RASMI: Pre Season Ya Yanga SC Kufanyika Tanzania, wachezaji 7 watajwa sababu

RASMI: Pre Season Ya Yanga SC Kufanyika Tanzania, wachezaji 7 watajwa sababu

Wanajamvi na mashabiki wote wenzangu wa Utopolo FCa.k.a Mabingwa Wa Kihistoria Wa LigiKUU Tanzania a.k.a Mabingwa watetezi na pia Mabingwa wajao wa kombe la Ngao ya Hisani ya Agosti 13, 2022.

Wakati huu napenda kuwaletea taarifa nzuri ambazo wengi wenu mlikuwa mkizitamani.

Nimetoka ofisini hapa mitaa ya Jangwani. Ofisini palikuwa na utulivu mkubwa mithili ya kwamba ni siku ya Jumatatu na kila mtu alionekana yuko bize na jambo muhimu, hakika kweli watu wanapiga kazi aisee.

Jambo lililonileta hapa ni kufikisha Kamera za kisasa kabisa kwa ajili ya media ya timu ya Yanga SC maana waliomba kuzi import kutoka Ujerumani.

Katika pita zangu nikaona sio mbaya kupitia idara ya ukurugenzi kupata taarifa mbili tatu.

Moja ya taarifa niliyopewa na ambayo haijawekwa rasmi katika mitandao ya kijamii ni kuwa Mabingwa watetezi hawatosafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Nimetaarifiwa pia sababu ya msingi ni kwamba sehemu kubwa ya wachezaji watakao ripoti kambini mnamo tarehe 18.07.2022 hawatokuwapo kambini bali watakuwa katika majukumu ya timu ya taifa.

Hivyo uongozi umeona hauna sababu ya kuenda mbali kwa sababu wachezaji 7 wa kikosini hawapo.

Aidha, menajiment imetoa taarifa kuwa Logistics za maandalizi ya kambi yao ya nje ya nchi hayakuwa yamekamilika kwa wakati hivyo basi wameona ni vyema wasalie nchini kwa ajili ya maandalizi zaidi.

KONGOLE UONGOZI, PIA KONGOLE KWA MASHABIKI MLIO PAZA SAUTI ILI ZISIKIKE.
Mlipopanga kwenda Uturuki hadi mnadaiwa huko akili mliziweka maliwatoni?
FB_IMG_1611660294488.jpg
 
Back
Top Bottom