Kuna mambo ambayo rasimu imetoa majibu ya maswali yako, mengine hayana majibu.
Kimsingi, hakuna cheo cha WAZIRI MKUU. Kimekufa, na kilikuwa hakina maana yoyote kwa sababu makamu wa raisi alikuwepo.
Kuhusu wizara; Wizara 15 ni nyingi kwa sababu mambo ya muungano ni machache. Mambo ya muungano ni kama ifuatavyo.
- Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – WIZARA YA KATIBA
- Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – WIZARA YA ULINZI, WIZARA YA MUUNGANO
- Uraia na Uhamiaji – WIZARA YA MAMBO YA NDANI
- Sarafu na Benki Kuu - ????????
- Mambo ya Nje – WIZARA YA MAMBO YA NJE
- Usajili wa Vyama vya Siasa – Hakuhitaji wizaraa hapa, inahitajika taasisi inayojitegemea.
- Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano. – haihitajiki wizara.
Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu; serekali ya jamuhuri ya muungano inatakiwa iwe na wizara sita au saba hivi basi.
Kuhusu mapato; Zanzibar tayari ina Zanzibar Revenue Board (ZRB) na Tanganyika nayo iwe na TRB yao ili kushughulikia ushuru wa bidhaa yasiyotokana na mambo ya muungano.
Kwa kweli hakuna maelezo kuhusu CAG. Lakini nadhani kwa vile mambo ya muungano ni machache tu, mambo nyeti na yanayomgusa mwananchi wa kawaida kama, afya, miundombinu, rasilimali (???), elimu, kilimo, nk yako mikononi mwa serikali za washiriki wa muungano, kila mshirika atakuwa na CAG wake.