Tena hiyo jackpot utapunwa hizo buku mbili mbili ukija shituka umezeeka
Hayo ni maisha tu, Cha ajabu wewe hubet lkn hakuna chochote ulichowekeza, ni sawa na yule mpita njia aliyemshauri mvuta sigara aache kuvuta unajua nn kilitokea? Fuatilia
Mpita njia: rafiki kwann unapenda kuvuta sigara?
Mvuta sigara: kwa sababu kila nikijaribu kuacha nashindwa.
Mpita njia: sigara moja inauzwaje?
Mvuta sigara: Kati ya 200/250 na kuendelea
Mpita njia: kwa siku unavuta sigara ngapi?
Mvuta sigara: kuanzia 5/6 siku nikiwa vizuri nafikisha mpaka 10.
Mpita njia: ukipiga hesabu ya sigara unazo vuta kwa siku ukizidisha mara mwezi mara miaka uliyoanza kuvuta huoni hiyo hela ungeitunza ungekuwa tajiri na kutembelea gari lako la kifahari?
Mvuta sigara: wewe ni tajiri?
Mpita njia: hapana
Mvuta sigara: una gari la kifahari?
Mpita njia: hapana hata baiskeli Sina.
Mvuta sigara: unavuta sigara.
Mpita njia: hapana sivuti.
Mvuta sigara: embu niongezee 150 nikanunue sigara maana wewe na Mimi letu moja tu.