Rasimu ya katiba ya Warioba, ibara ya 54 inapendekeza raia kuwa na mamlaka ya kudai haki zilizoporwa. Hivi sasa ni uonevu mkubwa

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Rasimu ya katiba ya Jaji Warioba katiba ibara ya 54 imependekeza kuwa mahakama au chombo cha maamuzi kufanya maamuzi kwa kuzingatia haki na usawa na uhuru wa mtu binafsi

Sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu zizingatiwe.

Haki na maslahi ya jamii yazingatiwe.

Kila mtu awe na haki ya kufungua kesi kudai haki yake au ya mtu mwingine

Ndugu au mtu binafsi awe na nguvu kufungua kesi kudai haki za jamaa zake zinapovunjwa.

Pamoja na mahakama ya rufani kutilia mkazo juu ya kuruhusu kuwepo na upatikanaji wa haki za binadamu lakini bado hali sio nzuri. Mkazo uliwekwa kwenye kesi ya W.K. Butambala v Ag (Mwalusanya J) Lakini serikali haitoi wigo mpana kudai haki za binadamu.

Sasa hivi hapa Tanzania kuna matukio mengi ya vyombo vya dola kukingia vifua watu wanaovunja sheria na kuua watu wasio na hatia. Hii ibara ikiwekwa kwenye katiba mpya hapa Tanzania watu watakuwa na nafasi ya kudai haki za ndugu zao wanaopotezwa bila hatia.
 
Hiyo rasimu inasema unadai kwa njia gani?
Je umejaribu kuzitumia kudai hiyo haki ukazuiliwa?
 
Ata yasasa inasema hivo japo inatoa masharti kadhaa eidha kulingana na mazingira au hali ya uchumi
 
Majizi ya kura hayawezi kukubali katiba mpya maana wao ni zao la shetani.
 
Mi CCM ikisikia tu chochote kuhusu hii Katiba ya Wananchi nguvu zinawaisha kabisa. Inajua ingepitishwa tu na kuwa Katiba, muda huu ingekuwa imeshang'oka madarakani.
 
Majizi ya kura hayawezi kukubali katiba mpya maana wao ni zao la shetani.
Mkuu tukianza kupata haki zetu baada ya ndugu zetu kuuwawa na wahuni mambo mengine yatafata. Hata wizi wa kura utazibitiwa kama utakuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…