RASMI: Pre Season Ya Yanga SC Kufanyika Tanzania, wachezaji 7 watajwa sababu

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Wanajamvi na mashabiki wote wenzangu wa Utopolo FCa.k.a Mabingwa Wa Kihistoria Wa LigiKUU Tanzania a.k.a Mabingwa watetezi na pia Mabingwa wajao wa kombe la Ngao ya Hisani ya Agosti 13, 2022.

Wakati huu napenda kuwaletea taarifa nzuri ambazo wengi wenu mlikuwa mkizitamani.

Nimetoka ofisini hapa mitaa ya Jangwani. Ofisini palikuwa na utulivu mkubwa mithili ya kwamba ni siku ya Jumatatu na kila mtu alionekana yuko bize na jambo muhimu, hakika kweli watu wanapiga kazi aisee.

Jambo lililonileta hapa ni kufikisha Kamera za kisasa kabisa kwa ajili ya media ya timu ya Yanga SC maana waliomba kuzi import kutoka Ujerumani.

Katika pita zangu nikaona sio mbaya kupitia idara ya ukurugenzi kupata taarifa mbili tatu.

Moja ya taarifa niliyopewa na ambayo haijawekwa rasmi katika mitandao ya kijamii ni kuwa Mabingwa watetezi hawatosafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Nimetaarifiwa pia sababu ya msingi ni kwamba sehemu kubwa ya wachezaji watakao ripoti kambini mnamo tarehe 18.07.2022 hawatokuwapo kambini bali watakuwa katika majukumu ya timu ya taifa.

Hivyo uongozi umeona hauna sababu ya kuenda mbali kwa sababu wachezaji 7 wa kikosini hawapo.

Aidha, menajiment imetoa taarifa kuwa Logistics za maandalizi ya kambi yao ya nje ya nchi hayakuwa yamekamilika kwa wakati hivyo basi wameona ni vyema wasalie nchini kwa ajili ya maandalizi zaidi.

KONGOLE UONGOZI, PIA KONGOLE KWA MASHABIKI MLIO PAZA SAUTI ILI ZISIKIKE.
 
Jambo jema sana hili

Wachezaji 7 wote ambao ni muhimu kabisa ambao watakuwa timu ya Taifa mpaka tarehe 30 mwezi wa 7 ndio mechi ya mwisho kuchezwa na timu ya Taifa na kwa maana hiyo wachezaji hao automatic watakuwa wameikosa Kambi hiyo hasa ikiwekwa nje ya nchi

6.8.2022 kutakuwa na wiki ya mwananchi hvyo kwa ratiba hiyo hakuna haja ya kwenda kambi nje ya nchi bila wachezaji wako muhimu

Yanga hatutakiwi kurejea makosa kama ya Mwaka jana
 
Vipi taarifa za dokta kususa baada ya kuona Ki kasajiliwa kwa pesa ndefu huku yeye ajalipwa pesa zake?

Ni vigumu sana watu wenye ngozi nyeusi kususa.

Wako tofauti kidogo na yule muhindi wa Bilioni 20 hewa.

Ambaye kwa sasa amejiweka kando kidogo na wakina Try Again wanaiendesha timu kutumia pesa za mdhamini mpya M-Bet ambaye alisainishwa July mosi.
 
Mhh poleni hela imekwishia si mseme tuuu jamani?
 
Vipi taarifa za dokta kususa baada ya kuona Ki kasajiliwa kwa pesa ndefu huku yeye ajalipwa pesa zake?
Kwani wachezaji wanahitajika kambini tarehe ngapi? Unapotuambia kasusa amesusaje hebu tuambie, wachezaji wote wanaanza kuripoti kambini twrehe 18, Na huyo Aucho utamuona akiingia kambini hizo propaganda zinazosambazwa na wale Mbumbumbu fc wapeni pole yao
 
hahahahahaha Genius senzo wakati linaingia mkataba na waturuki hawakujau hii ratiba? au mechi ya taifa stars imestukizzwa? vichaa nyieeee sasa mkalipe hiyo milions 200 ya waturuki haraka..yaani mna book mwezi kabla bila kujua ratiba? Aziz ki kachafua madaftari..hongera Yacouba kwa kumstua mshkaji wako asichukue hela nununusu kama kina Aucho
 
Aziz K amewaumiza Wana Simba wengi sana, Baada ya game ya ngao ya jamiii wata paraganyika vibaya. Kwasasa waacheni wachonge.
Msije mkamtimua profesa wenu maana nyie uto hamnaga uvumilivu kabisa
 
Aziz K amewaumiza Wana Simba wengi sana, Baada ya game ya ngao ya jamiii wata paraganyika vibaya. Kwasasa waacheni wachonge.
actually tumemfurahia sana, yaani ilikuwa ni mwendo wa kujitekenya na kucheeeka kwa sauti..ujio wake tayari impact za kufurahsiha zishaonekana halafu unasema tusikitike , we are glad yupo hapo utopoloni
 
Msije mkamtimua profesa wenu maana nyie uto hamnaga uvumilivu kabisa
Ubingwa umewapa utulivu wa uongo timbwili lao huwa linajulikanaga kwa sasa wanajifanya eti wastaarabu, hata kwenda kupokea new signings airport wameacha.
 
Natamani sana kuona viongozi wa Yanga na benchi la ufundi wakiibakiza timu nchini kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi, na pia kwa ajili ya mechi za Kimataifa.

Hayo mambo ya kwenda kuweka kambi nje ya nchi, ni mbwembwe tu.
Pesa za magodoro fake zimekombwa zoteeee. [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mkalipe bill ya watu Uturuki huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…