Nanukuu:
MADARAKA YA RAIS
Ndugu Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba, Rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu. Hata hivyo inapendekezwa Rais ashirikiane na taasisi na vyombo vingine katika uteuzi. Kwa mfano:
Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais atateua na Bunge litathibitisha.
Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu Rais atawateua kutokana na majina ya watu waliopendekezwa na Tume ya Uutumishi wa Mahakama na baada ya hapo Bunge litathibitisha.
Kuhusu Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama inapendekezwa kianzishwe chombo kipya kitakachoitwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo kati ya majukumu yake itakuwa ni kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kuhusu Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu watateuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma.
KINGA YA RAIS
Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.
(Tume hapa inamaanisha rais ni Mungu asiyekosea,asiye na ndugu,asiyesoma mikataba kwa makosa,asiye mfanya biashara,ambaye hajatumia pesa zake na za washirika wake kuingia madarakani,
Kama sio,kwani awekewe kinga,hapa sio kuuza nchi na rasilimali zetu kwa kutumia kipengele hicho kinachomfanya mfalme na muungu mtakatifu?)
IDADI YA MAWAZIRI
Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na tano na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.
(Hapa sielewi kabisa,hata cha kuandika sina)
BUNGE
Ndugu Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu wenye Ulemavu.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.
Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.
(Je,inamaanisha wananchi tutakuwa tunachagua mtu au chama,kwanini ijichanganye na kutenda tofauti kwa mgombea huru,iwapo tunachagua mtu,kwanini chama kipewe nafasi ya kutupatia mtu ambaye sisi wananchi hatujamchagua,na kwakuwa kuna kipengele kinatoa nafasi wananchi wamtimue mbunge akichemka,je huu mwanya uliopo hapa hautatumiwa kumfukuza mbunge aliyechaguliwa na chama iwapo jimbo litakuwa wazi kwa sababu tajwa hapo juu?)
Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa kipindi chake.
Inapendekezwa pia kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi inayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha Siasa basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.
Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi wa vyama vya Siasa.
"Nachanganyikiwa kila ninaporudia kuisoma rasimu hii ya katiba ya Tanzania yetu"
mawazo yangu tu
~seen today~