RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Serikali tatu safi maoni yangu huenda yakawaimplemented,
wabunge 20, 50, 5 walemavu sio mbaya. Kiukweli naona mambo yatakuwa safi sana.
Jaji Kisanga alitoa pendekezo hili enzi za mkapa, mheshimiwa akawa mkali,akihisi kama vile tume inawasemea wananchi.
Hatimaye wazo limetinga ndani ya rasmu.
 
Tutarajie upinzani baadhi ya maeneo, kama madaraka ya rais, natamani nisikie maoni ya lissu na chadema kiujumla!
 
Sijui... but nadhani hao 'wataalamu' walitakiwa waje na majibu...
Unaona sasa!! umeulizwa swali dogo la mtego umeshindwa kujibu, kama unajuwa Tume ilikuwa na wataalam na maprofesa na wanasheria unadhani wao hawana akili na walichoimplement?
 
Kuna hatari naiona hapa! Kama tukikubaliana na katiba hii maana yake itabidi bara tuanze mchakato wa katiba yetu! Hapo ndio naona kale kampango ka JK kuongezewa muda! Maana there is no way tutaingia uchaguzi bila katiba
Jk hawezi ongezewa muda kwakuwa yeye ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hapo ataongezewa muda kuwarais wa nchi gani?
 
Sijui... but nadhani hao 'wataalamu' walitakiwa waje na majibu...
Serikali ya Tanganyika itakuja baada ya kupata katiba ya muungano, inaweza kutokea kati ya haya mawili either Kikwete aongezewe muda au tupate serikali ya mpito itakayoongoza wakati wa kuandaa katiba ya Tanganyika.
 
Duuuh!Zile ndoto zangu za kugombea ubunge zimepotea hivi hivi yaani.Sipati picha wabunge wa Dar watakuwa akina nani aisee sijui Nape,sijui Mnyika,Sijui Mdee..Ubunge utakuwa ishu sana.Kazi ipo
 
bethlehemu warushe draft yote kwennye mtandao watu tuwe mbele kwenye kuchambua. Unaweza kukuta taarfia inachukua wiki nzima kabla ya kuweka kwenye mtandao.Watu wengi hivi sasa hawana access na tv kutokana na ukirittimba wa kisimbusi
mkuu usihofu, haitapita muda mrefu itawekwa na tutaijadli humu JF.
 
Kwenye Uraia wa nchi mbili wametudanganya eti itashughulikiwa na nchi husika. Kama Zanzibar na Bara tuna Uraia mmoja itakuwaje Zanzibar au Bara upande mmoja uwe na Uraia wa nchi mbili??
Hapa mi naona tumedanganywa
 
Atarithiwa na mkewe(Joke) Hii ni moja ya changamoto mkuu
Tayari tumeanza na contradiction.Lakini Jaji Warioba kasahau kwamba Demokrasia ina gharama zake na mojawapo ni hii ya uchaguzi.Kwa vile ni mwanzo wa mchakato nadhani Watanzania watakuwa makini kusahihisha makosa kama haya.
 
Je kama Mbunge alitoka upande wa Mgombea binafsi ambaye pia nimesikia Rasimu inapendekeza awepo mara baada ya kupitishwa kuwa Katiba ni nini kitafanyika?.

Hapo umeneno wana assume kama vile hakutakuwa na mgombea binafsi asiyekuwa na chama huyo nani atamrithi, au watatakiwa kuacha wasia wa nani atarithi kiti chake, hili jambo ni la ovyoo, demicrasia lazima iheshimiwe, watu wachague viongozi hii nchi democrasia ndo inakua hata kupiga tu kura watu bado hawajitokezi kuache kuweka vichocheo vya kukuza voter apathy nchini ni kosa kubwa! Akifa/akijihudhuru au kwa namna yoyote nafasi ya kuchaguliwa yoyote ikibaki wazi lazima uchaguzi ufanyike, hii ndo gharama ya democracy!
 
kuwepo na wabunge wa aina mbili
wakuchaguliwa na watateuliwa na rais na ni kundi moja tu la walemavu hakuna viti maalumuuuuuuuuuuuuuuu
kila jimbo litoe wabunge wawili, wa kiume na wa kike,
Hapo ni ujinga mtupu. Jimbo kuwa na wabunge wawili kwa maslahi ya nani na kuwakilisha nani? na raisi anakuwa na wabunge kuwakillisha nini?. inamaana tutakuwa na wbunge zaidi ya 700 na gharama za kufuga wadudu hao zitalipwa nani.Wanawake wanaweza na wamekwisha jiwezesha waingie kupambana.Lazima mihimili hii iwe tofauti.
 
Hivi nimesikia vibaya au ni kweli RAIS ANAWEZA KUONGOZA KWA MIAKA 15? I hope nimesika vibaya
 
jambo jingine ni kuhusu maadili, hili lilizungumzwa sana, maadili ndani ya jamii, ndani ya utawala na ndani ya nchi kwa ujumla

tume inapendeklkeza mambo 3
1. maadili ya viongozi yawe kwenye katiba
2.miiko ya viongozi yawe kwenye katiba
3.kiundwe chombo maalumu cha kusimamia maadili ya taifa
hivi ile tume ya maadili ya viongozi wa umma itakua tofauti na hiki chombo???naamin hiko chombo pia kitaangalia maadili hata juu ya rushwa,sasa TAKOKURU YA HOO-SEA ITAKUFA?MBONA NAONA HAPA TUNACHEZA WIMBO ULEULE
 
Hapo nafikiri labda hujapaelewa vizuri, mimi nafikiri wana hoja ya maana kwamba, kama Mbunge akifariki basi hakuna haja ya Uchaguzi ili kuokoa gharama, basi mrithi wake atatoka Chama kile kile tu, hivyo ina maana Chama chake watateua tu, badala ya uchaguzi kufanyika, kwa maana nyingine tunapaswa tuchague Sera za Chama na SIO mtu!

This is too low!! Hii ni sawa na kumpeleka mwanao kwenye shule nzuri kwa majengo na vifaa vya kufundishia lakini haina walimu!! Sera nzuri bila wasimamizi wazuri?
 
Mkuu mimi nishaona 2015 hakuna dalili ya uchaguzi...

Hii dalili ni kubwa ya either kutokuwepo uchaguzi 2015 au kufanya uchaguzi kwa kutumia katiba
tuliyonayo sasa,watanzania akili mu kichwa'
 
Back
Top Bottom