RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

naipongeza serikali ya kiwete, tutamkumbuka kiwete mzee wa katiba na uhuru
 
Sasa kama uongozi wa nchi itakuwa ni serikali 3, jmt, tanganyika, na zanzibar.. Je katiba ya tanganyika inatengenezwa na tanganyika yenyewe???
 
Mh Bilal anawapa pole wajumbe na kuwapongeza kwa kazi nzuri.Anasema kazi ilobaki ni ya wajumbe wa mabaraza ya katiba.
 
kazi kwelikweli,ila ni bora Tanganyika yetu irudi na walowezi wote waondoke! tehtehtehteh!!
 
Htimaye Tanganyika yetu tuliyoiuza muda mrefu sasa tumeipata,sasa ni wakati wa kuwekana sawa.

Sasa mkuu mbona hawajatoa muongozo wa kuundwa kwa serikali ya Tanzania bara? 2015 tutachaguaje viongozi wetu?
 
Mi nadhani hii tume ilazimishwe kutengeneza katiba za Tanzania bara na Zanzibar haraka sana, tena kwa gharama zao wenyewe. Haiwezekani watumie hela yote kufanya upuuzi kama huu!!!

hakuna haja ya kulazimisha tume.Hapa kila Nchi itengeneze katiba yake kwa matakwa yake yenyewe mbali na hii katiba ya shirikisho.Na unaposema tume watengeneze haraka katiba ya Tanzania bara na ile ya Zanzibar kwa haraka,hapa nafikiri umesahau kuwa wenzetu Wazanzibar tayari walikuwa na katiba yao hivyo kuiamlisha tume ni sawa na kuivunja katiba ya Zanzibar.
 
Kwa hiyo kama katiba hii ikikamilika 2014, uchaguzi wa 2015 utakuwa na katiba mpya kwenye eneo la serikali ya shirikisho peke yake. Uchaguzi wa Tanzania bara na wa Zanzibar utafuata katiba gani?!!!
hahahaha huku zanzibar tuna katiba yetu wewe ifufueni tanganyika au ndio mtaita tanzania bara
 
Bunge la Jamhuri litakuwa na wabunge 75,(50 kutoka tanzania bara ie wawili kwa kila mkoa na 20 kutoka zanzibar,na watano kutoka katika makundi maalum)
 
Huwezi kukuta Lumumba project akichangia mada kama hizi..............wao ni udaku na habari za watu tu!
 
Kwa ujumla wamefanya kazi nzuri sana, niwapongeze sana kwa uchambuzi makini pamoja na vikwazo walivyopambana navyo ila wamefanya kazi njema, mapungufu hayakosekani ndio maana itajadiliwa tena na bunge la katiba ili kuiweka sawa.
 
Kifo cha ccm kimewadia,sasa rais kushtakiwa na bunge,viti maalum hakuna, pamoja na mengi mazuri kali ni kuwa mbunge akifariki,mrithi atatoka chama alichokuwa aliyefariki,hapa kuna tatizo kwani ni sawa na kuamini wananchi walichagua chama na si mtu kwa sifa na uwezo wake,pia ni kuamin anayepewa nafasi anakubalika na pia ni kuwanyima haki za msingi watu wanaopenda na wenye nia ya kuleta maendeleo. My intake: Tusitishwe na gharama za uchaguzi kwa kumteua mtu asiyefaa.
 
Rasimu inapendekeza serikali tatu. Katiba ya Tanganyika wapi, na/au lini itatengenezwa?

Siku zote Watanzania ni watu wa kutengeneza deals, walipewa deal la rasmu ya katiba ya URT wao wamependekeza serkali 3 hali wakifahamu kabisa Bara hakuna katiba na hivo hiyo task ipo pending kama deal. wewe hizo posho na masurufu yote yale unategemea nini... ngoja nchi iliwe kabla hatujaanza kuvurugana na issue ya muundo wa Muungano
 
Sasa kama uongozi wa nchi itakuwa ni serikali 3, jmt, tanganyika, na zanzibar.. Je katiba ya tanganyika inatengenezwa na tanganyika yenyewe???
Ndio maana yake, unataka Tanganyika ipangiwe na znz, unataka znz ipangiwe na Tanganyika?
 
Mi ndio najiuliza sasa 2015 Tanzania bara tutajichaguliaje viongozi?

Hapa naona harufu ya Tanganyika kuendelea kudandia katiba ya muungano bila katiba yake yenyewe kama ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom