Wakuu wote salamu kwenu!
Nimefuatilia na kusoma rasimu ya katiba iliyotolewa leo. Rasimu ile ina mambo mazuri na mengine ambayo hayajakidhi nyoyo zetu. Mojawapo ni ukomo wa Madaraka ya Rais, Teuzi zake nk. Nilichogundua/kiona mimi hii rasimu ni kwa serikali ya Muungano, maana yake sisi kama Watanganyika/Wazanzibar tuna kazi nyingine tena ya kuunda katiba zetu kwa nchi zetu husika.
Katika hili,maana yake Bunge la Tanganyika laweza kuwa na Wabunge tuseme 500, au 10 au 100 kutokana na matakwa ya Watanganyika (wale wabunge 75 na mawaziri 15 ni wa Muungano) Nafikiri watu wengi humu jukwaani hawajaliona hilo. Sasa kinachofuata ni kuweka katiba makini kabisa kwa serikali yetu ya Tanganyika.once hii ya muungano ikipita basi kiu yetu yote ya maendeleo tuihamishie kwenye katiba yetu ya muungano.
Tutengeneze katiba itakayotufaa kwa miaka 50 kama sio 100 mbeleni. Na hapo ndipo issue za mikataba ya nchi lazima ijadiliwe bungeni na mambo mengine yote tunayotamani tutakapopata pa kuayasemea.