Rasimu imeacha mambo ya msingi mengi tu kubainisha kwa maoni yangu
1. Rasilimali za Nchi (Ardhi na Madini, Mafuta, gesi) haina budi kutamka bayana umiliki na faida zake
2. Mawaziri kutokuwa wanasiasa hili lazima liwe open bila chenga
3. Sioni mantiki ya kutaja umri wa Rais pasipo kutaja kiwango cha elimu yake; kwa kifupi hatutarajii kuwa na Rais au watendaji wakuu ambao ni 'undergraduate' (kujua kusoma na kuandika) ikiwa directors tu lazima wawe postgraduates
4. Imetaja kiswahili kama tunu ya taifa kwa maana inaleta umoja, lakini ilikuwa itaje wazi Kiingereza ni Lugha ya kufundishia katika level zote za elimu na pia official language, hii tusipepese macho-dunia iko katika vita ya utawazi ambao msingi mkubwa ni elimu na nguzo ya elimu ya utandawaizi ni kimombo
5. Haina maana kutaja wabunge wanaume au wanawake then kuacha sifa ya kujua kusoma na kuandika ili wakaendelee kupiga meza; kiwango cha elimu ya mbunge kibainishwe
6. Tume iliambiwa iandae Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio katika ya muungano, kwa maana ilitakiwa mambo yalioko ndani ya muungano yabainishwe au yatolewe ushauri (U-DC, RC Division Officers etc) maana kwa sasa kuna mlundikano mkubwa sana wa vyeo katika eneo moja; Tume watoe majibu isjie kuwa Pesa zote walizokula wameenda kuandaa misingi ya mambo saba tu, uhuni huu
7. Katiba ijibu kilio cha uwazi na upatikanai wa taarifa za Serikali katika masuala yote (hususan Mikataba ya Rasilimali za nchi isiwe siri, ijadiliwe na chombo mahsusi ili ikifanywa kisanii tunaju ni hicho chombo ndio kimefanya "uchenge" na iwekwe wazii, hakuna sababu za kuficha mikataba ya rasilimali ni janga)
8. Kada zote za juu zisiwe za kuteuliwa bali ziwe za kushindaniwa
9. Hili la wabunge 2 kwa jimbo siliungi mkono lakini nashawishika kulikubali kwa kuwa sina "alternative ya kuwa na mfumo bora wa kuweza kupata wabunge wanawake jimboni) na idadi yao inanishawishi. Hata hivyo, inategemea na muundo wa Serikali za tanganyika na Zanzibar ili kujua wapiga meza watakuwa wangapi
10. Katiba iwe wazi katika kulinda na kutetea haki za wananchi ili kuepusha ubabe wa polisi kwa raia simply wanachukuliana mabwana/mabibi; hili lianishwe vema haki za raia
11. Muundo wa mamlaka za juu za uongozi wa nchi kwanini hazina mapendekezo?
Kwa kifupi, Raimu ni tupu, ingefaa hata kuboresha iliyopo kama haitataja maeneo ya msingi kama baadhi hapo juu.