Chris wood
JF-Expert Member
- Dec 21, 2020
- 1,667
- 5,043
- Thread starter
- #21
AmenHongera sana kwa kuchukua maamuzi hayo na Mungu akusimamie katika maamuzi yako [emoji120]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AmenHongera sana kwa kuchukua maamuzi hayo na Mungu akusimamie katika maamuzi yako [emoji120]
Yaani bora anaeweka 1000 kwenye odds 2000 maana huyo anafanya starehe, kuliko huu ujinga wa sure odds unaweza pigwa ukachakaa.Pole sana Mkuu, Ila hizi kauli mbiu ndio huwa zinamaliza Watu.., "Eti Bet Kistaarabu" Nani kasema kwenye Ulevi kuna Ustaraabu!!!
Ni disaster ndugu.Mkuu tumalize ligi ndio utoe hayo maamuzi
Man city win
Madrid win
Tia laki utanishukuru
[emoji3][emoji3][emoji3]
kama anaweza kuweka 35 kwenye mkeka huyo hana njaa.Kuna jamaa yangu alishinda 1.2m mwaka jana, akambetia jirani yangu nae akashinda 1.5m. Hiyo ni mwaka jana, mwaka huu anzia january jamaa ni vipigotu ukiangalia betslip yake lost lost lost, alafu mkeka haweki below 35k, yote ni vipigo mpaka mda huu. Ukimwambia swala la kubeti ananyong'onyea.
Dah wewe n Gambler mkuuTulia wewe kama umeshindwa tuachie tubeti sisi
Betting sio dili asee .Kuna jamaa yangu alishinda 1.2m mwaka jana, akambetia jirani yangu nae akashinda 1.5m. Hiyo ni mwaka jana, mwaka huu anzia january jamaa ni vipigotu ukiangalia betslip yake lost lost lost, alafu mkeka haweki below 35k, yote ni vipigo mpaka mda huu. Ukimwambia swala la kubeti ananyong'onyea.
Tatizo ww unabeti kutoka kimaisha wengine tunabeti kama burudaniKwanza niseme tu mimi nikati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.
Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga amakuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting
Katika kipindi kifupi takriban mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.
Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau ,yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.
Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama,, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu,
Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu jamii forum nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea dar es salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.
Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.
Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.
Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia ,na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita jkt halafu 60000 naweka mfukoni,.kisha wale vibarua badala ya kuwa lipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari ,tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.
Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu ,muda wote sina furaha ,nilikuwa napenda kusoma,kuongeza ujuzi,kutafuta kazi,kuwekeza,kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.
Bado sijachelewa, ninamuda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama nitatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui,na adui wangu ane hujumu uchumi wangu ni betting.
Ni zaidi ya sembee maana inafanya mtu anakuwa na tamaa ya pesa nyingi. Badala yake unajikuta mfungwa wa vipigo kila kukichaKuna wafanyakazi wanakaribia kuingia rumande kisa kubet
Na wala hawajashtuka kama inawafilisi ndo kwanza wanalia waongezewe mshahara wanasahau nao pia hautatosha sababu ya bet
Shukuru umeshtuka hiyo kitu ni sawa na sembe.
Hiyo ni starehe ila mimi nilikuwa nabet kutoka kimaisha,Kwani ukiweka 1000 ukapata 5000 kuna shida gani? Kwanini uweke pesa nyingi kwa tamaa ya utajiri kwenye shughuli za watu?
Siwezi tembeza mihogo ndugu. Ila pesa yangu kuliko kuipeleka kwa muhindi ni bora nifanyie vitu vya maana.Sawa. Sasa Chukua Beseni La Mihogo Uanze Kutembeza Barabarani, Betting Ina Wenyewe Ndio Kazi Pekee Inayotumia 70% Ya Akili Kene Ubungo Wako.
Wamepoteana kwenye ramani! Unakula dola 100 unaliwa 600!kwan wale gurus wa Fx wanasemaje?