Rasmi serikali yaruhusu na kuzindua matumizi ya magari ya umeme Tanzania

Rasmi serikali yaruhusu na kuzindua matumizi ya magari ya umeme Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kutoka Dodoma Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko amezindua matumizi rasmi ya magari ya umeme Kwa Wananchi wanapotaka kuyatumia.

View: https://www.instagram.com/p/C7nwUkRtb0m/?igsh=MTltOXdyenk3cjZieA==
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezindua magari yanayotumia mfumo wa umeme ikiwa ni jitihada za serikali za kuwezesha wananchi kutumia nishati safi nchini. Uzinduzi wa magari hayo umefanyika Alhamisi Mei 30, 2024 jijini Dodoma sanjari na uzinduzi wa Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na kituo cha uzalishaji wa umeme wa jua.

"Niwapongeze wadau wetu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa hatua hii, mtakumbuka kwamba serikali inaendelea kutafuta mbadala wa kuwawezesha wananchi hasa wale walio na uhitaji zaidi wa nishati safi” Amesema Dkt. Biteko. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wadau wanaoshirikiana na Serikali kutafuta uwezekano wa kuwa na nishati safi ya uhakika ili kufikia malengo ya asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ifikapo 2034. Kwa upande wake mwakilishi wa UNDP, Weyinmi Omanuli ameipongeza serikali kwa hatua zinazoendelea kuelekea kuwawezesha wananchi wake katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.

Amesema kuwa kampeni ya Nishati Safi ya kupikia imekuwa kielelezo thabiti cha serikali kuwajali wananchi wake hususani wale wa kipato cha chini. Naye mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Cedric Marel amesema umoja huo una imani kubwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati kuendeleza jitihada za kuwakomboa wananchi kwa kuandaa mazingira wezeshi yanayolenga kuboresha maisha yao. Akitoa salamu za utangulizi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema hatua ya uzinduzi wa magari yanayotumia umeme ni mwendelezo wa mpango wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia. "Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa chini ya Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayolenga kuongeza matumizi ya nishati safi nchini” Amesema Senyamule.​

My Take
Safi sana, ukilalamika bei ya Juu ya Mafuta geukia magari ya umeme au gesi.

Samia amesema by 2034 anataka 80% ya Watanzania watumie Nishati safi.

Kazi za Samia zinaongea huhutaji propaganda.

View: https://twitter.com/EUinTZ/status/1796415222804312126?t=BHF9GAIIOipYbLaHcClY0w&s=19
 
Kuna Uzi ulikuwemo humu kuhusiana na magari ya umeme. Nataka nione tena uwezo wa kukaa na umeme. Tatizo ilikuwa battery zenye uwezo wa kukaa muda mrefu na umeme. Na vituo vya kuchajia umeme. Pia unachaji kwa muda gani?. Au tayari wamegundua battery ya kutumia kilomita zaidi ya 1500?
 
Back
Top Bottom