Rasmi Ibrahim Ajib Migomba atia saini kuitumikia yanga miaka 2

Rasmi Ibrahim Ajib Migomba atia saini kuitumikia yanga miaka 2

Huyo tayari mkuu na jezi yake ni no8 ndiyo kaandaliwa!
Mkuu kama hizi habari ni za Ndani siku zikiwa hazarani ntafarijika sana......

Huwa nafurahishwa sana pale tupo sajili kijana mdogo mwenye kipaji.....!
 
tangu nilvyoona rundo la wachezaji wa bongo ligi walivyokazana kucheza akiwemo ajib
nimwadharau sana...
 
upload_2017-7-5_17-14-18.jpeg


Dar es Salaam. Baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu, straika Ibrahim Ajib amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu.

Ajibu amesaini mkataba huo leo mbele ya mabosi wa Yanga na kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Nyota huyo anakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Yanga katika usajili wa sasa huku klabu hiyo ikiwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi
Ibrahim Ajib asaini rasmi klabu ya Yanga
 
wp_ss_20170705_0003.png

FB_20170705_15_27_52_Saved_Picture.jpg

Dahhhh.Yani hapa Yanga inaonesha kama ni team ya ndondo cup.
Kiukweli mpira wetu una safari ndefu.
Hivi walishindwa ata kupata tangazo moja la kubandika ukutani jamani?
Au viongozi wetu ni wapiga deal?
Mbona Singida utd wamependezesha kama zile team za kwa malkia vile?
 
Namuonea ajib huruma, ana ndoto fupi kiasi hiki! Anaenda sideways badala ya forwards!
Mbona hujamwonea huruma Niyonzima? Mpira ni maslahi kaka! Kama kayapata Yanga mwache aende tu!
 
Mkuu kama hizi habari ni za Ndani siku zikiwa hazarani ntafarijika sana......

Huwa nafurahishwa sana pale tupo sajili kijana mdogo mwenye kipaji.....!
Mkuu kama ni yule dogo wa Mbeya city nakuhakikishia maongezi yameshakamilika na akitoka Sauz tu anakuja kumwaga wino believe me.
 
Simba ni feeder club. Wamelea kipaji sasa lazima aende timu kubwa
 
Una muda gani hujawahi kuona watu wakisaini mikataba binafsi? saini za kukoroga zinaweza kufojiwa kirahisi sana ila finger print ni komesha kazi
Umenikumbusha mbali sana,kuna mtu alishawahi kukiri sahihi ni ya kwake kwenye mkataba fulani lkn alikataa kamwe hajawahi kusaini hcho kitu na wala haujui kabisa
 
Kama kawaida wakimataifa ofisi ya Katibu ina kiti kimoja anakaa anayesaini wengine wote wanasimama
 
ibrahim ajib ni mchezaji mzuri tu alikuwa simba muda mrefu na msaada wake pale simba ni kawaida sana tu hana tofauti na akina said ndemla na wala hana effect kwa simba!kila la kheri huko yanga na pia mkude aje tu kucheza yanga ni tawi lenu pia.
 
Yaani hadi leo saini huwekwa kwa dole gumba? Hebu wahusika jirekebisheni jamani, mnadhalilisha watu
Sikutegemea kabisa ndugu wakili msomi mselewa huulizie au upigwe na bumbuwazi juu ya kutumia dole gumba katika muktadha wa masuala ya mikataba
 
Back
Top Bottom