RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Kwa siasa za Tanzania, ni jambo gumu sana kuwa na katiba ya Tanganyika kabla ya mwaka 1015. Hata hivyo, maoni ya watanganyika kuhusu katiba ya Tanganyika tume ya katiba wanayo, kwa hiyo ni kiasi tu cha kukaa chini kwa mwezi mmoja na kuyaweka katika maandishi kama hii katiba. Ila, siasa za Tanzania na watu wanavyopenda sitting allowances, inaweza ikachukua mpaka 2020 ndio Tanganyika ipate katiba yake.
Kuhusu Tanganyika vs Tanzania bara. Ni woga wa watawala na kutokuwa objective katika kuwa wazi. Jina halisi la Tanzania bara ni TANGANYIKA, na wanatakiwa wawe BOLD kabisa. Jina Tanzania lilikuja baada ya muungano ulioasisiwa mwaka 1964, which means Tanganyika was there before and it was supposed to be there to stay. Hata hivyo, ulimwengu mzima watu wa visiwani wana inferiority complex, ndio maana Nyerere aliwaachia jina Zanzibar libaki nao. Waingereza wenyewe kwa sababu wako viziwani hata wanataka wajitoe EU.

Tanganyika anahitajika
 
Wana janvi, mimi ni Mtanganyika. Nimeshangazwa sana na mapendekezo ya tume ya Katiba kuhusu jina la Serikali mpya ya Tanganyika itakayoundwa. Wote mnafahamu kuwa imependekezwa iitwe Tanzania bara. Mimi siafikiani na pendekezo hili kwa sababu zifuatazo:

1. Kwa kuwa jina zanzibar bado litaendelea na kwa kuwa inafaamika wazi kuwa mshirika wa zanzibar katika muungano ni tanganyika, basi si busara kufuta jina la mshirika mmoja na kuliacha jina la mshirika mwingine. Kumbuka;
Tanzania = Tanganyika + Zanzibar, siyo Tanzania Bara + Zanzibar. Hivyo basi hakuna Tanzania bila uwepo wa Tanganyika. Iwapo ni lazima jina la Tanzania Bara liwepo basi ni sharti Zanzibar iitwe Tanzania Visiwani.

2. Kitendo cha kutotumia jina Tanganyika kitathibitisha madai ya muda mrefu ya Wanzanzibar kuwa Watanganyika ndio wenye uhitaji mkubwa katika muungano huu.

3. Tukiacha kutumia jina tanganyika itathibitika kuwa watanganyika tunalichukia jina la nchi yetu ya asili na hii ni ishara ya utumwa. Je muungano ukivunjika tutaendelea kujiita Tanzania Bara? Tutaonekana watu wa ajabu kweli.

Kwa maelezo hayo napendekeza serikali mpya iitwe Serikali ya Tanganyika na si Serikali ya Tanzania Bara.

Mwisho nawashauri watanganyika wenzangu kwamba kwa sasa tuelekeze mawazo yetu katika kushauri namna serikari yetu mpya itakavyokuwa badala ya kuelekeza mashambulizi kwa wanzanzibar wanaohitaji mamlaka kamili. Tukiendelea na hali hii itathibitika bila shaka kuwa watanganyika hatukujiandaa kuwa na serikali yetu. na kama hilo ni kweli, madai ya muda mrefu kuwa zanzibar ni koloni la tanganyika yataaminika. Naomba nikosolewe na kusahihishwa bila povu.
 
Kwa kuwa Rasimu iliyozinduliwa jana inazungumizia Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, tunahitaji kujua majukumu na mipaka ya Rais na mawaziri wa Tanganyika. Yote yanatakiwa yawepo ktk katiba mpya ya Tanganyika. Sasa najiuliza, je, rasimu hii ikipita kuwa katiba kamili 2014, ndo sisi watanganyika tutaanzisha upya mchakato upya wa katiba tena? Je, itawahi uchaguzi wa 2015?
Ni swali linalonichanganya.

Au ndo siri ya maombi ya miaka 2 zaidi ya kikwete imejificha hapa?


NB;
Nimetumia Tanganyika Vs Tanzania bara kwa kuwa mujibu wa Mapendekezo ya Tume nchi washrika zinaruhusiwa kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na nchi za nje. Kwa hiyo, kuwa na jina Tanzania na Tanzania Bara ktk medani za kimtaifa itawachanganya jumuia za kimataifa.
Nawasilisha

Aweda nimekuwa nikijiuliza haya yote bila kupata majibu sawia. Naona hapa kuna mtego wa aina fulani, ambao kiuhalisia inaashiria kuwa hakuwezi kuwa na uchaguzi 2015. Ili iwepo serikali ya muungano, lazima serikali 2 za nchi shiriki ziwemo. Kama katiba hii ikipita, itakuwa kinyume cha katiba kwa Serikali ya muungano kujishughulisha na mambo ya Tanganyika. Hivyo, inaonekana kama uchaguzi wa JMT utafanyikaka baada ya kupata pia katiba ya Tanganyika.

Kuhusu matumisi ya Tanzania bara dhidi ya Tanganyika, ni sawa na kujilisha upepo! Kama tutardhia kurejesha Tanganyika, hatuna budi kuirejesha na jina lake, vinginevyo ni njia ya kuiunika serikali ya Muungano kama ilivyo sasa. Kwa wengi imezoeleka, ukisema Tanzania maanayake ni Bara!!
 
Kwa ujumla wake Rasimu imetulia, nimeisoma nikagundua AIDHA imetatua kero nyingi zilizokuwa zinapigiwa kelele na watanzania mbalimbali AU imetoa mwongozo wa jinsi ya kuzitatua - big up to Warioba et al

Kidogo tu nimekwazika na issue mbili, tatu hivi;

i) kwenye sifa za mgombea ubunge jamani issue ya elimu ni muhimu sana, haya mambo ya kujua kusoma na kuandika tu hayatoshi jamani. Tung'ang'ane kiwango cha chini cha elimu kiwe angalau first degree jamani. Tumeshuhudia wabunge wengine ni mbumbumbu kabisa, ni kwamba tu ana vipesa na ni influential basi anapita!! hii hali itaendelea hadi lini?

ii) hili jina la Tanzania bara linanikwaza. Sina hoja nzito sana ila ni kwamba it doesn't sound good, ni bora tuite tu Tanganyika moja kwa moja

ii) rasimu inaipa majukumu na mamlaka mazito Tume ya Utumishi wa Umma wakati tume yenyewe ni very weak kwa sasa. Kuna haja ya kuboresha muundo wake kwanza - unless sijaliona hili ktk rasimu

Ila kwa ujumla ni mwendo mzuri, so far so good!! tuiboreshe tu kidogo kwa maslahi ya taifa letu, shida yetu tunaiangalia kwa jicho la kichama chama!!
 
Its a wastage of resources kuwa na serikali tatu.

If we are seriously into our Union, tuwe na serikali moja.

I see this as a diversion into the facts that need be addressed.

Mambo yote ambayo ni controversial na tyalionekana na wazee wetu hapo mwanzo, (Karume na Nyerere) yamo humu ndani).

I see a clear and crystal intwntion to diversify us from facts such as poverty and natural resources.

Tutaachwa tukijadili haya mambo watu wakifanya yao.

I suggest katika rasimu mpya neno Tanzania Bara be removed and replaced by Tanganyika, Hakuna kitu kama TANZANIA BARA bali kunaTanganyika.
Umenena sawa mkuu. Serikali mbili au moja, hii mambo ya serikali tatu ni wastage of resouces. Tutaishia kugharamikia utawala badala ya maandeleo. Nchi hizi kwa ukubwa ni tofauti sana. Kama ndogo sana haikubali kuwa kwenye mwavuli wa kubwa haitakua haki kwa nchi kubwa kugawana sawa uongozi wa taifa, vinginevyo tupeane mikono na kutakiana heri.
 
mkuu.... heshima kwako...
1. hujaangalia tume ya uchaguzi itatenga muda gani wa kampeni.
2. je. hao mabepali ndio watakua na influence kwenye vyama vya siasa tuu?
3. huja-angalia ni mfumo gani utatumika na vyama saisa kupata wagombe wa ubunge.
4. wengi walinza kampeni bila pesa, lakini kukubalika kwao kukawafanya wakawa supported na kujikuta wakichangiwa pesa za kampeni.
5. hata kama hao wenye pesa watoka kama wagombea binafsi..je hela ndio kila kitu kwenye kampeni?
5. also kumbuka kua hii ni-draft ya katiba. na sio katiba. soo anything can change.

so we have to respect maoni yako pia. HOPEFUL WATAKUSIKIA..ila kumbuka katiba bado.
 
Au ndo siri ya maombi ya miaka 2 zaidi ya kikwete imejificha hapa?
Haitawezekana JK aongezewe muda, atakuwa amevunja katiba. Sana sana autatafutwa utaratibu wa serikali ya mpito itakayounda katiba ya Tanganyika
 
Kwa kuwa Rasimu iliyozinduliwa jana inazungumizia Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania tu na siyo nchi washirika,
kwa kuwa Rasimu imependekeza serikali 3 ya Muungano, Zanzibar na Tanganyika, na
kwa kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina mifumo kamili ikiwepo ofisi, viongozi,sheria mbali mbali zinazoongoza nchi hiyo ikwepo mgawanyo madaraka miongoni mwao, na upande wa Tanganyika hamna kitu, na
Kwa kuwa serikali ya Tanganyika haina sheria yo yote na Tume ya Uchaguzi hasa ktk ngazi za wilaya na kata na mitaa nk,

Hivyo basi, Mimi najiuliza, je Rasimu hii ikipita na kuwa katiba, ndo sisi watanganyika, tutaanzisha upya mchakato wa kutafuta katiba mpya ya Tanganyika yetu kabla ya 2015?

Ikumbukwe kuwa, wazanzibar wana katiba yao tayari inayotoa mwongozo kuhusu uchaguzi na tume ya uchaguzi nk. Tanganyika haina mwongozo wowote. Na Tanganyika inahitaji aina viongozi wanaohitajika na kazi zao, idadi wa wabunge na kazi zao, Tume ya uchaguzi, kama Tunahitaji wakuu wa wilaya/mikoa au la. Tunahitaji mamlaka ya serikali za mitaa iweje nk.

Tunahitaji kujua majukumu na mipaka ya Rais na mawaziri wa Tanganyika. Yote yanatakiwa yawepo ktk katiba mpya ya Tanganyika. Sasa najiuliza, je, rasimu hii ikipita kuwa katiba kamili 2014, ndo sisi watanganyika tutaanzisha upya mchakato upya wa katiba tena? Je, itawahi uchaguzi wa 2015?
Ni swali linalonichanganya.

Au ndo siri ya maombi ya miaka 2 zaidi ya kikwete imejificha hapa?


NB;
Nimetumia Tanganyika Vs Tanzania bara kwa kuwa mujibu wa Mapendekezo ya Tume nchi washrika zinaruhusiwa kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na nchi za nje. Kwa hiyo, kuwa na jina Tanzania na Tanzania Bara ktk medani za kimtaifa itawachanganya jumuia za kimataifa.
Nawasilisha
...kaka..hakuna mjadala juu ya suala la katiba ya tanganyika!... we've been taken for granted for so long.... kufikia mahali hata "ndugu zetu ktk muungano kujiona ni werevu wa kupindukia"...ndani ya katiba ya tanganyika ninayoamini kutuongoza tunakotaka kwenda, lazima miongoni mwa mengineyo, mtanganyika ajulikane ni nani, na ale kiapo cha uzalendo kwa mama tanganyika, mahusiano yetu na ndugu zetu wa upande wa pili wa jamhuri ya muungano yawekewe sheria ambayo italinda haki zao kama wazanzibar ktk tanganyika lkn ikitambua kuwa raslimali zote za tanganyika ni za watanganyika na wasio watanganyika kisheria watazimiliki kwa ubia na watanganyika, nyumba za serikali ktk tanganyika ambazo maofisa wa serikali ya tanzania wasio watanganyika walizinunua zirudishwe kwa serikali ya tanganyika, kwa "utaratibu uiokuwa wakupoteza muda"...lkn pia, "bila kujali katiba ya muungano inasemaje"..zabuni zote za halmashauri na manispaa za tanganyika zitolewe kwa makundi ya vijana na kina mama tu!!!
 
Je umeridhika na madaraka ya rais kwenye teuzi? mi sijaona changes kubwa za kutuletea maendeleo kwa kweli, zaidi naona serikali tatu ni mzigo mkubwa.
 
Wakuu tupende tusipende sasa inaonekana jina lililopotea miaka karibu hamsini (50) Iliyopita sasa litarudi tena hivi karibuni.Wengi wetu tulipozaliwa hatukulikuta jina hili "Tanganyika" .Sisi tuliikuta "Tanzania" na jina la 'Tanganyika" tumelisoma tu kwenye vitabu vya historia na kusikia wazee wetu wakizungumza.Hata hivyo jina hili naamini liliundwa na wakoloni.

Kufuatia Rasimu mpia ya katiba ambayo naamini itapitishwa; tunatarajia kuwa na serikali ya "Tanganyika", serikali ya "Zanzibar" na Serikali ya Muungano ya Tanzania.Hili ni jambo ambalo halitaepukika tena.

Binafsi silipendi jina "Tanganyika" sina uhakika ni kwa nini ila nadhani ni kwa kuwa ni neno ambalo nimekuwa nikilisikia kwa nadra sana na zaidi nikisikia neno "Tanzania".Sitaona ufahari wowote mfano siku nikiwa nje ya nchi , nikaulizwa unatoka wapi nikasema natoka "Tanganyika".Nadhani kuwa watu wengi wa kutoka Tanzania bara nao wanajisikia hivi hivi.

Sasa mimi ningeshauri baada ya serikali tatu kuundwa; sisi watu wa iliyokuwa "TANGANYIKA" tujiite "JAMUHURI YA TANZANITE". Ni mawazo tu lakini!
 
pamoja kuangaza kila sehemu ya maisha yamgusayo mwananchi wa kawaida rasimu limesahau kutaja miaka ya msajiri wa vyama vya siasa kiutendaji...yasijirudie ya tendwa miaka nenda rudi yupo yeye tu..
Au kama kuna mtu amesoma iko kipengele na mimi sijakiona anijulishe...lakini nimepekua sijakiona....
Hongera jaji warioba.
 
Kutakuwa na mkanganyiko sana, kwani hata wabunge 50 wa kutoka Tanzania Bara ni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika majimbo ya mikoa 25, kwa hiyo wabunge wengi wa sasa hawataweza kugombania nafasi 25 za wanaume na 25 za wanawake, itabidi wasubiri ubunge katika serikali ya Tanganyika ambayo kwa wakati huo itakuwa haipo, na wao watakaa benchi muda wa kutosha tu!
 
Asalaam aleykhum ndugu zangu wana wa Tanganyika na Zanzibar. Pia amani ya bwana iwe pamoja nanyi ndugu zangu wana wa Tanganyika na Wazanzibari.

Kwanza napenda kutoa pongezi kwa ndugu zangu wana wa Zanzibari kwa kuitetea nchi yao na sasa wameipata na itatambulika katika katiba mpya kama nchi ya Zanzibar. Kweli wameonyesha uzalendo wa hali ya juu sana kwa kuhakikisha historia na hadhi ya nchi yao haipotei hata kidogo. Zanzibar itabaki kuwa Zanzibar hata ndani ya muungano. Hongereni sana wanaharakati wa Zanzibar. Kweli mmeonyesha ujasiri wa hali ya juu sana katika kuipigania Zanzibar yenu.

Pili nataka nichukue nafasi hii kuwapa pole ndugu zangu Watanganyika kwa kupoteza historia na hadhi ya nchi yao tukufu ya Tanganyika. Ni pigp kubwa sana na pia ni dhambi kubwa sana imefanywa na viongozi waliopewa dhamana na Watanganyika kuitetea nchi yao. Hatimaye katika katiba mpya, Tanganyika itakuwa imekufa na kuzikwa rasmi. Kwani itazaliwa nchi mpya kabisa itakayoitwa Tanzania bara. Kweli wanaharakati wa Tanganyika wameonyesha uzembe na uwoga wa hali ya juu sana kwa kukaa kimya na kuacha Tanganyika yao ikiangamia pasipo na mtetezi wa kuifanya iendelee kustawi na kushamiri kama Zanzibar.

Sasa niende katika hoja yangu kuu ambayo inataka kueleza na kuomba ufafanuzi wa ni kwa nini Tanganyika ife na izaliwe Tanzania bara waketi Zanzibar haijafa? Hapa kuna kitu nyuma ya pazia kwa viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuilinda na kuitetea Tanganyika yetu. Kosa kubwa sana tumelifanya na tutahukumiwa na vizazi vijavyo kwa kuruhusu nchi yao tukufu ya Tanganyika ife na kuzaliwa nchi nyingine ya Tanzania bara. Hivi watanganyika wamekuwa na mioyo gani ya kuachia nchi yao tukufu kufa na kuzaliwa nchi nyingine? Binafsi nawachukulia wanaharakati kama ndio wasaliti wakubwa kwa Tanganyika yetu. Nasikia uchungu sana nikiona Tanganyika inaangamia na kutoweka kabisa. Hii dhambi haitosahaulika vizazi na vizazi. Eti leo mtanganyika amekuwa zoba na mbumbu namna hii hadi kudanganywa kuwa nchi yake ya Tanganyika ipo haijafa bali ni jina tu ndio limebadilika na kuitwa Tanzania bara. Kama hoja ni jina tu, kwa nini basi pia na Zanzibar isiitwe Tanzania visiwani? Thubutu kabisa, kwa umakini na uzalendo alokuwa nao Mzanzibari kitu hiko kisingelithubutu kutokea kabisa. Zanzibari itabaki kuwa Zanzibari tu, na hili sio kwa hiyari au hisani ya watawala bali ni kwa ujasiri na uzalendo wa wana wa Zanzibar. Tanganyika itakufa na itazaliwa Tanzania bara sio kwa hiyari ya wana wa Tanganyika, bali ni kwa hujuma na usaliti wa mtanganyika mwenyewe.

Hitimisho langu ni kuwa, kama muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado upo na utaendelea kuwepo. Naomba basi pia Tanganyika itambuliwe kama Tanganyika katika hii katiba mpya. Ya nini izaliwe Tanzania bara wakati Tanganyika bado ipo na ina historia yake kama ilivyo Zanzibari?

Ni kweli tunaihitaji Tanganyika yetu. Tutaipigania mpaka ipatikane. Wazanzibari walikataa zamani kuitwa Tanzania Visiwani na sasa wa Bara tukakubali kupoteza jina letu. Ndiyo maana mwaka juzi 2011 Serikali ikawahadaa wananchi na ulimwengu kwa ujumla eti Tanzania ilifikisha miaka 50 ya uhuru!! Uwongo ulipitiliza mpaka. Hakuna nchi inayoitwa Tanzania Bara wala Tanzania iliyopata uhuru miaka 50 iliyopita. Ni TANGANYIKA iliyojitawala tarehe 9/12/1961 na siyo vingine. Kweli wa-Tanganyika tumezidi uzuzu. Asante kiroba kutupa ukweli.
 
hii ni rasimu ya muungano imependekeza bunge liwe na wabunge 75... 50 bara, 20 visiwani na 5 walemavu wateule wa rais. Majimbo 25 kwa bara na 20 kwa visiwani na kila jimbo litakuwa me na ke. Tusubr katiba ya bara itasemaje.

mkuu mbona haya unayoandika wewe hayapo kwenya hiyo taarifa? au macho yangu hayaoni vizuri? ngoja nikatafute miwani. ndio maana tulupendekeza serikali ya majimbo ili magavana ndo wawe wawakilishi kwenye muungano. serikali yake itakuwa ndogo sana yenye mawaziri wa mambo ya muungano tu. hii ingefuta wakuu wa mikoa na wilaya. aafu kuna mambo wanasema yatazungumziwa kwenye serikali husika mbona la mawaziri wameliweka? ina maana serikali ya muungano itakuwa na mawaziri 15? kushughulikia mambo yapi? hiii wangetuweke sisi watanganyika na hiyo ya muungano inakuwa na wizara saba tu zinatosha
 
uko sahii mkuu aweda swali lako mhimu sana kwa msikabali wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom