Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Rasimu ya katiba ya Jaji Warioba katiba ibara ya 54 imependekeza kuwa mahakama au chombo cha maamuzi kufanya maamuzi kwa kuzingatia haki na usawa na uhuru wa mtu binafsi
Sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu zizingatiwe.
Haki na maslahi ya jamii yazingatiwe.
Kila mtu awe na haki ya kufungua kesi kudai haki yake au ya mtu mwingine
Ndugu au mtu binafsi awe na nguvu kufungua kesi kudai haki za jamaa zake zinapovunjwa.
Pamoja na mahakama ya rufani kutilia mkazo juu ya kuruhusu kuwepo na upatikanaji wa haki za binadamu lakini bado hali sio nzuri. Mkazo uliwekwa kwenye kesi ya W.K. Butambala v Ag (Mwalusanya J) Lakini serikali haitoi wigo mpana kudai haki za binadamu.
Sasa hivi hapa Tanzania kuna matukio mengi ya vyombo vya dola kukingia vifua watu wanaovunja sheria na kuua watu wasio na hatia. Hii ibara ikiwekwa kwenye katiba mpya hapa Tanzania watu watakuwa na nafasi ya kudai haki za ndugu zao wanaopotezwa bila hatia.