Rasimu ya Mitaala Nchini: Umri wa kuanza darasa la kwanza ni miaka 6, elimu ya msingi mwisho darasa la 6
MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.

Maoni yangu:

1. Kutolewe mafunzo kwa watekelezaji wa mtaala huu kwa mfano walimu, workshop instructors nk. Hii itasaidia kuendana na mabadiliko haya hasa hasa kwa walimu waliokwepo kabla ya mabadiliko.

2. Kuongeza wafanyakazi kuendana na mahitaji ya utekelezaji wa mtaala kwa mfano walimu wa kozi na masomo mapya

3. Serikali ijipange kwa upande wa bajeti kugharamia miundombinu, mishahara, vitabu, mitambo nk.

4. Career guidance iwepo kwa wanafunzi watakaochukua mkondo wa amali ili wajue ni fani zipi zinaendana na vipaji vyao, malengo yao, uwezo wao na uhitaji katika soko la ajira.

5. Wananchi waelekezwe zaidi kuhusu mabadiliko ya mtaala na fursa zilizopo pale utekelezaji wa mtaala ukianza.

Mwisho:

Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya ya kuboresha mfumo wetu wa elimu, ambao unaenda sambamba na mabadiliko yaliyopo katika dunia ya sasa kwa kuzalisha watanzania ambao watakuwa wana utaalamu, wanajiamini, wana mtazamo chanya na wana fikra tunduizi.

Wadau tuendelee kutoa maoni yetu ili rasimu hizi ziboreshwe na ifike hatua ambayo serikali watafanya maamuzi katika utekelezaji wa sera na mtaala mpya.

Matokeo ya utekelezaji wa mtaala huu mpya na sera ya Elimu ya mwaka 2023 italeta tija na nchi yetu itaendelea kwa kasi kubwa
Mdau wa Elimu.

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri elimu ya uzazi au tuseme reproduction ianze kufundishwa kuanzia kidato cha kwanza maana ndipo watoto wengi chuchu zinaanza kutoka na vijana wanaanza kuota ndevu na ndevu za kule mahali zinaanza kuota kwa mabinti na vijana wa kiume.
 
Nashukuru baadhi ya mapendekezo ambayo tuliyapigia kelele humu jukwaani, yamepitishwa.

NB:- kwenye hiyo namba 4, naamini ubaguzi wa lugha kwenye kufundishia utafanyiwa kazi kati wanafunzi wa shule za kawaida na wale wa michepuo ya kiingereza (English medium).

Yaani iwe hivi; wanafunzi wanaonza na lugha ya Kiswahili, wamalizie na lugha hiyo hiyo. Na wale wa English medium nao wafanye mitihani yao kwa lugha ya Kiingereza.

Yasitokee tena haya mauza uza ya sasa ya mtoto kusoma kwa lugha ya Kiswahili kutoka darasa la 1-7! Halafu Sekondari anaenda kufundishwa kwa kugha ya Kiingereza.

Nimefarikia pia kuona wanafunzi watafundishwa Historia ya Tanzania pekee! Maana ilikuwa inashangaza kuwakaririsha watoto masuala ya Mfecane war, Vita ya Kwanza na Pili ya Dunia, nk huku vitu vyote bikiwa ni useless katika maisha yake ya kila siku.

Naamini hata katika hiyo Historia Mpya ya Tanzania, wanafunzi watafundishwa vitu vyenye manufaa tu kwenye maisha yao.

Sitapenda kuona wataalamu wetu wakiweka Historia ya kuwasifia Wakoloni, huku Mababu zetu wakidharauliwa. Ikiwezekana viwekwe vile vipengele ambavyo ni chanya tu.
 
MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.

Maoni yangu:

1. Kutolewe mafunzo kwa watekelezaji wa mtaala huu kwa mfano walimu, workshop instructors nk. Hii itasaidia kuendana na mabadiliko haya hasa hasa kwa walimu waliokwepo kabla ya mabadiliko.

2. Kuongeza wafanyakazi kuendana na mahitaji ya utekelezaji wa mtaala kwa mfano walimu wa kozi na masomo mapya

3. Serikali ijipange kwa upande wa bajeti kugharamia miundombinu, mishahara, vitabu, mitambo nk.

4. Career guidance iwepo kwa wanafunzi watakaochukua mkondo wa amali ili wajue ni fani zipi zinaendana na vipaji vyao, malengo yao, uwezo wao na uhitaji katika soko la ajira.

5. Wananchi waelekezwe zaidi kuhusu mabadiliko ya mtaala na fursa zilizopo pale utekelezaji wa mtaala ukianza.

Mwisho:

Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya ya kuboresha mfumo wetu wa elimu, ambao unaenda sambamba na mabadiliko yaliyopo katika dunia ya sasa kwa kuzalisha watanzania ambao watakuwa wana utaalamu, wanajiamini, wana mtazamo chanya na wana fikra tunduizi.

Wadau tuendelee kutoa maoni yetu ili rasimu hizi ziboreshwe na ifike hatua ambayo serikali watafanya maamuzi katika utekelezaji wa sera na mtaala mpya.

Matokeo ya utekelezaji wa mtaala huu mpya na sera ya Elimu ya mwaka 2023 italeta tija na nchi yetu itaendelea kwa kasi kubwa
Mdau wa Elimu.

USSR

Sent using
 
Naona bado kutakuwa nanmzunguko mjubwa...haswa ukizingatiwa masoko yataendela kuwa mengi...nadhani ungekuwa vyema masomo yakapunguzwa yasizdi matano kwa kila darasa/mchepuo...

O level history liko mara mbili, kwa nini singeungwanishwa ikawa somo moja, Sawa na kwenye somo la biashara na usimamizi...

Mwisho nadhani vitendo vikiwa vingi kuliko nadharia itasaidia Sana kwa wanafunzi
 
Mengi ni mazuri hapo kwenye bodi ya walimu ndo shifa itakapoanza Anza,Mpk sijuii Mtu awe na leseni
Nadhani hyo wangeiondoa
 
Mambo mengi yako vizuri ila tatizo liko kwenye lugha, tungeamua tu kufanya kiingereza kuwa lugha ya kufundishia ili kuendana na soko la ajira. Kiswahili kibaki tu kama somo na huku mtaani tuendelee kuupepeta kwa kiswahili.
 
1. mtihani wa darasa la saba utafutwa. mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (standard six national assessment).

3. mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, kiingereza kitakuwa kama somo kwa shule za kiswahili medium na lugha ya kufundishia english, kiswahili kitakuwa kama somo kwa shule za english medium.

5. elimu ya msingi itakuwa miaka 6. mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. masomo ya elimu ya msingi yatakuwa kkk, jiografia, kiswahili, sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). mwanafunzi atachagua kutokana na

uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:

-kilimo na ufugaji

-umakenika

-biashara na ujasiriamali

-sanaa bunifu

-elimu ya michezo

-ufugaji wa nyuki

-uchimbaji wa madini

-urembo

13. mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:

-hisabati

-elimu ya biashara

-kiingereza

-historia ya tanzania na maadili

15. wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:

-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (necta)

-cheti cha amali (nactvet)

16. kila shule itakuwa na wakala wa veta ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika a-level na ualimu.

19. coding itafundishwa shule ya msingi.

20. information and computer studies (ics) itabadilishwa na kuitwa computer science. somo limesukwa upya.

21. civics itaunganishwa na historia ya tanzania na maadili kwa o-level.

22. o-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya sasa.

23. katika o-level masomo ya biology na geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. maudhui yake yameingia katika somo la historia ya tanzania na maadili.

25. general studies (gs) katika a-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. michepuo katika elimu ya o-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). michepuko iliyoongezeka ni:

-sanaa

-lugha

-muziki

-michezo

-tehama

28 masomo ya o-level yatakuwa:

-biology

-physics

-chemistry

-history

-geography

-historia ya tanzania na maadili

-hisabati

-kiswahili

-english

-elimu ya biashara

-utunzaji wa taarifa za fedha

-computer science

-bible knowledge

-elimu ya dini ya kiislamu

29. astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. watakaosoma stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. walimu wa sekondari wote watakuwa na shahada (degree). kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. vyuo vilivyokuwa vinatoa stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada

(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe

na umahiri zaidi. kisha walimu watapata leseni.

35. mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.

maoni yangu:

1. kutolewe mafunzo kwa watekelezaji wa mtaala huu kwa mfano walimu, workshop instructors nk. hii itasaidia kuendana na mabadiliko haya hasa hasa kwa walimu waliokwepo kabla ya mabadiliko.

2. kuongeza wafanyakazi kuendana na mahitaji ya utekelezaji wa mtaala kwa mfano walimu wa kozi na masomo mapya

3. serikali ijipange kwa upande wa bajeti kugharamia miundombinu, mishahara, vitabu, mitambo nk.

4.career guidance iwepo kwa wanafunzi watakaochukua mkondo wa amali ili wajue ni fani zipi zinaendana na vipaji vyao, malengo yao, uwezo wao na uhitaji katika soko la ajira.

5. wananchi waelekezwe zaidi kuhusu mabadiliko ya mtaala na fursa zilizopo pale utekelezaji wa mtaala ukianza.

wadau tuendelee kutoa maoni yetu ili rasimu hizi ziboreshwe na ifike hatua ambayo serikali watafanya maamuzi katika utekelezaji wa sera na mtaala mpya.

matokeo ya utekelezaji wa mtaala huu mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 italeta tija na nchi yetu itaendelea kwa kasi kubwa.
 
Tatizo wameandaa maneno bila kuandaa vitendo ndo mwanzo wa kufeli kutakapoanzia, majibu wanayotoa walioandaa hiyo rasimu nayo yanaonyesha hawajajiandaa kutekeleza mpango kiufasaha bali maneno, elimu iliyopo imeshaonyesha kufeli sana kutoa wahitimu wenye fani na tupo nyuma sana na shida siyo walimu bali mfumo wa elimu uliopitwa na wakati Sasa Nini kinashindikana kuhamishia bajeti yote kwenye kubadili mitaala haraka sana na mabadiliko yaanze mara Moja ili watoto na vijana walio kwenye elimu watoke na elimu Bora.

Kingine kilichoharibu elimu ni private sekita kufanya biashara kwenye elimu na muda wa watoto na hicho ndo kilitakiwa kuondolewa haraka ili elimu ichukue sehemu yake, kama kutengeneza muda wa watoto kukaa shule na siku za kuwa shule ili watoto wasigeuke vichaa wa elimu na kuchoshwa afya ya akili na mwili bila mapumuziko, zamani shule zilitumia muda kidogo na muda mwingine watoto walienda likizo na kukaa na jamii zao lakini walifaulu na uelewa wao ulikuwa vizuri maana kusoma tu peke yake mwaka mzima au masaa 24 hakuleti akili bali elimu na mapumuziko, pamoja na maisha halisi ya jamii kunaleta akili Bora, Sasa imagine mtoto wa darasa la nne akaishi boarding eti afaulu mtihani wa nadhalia Sasa huyo mtoto akitoka huko boarding kurudi nyumbani anachukia maisha ya kuwa chini ya wazazi tayari na kusoma kote bila kupumzika anakuwa garasha la maadili, hivi ndo vitu vilitakiwa kuondolewa kwenye maisha ya watoto ili elimu ichukue mkondo wake, hayo mambo ya kugeuza watoto vitega uchumi wa watu kujifaidisha huku watoto wakipoteza maadili Yao na elimu ya umri wao kuwa kama majukumu ya watu wazima na wakati hata hao watu wazima wanajipumzisha kwa ruhusa na likizo na ikitokea kazi zinakuwa nyingi basi wanaomba kufanya kazi kwa shift ili wapate muda wa kupumzisha akili Sasa hawa watoto kwanini wasilindwe kwenye muda wa kukaa shule na mapumuziko Yao ila tunawaza tu kutengeneza mitaala mipya.

Kingine walimu waliosomea ualimu ni tofauti ni watu waliosomea fani Sasa unaposema watu waliosomea fani zingine ndo wakawe walimu hapo napo tutaharibu elimu kwa kiwango kikubwa maana fani zingine zote zinaajili kwa kusomea na kuwa compitet Sasa ualimu kwanini ugeuzwe wa miezi sita wakati walimu wapo mitaani wamejaa na fani Yao, mimi naona hii mipango ya elimu haipo kuondoa mfumo wa kizamani na kuleta elimu kutoka kwa walimu waliobobea kwenye fani Yao, Sasa Nini kinashindikana kuwapa muda walimu waongeze level za elimu zao na kama ni hao walimu wa karakana au veta wapo wengi sana, Sasa kwanini tuchukue watu wenye fani kuwa walimu wakati wao wamesomea fani na siyo kusomea ualimu au wafundishaji.

Kwa hayo tu mapungufu tayari waandaaji wa huu mpango inaonyesha hawapo kwaajili ya kubadili na kuleta elimu yenye tija kwa vitendo ila ni kama kumfurahisha Raisi kwamba wameleta mabadiliko kwenye uongozi wake ila yakiwa yapo kwenye udhaifu sana.
 
Kingine kila mkoa kuwa na ufundi au elimu yake napo ni hoja dhaifu sana itakayokwamisha elimu Bora, wao watoe kombi zote zipatikane kila mkoa maana Kuna watoto kuhama mikoa kwa ajili ya kuongozana na wazazi wao wanapohama kikazi Sasa comb zikiwekwa kwa mikoa Nini tutakuwa tunataka kufanya kwenye elimu ya watoto kama siyo kuleta maadili ya ajabu ya watoto kujilea wenyewe kwa kushindwa kuhama na wazazi wao kisa sehemu atakayo kwenda elimu yake haipo, kwakweli hao wanaotengeneza watengeneze vitu halisi katika jamii yetu na siyo kuleta maneno au matendo yasiyoleta Radha nzuri ya maarifa.
 
Kuchagua somo moja la fani ni kupuyanga,mtoto mwenye uwezo achague masomo ya fani hata mawili hadi matatu
Hofu yangu kuu ni miundombinu,isije kuwa ya elimu bure kuanza mwakani kwa watoto kutokuwa na vifaa wala madarasa ya kutekeleza huo ufundi na mwakani hao walimu watakuwa trained lini??
 
Kiswahili kitumike hadi chuo kikuu. Kiingereza kifundishwe kama lugha.
Wakija wawejezaji, au watia misaada na mikataba ya kimataifa wao pia wataongea kiswahiliiii
Lugha ndo maendeleo ndo maaba unaona rasimu imeweka kichina kiarabu kufaransa ili tujue lughaaaa
Kiswahili tyr ni lugha mama acha kiingereza kama lygha ya dunia kitumike kufundishia maana dunia ya leo angalabu kiingereza ndo lugha ya kimataifa kwenye mawasiliano
 
Back
Top Bottom