Rasmi: Serikali yaridhia kutungwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Rasmi: Serikali yaridhia kutungwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Baraza la Mawaziri limeridhia kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi.

Amesema kwa mara ya kwanza sheria hiyo itasomwa katika mkutano wa Bunge utakaoanza Jumanne ya Septemba 13, 2022 jijini Dodoma huku akiwataka wadau watakaokuwa na nafasi ya kutoa maoni wafanye hivyo.

Nape ameyasema hayo leo Jumatano, Septemba 7, 2022 wakati akifungua mkutano wa wadau wa mawasiliano na TEHAMA (Connect to Connect) Afrika.

"Tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu kuwa na sheria ya kulinda data binafsi na habari njema ni kwamba kwa sasa tumeruhusiwa kuendelea na mchakato na mwezi huu sheria itasomwa bungeni," amesema.

PIA SOMA:
Chanzo: Mwananchi
 
Hatua nzuri ya kuishi kama binadamu waliostaarabika kwa kiwango cha juu
 
Hawachelewi kukuchorea ramani mpaka uvunguni kwako
 
NAPE VIJANA WANAOMBA HUDUMA YA PayPal MBONA UMEZIBA MASIKIO?

ULIPOTOLEWA BASTOLA NA KISANDUKU HAWA VIJANA WALISIMAMA NA WEWE!

ULIPOENDA IKULU KUMWAGA MACHOZI YA MSAMAHA HAWA VIJANA WALISIMAMA NA WEWE!

usiwasahau!
 
Tutajie mmoja kati yao
 
Back
Top Bottom