Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Seriously mkuu lakini emu nambie ukweli, umeweza kuacha kabisa????

historia yako inafanana na mimi japo sikuwai acha gari mbili, lakini kimtonyo nilikuwa nastake high sasa kuna muda naliwa kuna muda nakula, faida kubwa nakumbka niliwai pata milioni 5 tu.

huwa kuna jini la kubet unakuta kuna siku unarudi rudi.
 
Safi sana na hongera mkuu,mi ni miongoni mwa wapingaji wa kamari,ukiona jambo limezuiwa na mungu hilo halifai totally,uenda ukaokoa na wengine ambao wako katika huo utumwa wa kamari.
 
Kubet ni starehe

Ni mchezo wa bahati nasibu

Sasa wewe ulitaka ikutoe kimaisha kosa lilianzia hapo

Ulishawahi kuskia wapi watu wanahimizwa kubet kama kazi
Ukisikia matangazo ya vyombo vya habari,ni kama vile hiyo ni ajira,waliobobea katika kamari,uwambii kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…