official language, hii tusipepese macho-dunia iko katika vita ya utawazi ambao msingi mkubwa ni elimu na nguzo ya elimu ya utandawaizi ni kimombo
5. Haina maana kutaja wabunge wanaume au wanawake then kuacha sifa ya kujua kusoma na kuandika ili wakaendelee kupiga meza; kiwango cha elimu ya mbunge kibainishwe
6. Tume iliambiwa iandae Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio katika ya muungano, kwa maana ilitakiwa mambo yalioko ndani ya muungano yabainishwe au yatolewe ushauri (U-DC, RC Division Officers etc) maana kwa sasa kuna mlundikano mkubwa sana wa vyeo katika eneo moja; Tume watoe majibu isjie kuwa Pesa zote walizokula wameenda kuandaa misingi ya mambo saba tu, uhuni huu
7. Katiba ijibu kilio cha uwazi na upatikanai wa taarifa za Serikali katika masuala yote (hususan Mikataba ya Rasilimali za nchi isiwe siri, ijadiliwe na chombo mahsusi ili ikifanywa kisanii tunaju ni hicho chombo ndio kimefanya "uchenge" na iwekwe wazii, hakuna sababu za kuficha mikataba ya rasilimali ni janga)
8. Kada zote za juu zisiwe za kuteuliwa bali ziwe za kushindaniwa
9. Hili la wabunge 2 kwa jimbo siliungi mkono lakini nashawishika kulikubali kwa kuwa sina "alternative ya kuwa na mfumo bora wa kuweza kupata wabunge wanawake jimboni) na idadi yao inanishawishi. Hata hivyo, inategemea na muundo wa Serikali za tanganyika na Zanzibar ili kujua wapiga meza watakuwa wangapi
10. Katiba iwe wazi katika kulinda na kutetea haki za wananchi ili kuepusha ubabe wa polisi kwa raia simply wanachukuliana mabwana/mabibi; hili lianishwe vema haki za raia
11. Muundo wa mamlaka za juu za uongozi wa nchi kwanini hazina mapendekezo?
Kwa kifupi, Raimu ni tupu, ingefaa hata kuboresha iliyopo kama haitataja maeneo ya msingi kama baadhi hapo juu.

Thats why I love JF.......Mkuu Heshima mbele......maoni safi kabisa.....
 
9. Hili la wabunge 2 kwa jimbo siliungi mkono lakini nashawishika kulikubali kwa kuwa sina "alternative ya kuwa na mfumo bora wa kuweza kupata wabunge wanawake jimboni) na idadi yao inanishawishi. Hata hivyo, inategemea na muundo wa Serikali za tanganyika na Zanzibar ili kujua wapiga meza watakuwa wangapi

Mfumo bora wa kuweza kupata wagombea bora ni kutengeneza mazingira sawa kwa wote ya kugombania nafasi ya/za uwakilishi majimboni.

Habari za lazima sijui mbunge mmoja awe mwanamke na mwingine awe mwanaume ni upuuzi mtupu. Mbona kwenye urais hawajaweka hayo mambo?

Kwamba lazima wanawake na wanaume wapokezane - yaani rais akiwa mwanaume basi mwanamke lazima awe makamu wake na mwanamke akiwa rais basi makamu wake lazima awe mwanamme na iende hivyo kwa zamu kila muhula wa uchaguzi na mmoja wapo akimaliza muhula wake kama rais basi safari ijayo lazima mgombea / wagombea urais wote wawe wa jinsia tofauti na wale wanaomaliza muda wao ili kuleta usawa na uwiano baina ya jinsia.

See how absurd and ridiculous that sounds?
 
Zitto Z.Kabwe. Anaenguliwa rasmi kwenye mbio za urais 2015 kwa kukosa sifa za kiumri.Rasimu yataka mgombea urais awe na miaka isiyopungua 40.Mwaka 2015, Zitto atakuwa na miaka 39! Ubunge alishaaga,itakuwaje? Ataibukia kwenye uwaziri?
 
hili bunge litakua na wabunge wangapi kama kweli tunataka tuwe na wabunge wa2 wa kiume na kike?
kwa nini wasishindanie nafasi moja badala ya kujaza wabunge wengi kiasi hicho ambao watakua wanatumia kodi nyingi za watanzania?
 
Wakuu,
Mchakato wa Kutengeneza Katiba yetu ya Tanganyika unaanaza lini??????
Cant wait to be not a Tanzanian Citezen, Rather, Citizen wa Tanganyika

cant wait kuwa raia wa Tanganyika, Cant Wait kuona Bendera yangu ikipepea, yaaan kuimba wimbo wangu wa Tanganyika...du nina Furaha kweli...
Ila maswali bado najiuliza, Hii Ikulu ya Magogoni itakuwa ya Muungano au ya Tanganyika? Hivi haya madeni ya nchi yaliyopo yatalipwa na Tanganyika, Zanzibar au Tanzania?mh maswali nayo ni mengi sana..
 
Back
Top Bottom