Rasmi nawaondoa simba kwenye mbio za ubingwa 2021-2022

Mr. Sound

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
2,227
Reaction score
4,773
wakuu salaam,

Chama na Miqueson walichangia magoli 40+ ambayo ni zaidi ya nusu ya magoal yote tulopata msimu uliopita, leo hawapo na sajili tulizofanya hazioneshi dalili ya kutengeneza walau nusu ya magoal hayo.

kinachonisikitisha ni kuona vile Chama aliondoka kizembe ajili ya upumbavu wa Mo, wanasimba tujiandae kisaikolojia kupitia wakati mgumu maana furaha tuloizoea mo kaiharibu kwa ujeuri wa pesa.

Mpaka hapa msimu huu nawaona yanga na azamu wakichuana vikali kulitwaa taji la ligi huku sisi tukianza kujenga upya team.
 
Naiona Simba inakwenda kuwa kama Africa Lyon. Nimeanza kuingiwa na shaka na huyu mwekezaji. Tabia yake ya kuingilia uhuru wa wachezaji, ubahili, kutokujua jinsi ya kuimarisha brand ya Simba kiasi cha kununua mabasi ya kishamba matatu!

Nilikuwa nafuatilia mwalimu alimtaka Aucho,ila ubahili ukafanya Yanga wamnunue.Pamoja na kuamimishwa kuwa huyu mwekezaji ana hela,bado alikuwa hawezi kushindana na Yanga wakitaka mchezaji.

Nini kiliwazuia wasisaini mkataba mnono na Azam waliosaini Yanga?Kama tulikataa bilioni 48 za Azam,tunawezaje kujisifia kwa kusaini 800M kwa miaka minne?Kama ni ushindani wa biashara, basi weka wewe hiyo pesa timu inunue wachezaji wazuri
 
Ligi ikishaaanza rasmi msije anza kulia lia mkamio fc maana kebehi zenu ni mechi moja tu ya kumfunga simba afu ndanda anakubutua CAF umefungashiwa virago huliwazii hilo..? Haki Luc Emely alikua sahihi
 
simba haiwezi kua kama africa lion ila tabia ya kuingilia uhuru wa watu wa jeuri ya pesa hauna afya kwa team yetu, bila upuuzi ule tungeendelea kumshuhudia chama msimu huu.
 
Ligi ikishaaanza rasmi msije anza kulia lia mkamio fc maana kebehi zenu ni mechi moja tu ya kumfunga simba afu ndanda anakubutua CAF umefungashiwa virago huliwazii hilo..? Haki Luc Emely alikua sahihi
hujui mpira, unadhani kuipenda team ni kuitetea tu hata ikifanya vibaya? kuna wakati ukosoaji unahitajika zaidi ajili ya kuijenga na kuiimarisha team.
 
Naiona Simba inakwenda kuwa kama Africa Lyon.Nimeanza kuingiwa na shaka na huyu mwekezaji.Tabia yake ya kuingilia uhuru wa wachezaji,ubahili,kutokujua jinsi ya kuimarisha brand ya Simba kiasi cha kununua mabasi ya kishamba matatu...
Wewe ndio kolo uiiebaki mwenye akili..
 
wakuu salaam,

chama na miqueson walichangia magoli 40+ ambayo ni zaidi ya nusu ya magoal yote tulopata msimu uliopita, leo hawapo na sajili tulizofanya hazioneshi dalili ya kutengeneza walau nusu ya magoal hayo...
Huna akili chama ameondoka kizembe vipi

Yanga karibia kila msimi zaidi ya nusu ya wachezji wanaondoka na bado huwa wanatufunga, kwahiyo sisis simba wachezaji wawili kuondoka ndio tunaanza kujenga team
 
hujui mpira, unadhani kuipenda team ni kuitetea tu hata ikifanya vibaya? kuna wakati ukosoaji unahitajika zaidi ajili ya kuijenga na kuiimarisha team.
Sawa kama mpira ni mechi moja pole sana. Kila.mwaka si mnajitapa afu mwisho wa siku hola. Tujifunze kuweka akiba ya maneno maana ukweli unajulikana mwishoni tena wazi wazi.bila kificho.
 
Kila mtu eti amekua mchambuzi wa soka.
Msimu uliokwisha kwenye mapinduzi cup Zanzibar Yanga walibeba ubingwa Chama na Merquison wakiwemo.

Kwenye mechi ya ligi pia msimu uliokwisha Yanga mbovu kuliko zote walipata goli dakika za mwanzo kama mechi ya jana kika ng'ang'ania mpaka mwisho,Chama na Merquisone wakiwemo.

Mechi za Darby sio mechi za kawaida bali ni vita vikuu vya soka.
 
Huna akili chama ameondoka kizembe vipi

Yanga karibia kila msimi zaidi ya nusu ya wachezji wanaondoka na bado huwa wanatufunga, kwahiyo sisis simba wachezaji wawili kuondoka ndio tunaanza kujenga team
hukumsikia magoli akizungumzia suala la chama au ndo umecomment tujue unajua kuandika?
 
Sawa kama mpira ni mechi moja pole sana. Kila.mwaka si mnajitapa afu mwisho wa siku hola. Tujifunze kuweka akiba ya maneno maana ukweli unajulikana mwishoni tena wazi wazi.bila kificho.
mpira sio mechi 1 bt sajili zile sidhani kama watatupa hata nusu ya magoal ya chama na luis, ujue misimu yote yanga walohangaika kuchukua ubingwa ni ajili ya uhaba wa magoal na hili ndo tatizo linalotukabili kwa sasa, tunacheza vizuri sana bt mipango ya magoal ndo haieleweki.
 
Tatizo la yanga la kutokupata magoli limehamia Simba rasmi
Jeuri ya moo kumuondoa Chama itawatokea puani Wana msimbazi msimu huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…