Hata mimi nakubaliana na wewe leo kuwa Betting ni laana tena laana mbaya sana.
Kuna jamaa namfahamu alianza Betting tangu mwaka 2007 wakati huo wengi wenu mlikuwa hata hamjui Betting ni kitu gani.
Ni miaka karibia 14 imepita na jamaa amefilisika kabisa , amechoka mbaya sana, mpaka sura yake imeharibika, amezeeka kabla ya wakati.
Nilikutana naye mwezi uliopita sikuamini kama ni yeye kwa jinsi alivyochakaa. Kwa sababu alikuwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ikabidi anieleze ukweli wake kuwa kilichomfilisi na kumkongoroa ni betting.
Kwa kifupi jamaa anajuta na anasema kwa kipindi cha miaka 14 amepoteza mamilioni ya pesa kwenye sports betting na online casino.
Kama wewe umeamua kuacha, umefanya uamuzi sahihi kabisa.