Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Duh mkuu unamuwekea muhindi hadi 250,000/=? Jamani watu mna hela hadi naona wivu?[emoji848] hongera kwa kupata 10mil
Hiyo ndogo mbona, hiyo 4.9mil niliwahi mpa Chelsea ushindi akicheza na Watford wakatoa Draw dakika ya 93
Nilitukana sana
 
Wakuu kutokana na mafanikio na hasara mlizopata kupitia hiyo Betting je would you recommend wengine ambao hawaijui kujaribu bahati zao ama tusiingie kabisa huko? Hizo wins zinatamanisha ila pia hivo vipigo mmh[emoji848]
Hii ni biashara kama zingine, wanao umia ni wale waaoweka mtaji mdogo wakitegemea kupata zaidi... Mf mtu anaweka 500 apate 1mil
 
Yaani mnaoingia kwenye betting,forex na gambling games zozote.... wakati shuleni mlifeli hesabu za probability, differentiation na integration wala statistics...mnajitafutia kifo.
Aiseee
 
Hii ni biashara kama zingine, wanao umia ni wale waaoweka mtaji mdogo wakitegemea kupata zaidi... Mf mtu anaweka 500 apate 1mil
Sasa hapo nani mjinga anaeweka 1m analiwa yote au an aeweka 500 kujifurahisha
 
Betting kwa kiswahili ni bashiri, sasa wewe unataka uishi maisha ya kubashiri?

Siku zote unapo bet weka kiasi ambacho hata ukipoteza hutolaumu.
 
Hizo hela za betting ungeamua kununua vitu vya geto, ungekuwa mbali sana.
Kamari haiwezi kukutoa kimaisha. Vijana wengi mnadanganyana sana vijiweni.
Fanya kazi na Mungu ataibariki kazi ya mikono yako
Wewe ambaye hu bet hivyo vitu vingi vya ghetto umeshanunua?
 
Siku zote masikini ndiyo wanahela. Ukitaka kupata pesa nyingi weka huduma inayowalenga masikini. Utapiga pesa sana.
Mo siyo mjinga kuuza kiberiti kwa shilingi 100. Fikiria ni masikini wangapi wanatumia kiberiti. Ni pesa ndefu sana
Betting inaamisha pesa kutoka kwa masikini kwenda kwa masonko
 
Jana kwa mfano unashindwaje kuweka tot win, barca win juve win na arsenal uweke 5000 upige 20,000. Mimi niliweka 1000 nikapiga 8000, naridhika na nafurahia mchezo sasa kama wew umefanya ni ajira shauri yako, acha tu.

sasa ulishindaje na tot alipigwa ?
 
Tena hiyo jackpot utapunwa hizo buku mbili mbili ukija shituka umezeeka
Hayo ni maisha tu, Cha ajabu wewe hubet lkn hakuna chochote ulichowekeza, ni sawa na yule mpita njia aliyemshauri mvuta sigara aache kuvuta unajua nn kilitokea? Fuatilia

Mpita njia: rafiki kwann unapenda kuvuta sigara?

Mvuta sigara: kwa sababu kila nikijaribu kuacha nashindwa.

Mpita njia: sigara moja inauzwaje?

Mvuta sigara: Kati ya 200/250 na kuendelea

Mpita njia: kwa siku unavuta sigara ngapi?

Mvuta sigara: kuanzia 5/6 siku nikiwa vizuri nafikisha mpaka 10.

Mpita njia: ukipiga hesabu ya sigara unazo vuta kwa siku ukizidisha mara mwezi mara miaka uliyoanza kuvuta huoni hiyo hela ungeitunza ungekuwa tajiri na kutembelea gari lako la kifahari?

Mvuta sigara: wewe ni tajiri?

Mpita njia: hapana

Mvuta sigara: una gari la kifahari?

Mpita njia: hapana hata baiskeli Sina.

Mvuta sigara: unavuta sigara.

Mpita njia: hapana sivuti.

Mvuta sigara: embu niongezee 150 nikanunue sigara maana wewe na Mimi letu moja tu.
 
Mkuu Hujaingia Deep naongea Kutoka Experience......!! Nimeshuhudia Mjeshi wa Nyota Tatu akiuza Friji na Kitanda Ili akacheze Kamari... Nimeshuhudia Watu wazima na Familia zao wakicheza Mshahara Wote Familia zinalala Njaa... Aisee acha Tuu.... Hili Ni Janga Kubwa kuliko Unga... Ni vile athari zake hazionekani kwa Haraka maana Mtu anagugumia Maumivu ndanikwa Ndani... Tafuta Documentary Moja Ya BBC Wameonesha Athari za Hi kitu nadhani ilikuwa Uganda... Watu wameuza Hadi Nyumba Na Wameishia Kujiua....
Kama Haushiriki Mshukuru Sana Muumba wako na Pia Jiweke Mbali kabisa Na KAMWE USIJARIBU.....!!!
Mtu anayeuza nyumba na vitu vya ndani vya muhimu ili abeti huyo ni mpumbavu.
 
Hayo ni maisha tu, Cha ajabu wewe hubet lkn hakuna chochote ulichowekeza, ni sawa na yule mpita njia aliyemshauri mvuta sigara aache kuvuta unajua nn kilitokea? Fuatilia

.

Wazo zuri ndugu endelea kufuma mikeka especially hiyo jackpot, uwezekano wa kuwa millionaire ni mkubwa
 
Nmeliwa 300k jana ila cjawahi fikiria kuacha betting mwaka wa saba huu npo kwenye game
 
Achana na kitu inaitwa addiction...Kuna mhindi mwaka wa tano huu anavaa t-shirt moja, kisa kubet
Hao ni binadamu wenye psychology displine ndogo.

Addiction kama ya opium(unga) hii inafanya hadi mwili unauma yaani unakuwa mgonjwa kabisa na huwezi kufanya lolote bila la kusniff.

Kwenye kamari ni easy kujua when to stop.

Addiction ya kukubali kupoteza mfano jerojero kama hawa wa bodaboda wanavyobet hii haina madhara yoyote.
 
Back
Top Bottom