Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Pole sana Mkuu, Ila hizi kauli mbiu ndio huwa zinamaliza Watu.., "Eti Bet Kistaarabu" Nani kasema kwenye Ulevi kuna Ustaraabu!!!
Yaani bora anaeweka 1000 kwenye odds 2000 maana huyo anafanya starehe, kuliko huu ujinga wa sure odds unaweza pigwa ukachakaa.
 
Kuna jamaa yangu alishinda 1.2m mwaka jana, akambetia jirani yangu nae akashinda 1.5m. Hiyo ni mwaka jana, mwaka huu anzia january jamaa ni vipigotu ukiangalia betslip yake lost lost lost, alafu mkeka haweki below 35k, yote ni vipigo mpaka mda huu. Ukimwambia swala la kubeti ananyong'onyea.
 
kama anaweza kuweka 35 kwenye mkeka huyo hana njaa.
 
Betting sio dili asee .
 
Tatizo ww unabeti kutoka kimaisha wengine tunabeti kama burudani
 
Kuna wafanyakazi wanakaribia kuingia rumande kisa kubet

Na wala hawajashtuka kama inawafilisi ndo kwanza wanalia waongezewe mshahara wanasahau nao pia hautatosha sababu ya bet

Shukuru umeshtuka hiyo kitu ni sawa na sembe.
Ni zaidi ya sembee maana inafanya mtu anakuwa na tamaa ya pesa nyingi. Badala yake unajikuta mfungwa wa vipigo kila kukicha
 
Kwani ukiweka 1000 ukapata 5000 kuna shida gani? Kwanini uweke pesa nyingi kwa tamaa ya utajiri kwenye shughuli za watu?
Hiyo ni starehe ila mimi nilikuwa nabet kutoka kimaisha,
Yaani siku nilikuwa nikibahatisha napata pesa nyingi na fungu kidogo natenga kwenda kula raha na mademu, sasa hiyo 3000 hata nikishinda nitafanyia nini hata pesa ya bundle haijarudi
 
Sawa. Sasa Chukua Beseni La Mihogo Uanze Kutembeza Barabarani, Betting Ina Wenyewe Ndio Kazi Pekee Inayotumia 70% Ya Akili Kene Ubungo Wako.
Siwezi tembeza mihogo ndugu. Ila pesa yangu kuliko kuipeleka kwa muhindi ni bora nifanyie vitu vya maana.

Kuhusu hiyo 70% unajidanganya labda uwe newbie kwenye gemu. Kwa kiswahili hiyo ni bahati nasibu
 
Jana kwa mfano unashindwaje kuweka tot win, barca win juve win na arsenal uweke 5000 upige 20,000. Mimi niliweka 1000 nikapiga 8000, naridhika na nafurahia mchezo sasa kama wew umefanya ni ajira shauri yako, acha tu.
 
Mkuu tatizo unabet kimaskini unaweka 500 ili ushinde million unaona inawezkana? Hio ni bht sana asee. Mimi niliweka 500k nikala 6m na usheee lakin ningeweka 500 hapo ningeshinda 6000 unaona utofauti hapo nmepata faida ya 5.5m. Ukibet ukaweke pesa ndogo lazma uweke tim nyingi ili dau liwe kubwa lakin ukiweka timu chache dau kubwa unakua na probability kubwa ya kushinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…