Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sure,point mkuuHata kina Andrea Ayew walitokea kwenye timu ya vijana.Matumaini yangu wakifanya vizuri,utakuwa ndiyo mwanzo watanzania kukua kisoka.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] Sasa mkuu bila kushndana nawalio Bora tutawezaje kuwa Bora ?Mngejua kundi Alilopangwa serengeti ni bora angemwachia tu Congo akamalizane nao mwenyewe
[emoji3] [emoji3] [emoji1] [emoji3]Wamfanye Diamond Platinum kocha mkuu mbeba bendera, ana uzoefu na fainali na kuondoa ukweli wa kuqualify kimbelekombeleko
Ndio mkuuKwa hiyo tukishanda tunachukua AFCON ya viboys au
Ngoja na sisi watukatie rufaa na vijeba vyetu!HATIMAYE timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys imerejeshwa kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akiwa mwenye furaha kubwa amesema jioni ya leo; "Timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 imefaulu kucheza fainali za Afrika. Hongera Serengeti Boys! Hongera Tanzania!,"amesema Malinzi bila kufafanua.
Mwanzoni mwa mwezi uliopita, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliwapa siku 10 Shirikisho la Soka Kongo (FECOFOOT) kumuwasilisha mchezaji Langa Lesse Bercy mjini Libreville, Gabon afanyiwe vipimo vya MRI ili kuthibitisha umri wake kama anaruhusiwa kucheza mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17.
Katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF jana mjini Libreville, FECOFOOT walitakiwa kumpeleka mjini humo Langa Lesse Bercy akafanyiwe vipimo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya zoezi hilo kushindikana mara mbili.
Na hatua hiyo ilifuatia Rufaa ya TFF dhidi ya mchezaji huyo baada ya Kongo kuitoa U-17 ya Tanzania katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za mwaka huu zilizopangwa kufanyika Madagascar.
Awali, Kongo walitakiwa kumpeleka mchezaji huyo makao makuu ya CAF mjini Cairo, Misri kwa vipimo, lakini mara mbili wakashindwa kufanya hivyo.
source: binzubeir blog
Mngejua kundi Alilopangwa serengeti ni bora angemwachia tu Congo akamalizane nao mwenyewe
Mkuu Tanzania tulishakutwa na hilo sakata la vijeba, timu yetu ilifuzu fainali za vijana U17 zilizopita ikaondolewa kwa kudanganya umri wa wachezaji. Naamini makosa hayajarudiwa.Ngoja na sisi watukatie rufaa na vijeba vyetu!
waache kuweka mamluki, ni ujinga tu waafrika tunakuwa nao, ni heri timu itolewe mapema kwa kuwapa nafasi wachezaji wenye umri stahili, kuliko kuwa bingwa kwa kupanga mibabu iliyofoji umri!
lengo la mashindano ya vijana ni kusaidia nchi kuibua na kulea vipaji vya vijana ili wawe hazina hapo baadae ktk timu za taifa, huku kwetu mizee inadandia na ujinga wa mashirikisho ya soka, yanataka cosmetic sifa ilhali wakijua hawana kitu cha kujivunia kwa kuwa wali-cheat!
Wapo kambini since day oneInabidi madogo warudi kambini fasta
Wewe sio MtanzaniaMngejua kundi Alilopangwa serengeti ni bora angemwachia tu Congo akamalizane nao mwenyewe
We ni Mtanzania kweli?Wamfanye Diamond Platinum kocha mkuu mbeba bendera, ana uzoefu na fainali na kuondoa ukweli wa kuqualify kimbelekombeleko
Mkuu mimi sijakuelewaNgoja na sisi watukatie rufaa na vijeba vyetu!
waache kuweka mamluki, ni ujinga tu waafrika tunakuwa nao, ni heri timu itolewe mapema kwa kuwapa nafasi wachezaji wenye umri stahili, kuliko kuwa bingwa kwa kupanga mibabu iliyofoji umri!
lengo la mashindano ya vijana ni kusaidia nchi kuibua na kulea vipaji vya vijana ili wawe hazina hapo baadae ktk timu za taifa, huku kwetu mizee inadandia na ujinga wa mashirikisho ya soka, yanataka cosmetic sifa ilhali wakijua hawana kitu cha kujivunia kwa kuwa wali-cheat!
kwa maana hiyo unadhani vijeba hamna?Mkuu Tanzania tulishakutwa na hilo sakata la vijeba, timu yetu ilifuzu fainali za vijana U17 zilizopita ikaondolewa kwa kudanganya umri wa wachezaji. Naamini makosa hayajarudiwa.
hujanielewa kwamba nimeongea pumba au unahitaji ufafanuzi Zaidi:Mkuu mimi sijakuelewa
kambi walishaanza wiki hii mwanzoniInabidi madogo warudi kambini fasta