Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Kwa wanaobet sh 2000 au 500 hawawezi kukuelewa tuliobet mpk milioni na zaidi tunaelewa.

Betting ilinifilisi nikapoteza gari 2 na pesa kibao nakadria nimepoteza takriban mil 30 kwenye betting. Mungu mwema nime quit nimekubali hasara sitarudi tena, nimeanza upya maisha yangu nje ya betting.

Kwa ufupi huwezi tajirika kwa
kamali, utaishia kuwa masikini wa kutupwa. Utapata leo mil 2 kesho utavuta kuiweka kwa odd 2 upate mil 4 unaliwa unapoteza unapambana kuokoa ulicholiwa ndio unapoteza zaidi. Ukija kupata tena basi umeoata sehemu tu ya ulichopoteza .

Kama hujawahi kubet nakusihi usijaribu kabisa huo ni ukoma
Seriously mkuu lakini emu nambie ukweli, umeweza kuacha kabisa????

historia yako inafanana na mimi japo sikuwai acha gari mbili, lakini kimtonyo nilikuwa nastake high sasa kuna muda naliwa kuna muda nakula, faida kubwa nakumbka niliwai pata milioni 5 tu.

huwa kuna jini la kubet unakuta kuna siku unarudi rudi.
 
Kwanza niseme tu mimi ni kati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga ama kuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting.

Katika kipindi kifupi takribani mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau, yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.

Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu Jamiiforums nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea Dar es Salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.

Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia, na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita JKT halafu 60000 naweka mfukoni kisha wale vibarua badala ya kuwalipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari, tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu, muda wote sina furaha, nilikuwa napenda kusoma, kuongeza ujuzi, kutafuta kazi, kuwekeza, kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, nina muda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama ni tatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui na adui wangu anaehujumu uchumi wangu ni betting.
Safi sana na hongera mkuu,mi ni miongoni mwa wapingaji wa kamari,ukiona jambo limezuiwa na mungu hilo halifai totally,uenda ukaokoa na wengine ambao wako katika huo utumwa wa kamari.
 
Back
Top Bottom