Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Nashukuru mungu hii kitu nimeacha miaka miwili nyuma.. Hali yangu ilikuwa tete, nilikuwa teja la kutupwa.. Imenifilisi kiasi fulani.. 1xbet, live betting ndio ugonjwa wangu.

Huu si mchezo wa maana hata kidogo.
Kweli kabisa. Unakuwa na mategemeo makubwa ya kupata pesa nyingi kwa mkupuo, kumbe ndio unajikanga na kutajirisha ma patel humu mjini.
 
Tupe somo kaka, zile over unakula mwenyewe tu

Mim over hapan [emoji23][emoji23][emoji23]Yan mim nikiweka over mkeka unachanika juzi Kati nilimpa Bayern over 1.5 alafu akafungwa 2-1 [emoji2][emoji2]kuna siku nikampa simba over 0.5 first half stake 250K ikaisha 0-0 mim ni mwendo wa under tuu stake kubwa
 
Dah wewe kama mimi mzee! Yani over sinaga upepo nazo kabisa! Nachezaga Cricket kuna league moja inaitwa gold league nachezaga points za individual team zinaitwa runs!

Nikiweka over tu jua hio over hawafikishi! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ naliwa yani ila under mambo mswano!
 
Leo siko kwenye mood ya kubishana ndugu , hapana nilipo nauguza maumivu sitafuti Ligi hapa.
Naona wewe betting umeijulia ukubwani. Ngoja nikusaidie mchezo wowote ambao unakupa chance, percentage/possibility fulani ili ushinde hiyo ni gambling/betting.

Unachekesha sana Biko unasema ndio bahati na sibu yes, maana unakuta ni wewe against mlioshiriki, kama mlioshiriki ni 100 hapo chance ya kupata ni 1/100.

Hivyo hivyo ucheze mpira wa miguu kuna chance zake, iwe umeweka direct win,,kona, yellow card zote zina chance zake, haina guarantee eti lazima ushinde. Unaweza kuweka PSG awin dkk ya 15 neymar anapigwa red muhindi anachenge odds maana hapo possibility ya kushinda imepungua.

Miaka 9 kwenye game hujawahi chaniwa kwa odds ya 1.05? Unaona mdau hapo amezungumzia cricket kuwa haina draw hapo anamaanisha chance ya kula imeongezeka kutoka 0.3 hadi kufika 0.5 yaani 50/50.
 
Betting nikiboko nimefanya hii kwa miaka mitatu Ila hasara Ni kubwa saiv nimeamua kufanyo hold tu ya crypto currency na Kama stellar,Bitcoin ,etherium,litcoin na nyingne nying hii Naona kabsa kwanza nilichelewa but all in all ni nzur Sana.
 
Mkuu kwanza pole,sana ila hii betting is not for everybody, pia hapa unaniona nishawahi kula ada kisa betting, ila bado game on ila now vipigo vimezidi natulia mpaka mwezi wa sita.ila nishawahi kula 80k kwa buku.So this game is a matter of chance.Ila huu mchezo huwezi kutoboa kimaisha fanya for fun...

Last ukiambiwa sehemu fulani kuna fursa jua katika mental hard drive yako.Wewe ndo fursa.

Ila kama admini wa group la risk takers nasikitika kupoteza mwanachama muhimu sana ..dah..haya.
 

Man Ungelijua Kila Kazi Inachangamoto Zake Na Kila Biashara Haikosi Hasara Usingekuwa Na Maneno Mengi. Kwa Ufupi Ulifanya Kitu Usichokijua, Betting Haimtaki Mtu Mwenye Kichwa Cha Kufugia Nywele
 
Betting nikiboko nimefanya hii kwa miaka mitatu Ila hasara Ni kubwa saiv nimeamua kufanyo hold tu ya crypto currency na Kama stellar,Bitcoin ,etherium,litcoin na nyingne nying hii Naona kabsa kwanza nilichelewa but all in all ni nzur Sana.
Umefanya la maana kuliko kupoteza bora ufanye investment
Mwaka 2019 wakati bitcoin ina drop watu wanaipigia kelele ilifika hadi usd 3000 na kipindi hicho nilikuwa naweza kutoa usd 1500 ninunue hata nusu bitcoin lakini washikaji wakaanza kusema tohold kwanza inaweza drop hadi 500 ndio hadi leo unaona imefika 60000 roho inauma
Mbaya zaidi watu wanasema by 2028 huko inaweza fika 500,000usd roho inaniuma kwa kweli
 
Mimi huwa naamini kila kitu maishani ni kamari. Hivyo betting nitaacha siku wao wakiacha
Nina rekodi ya kuliwa 4.9mil baada ya Chelsea kudraw.
Nina Rekodi ya kupiga 10mil stake 250K
 
Ndio asee kutoboa, kwenye life kupitia betting nikazi sana ,wengi wanabeti,wengi wanaliwa,wengi wanapoteza,wanaofaidika ni wachache sana.
 
Man Ungelijua Kila Kazi Inachangamoto Zake Na Kila Biashara Haikosi Hasara Usingekuwa Na Maneno Mengi. Kwa Ufupi Ulifanya Kitu Usichokijua, Betting Haimtaki Mtu Mwenye Kichwa Cha Kufugia Nywele
Ndio ukweli huo betting kuliwa kwingi, kula kidogo.

Mimi kuna mwezi nimekula zaidi ya 9million za muhundi lakini nikirudi kupiga hesabu ninahasara kubwa tu.

Ndio maana kukutolea uvivu jaribu kuangalia kwenye betting history yako uone kama toka umeanza kubet umepata faida au unatumika kuwasomesha watoto wa muhindi shule za gharama kwa pesa yako
 
[emoji3][emoji3][emoji3] huu hauhitaji hasira
 
We endelea kulia, izo zote nimepiga ndani ya wiki hii. Cheza live than angalia mpira vizuri kabla ya kustake
 
We endelea kulia, izo zote nimepiga ndani ya wiki hii. Cheza live than angalia mpira vizuri kabla ya kustake
View attachment 1771945View attachment 1771946View attachment 1771947View attachment 1771948View attachment 1771950
Hapo umemuonesha upande wako wa bahati ili kumufanya awe inspired.
Muoneshe pia upande wa maumivu ili awe cautious.

Nijuavyo mimi, watu wa gambling ni kama motivational speakers. Wanakuonesha upande mmoja mzuri. Mengine utakutana nayo huko mbele ya safari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…