Rasmi serikali yaruhusu na kuzindua matumizi ya magari ya umeme Tanzania

Rasmi serikali yaruhusu na kuzindua matumizi ya magari ya umeme Tanzania

Batter miezi 7 tu zinakufa afu nigharama kinoma,kwenyegesi bado tupo nyuma asasa vituo vyakujazia gas🐸👈,diesel, petrol,ndo suluhisho.
Kaka una miliki gari? Umewahi endesha brand ngapi mpaka sasa? Hakuna gari duniani lisilo na changamoto. Ndio maana spear zipo, ndio maana yananunuliwa duniani kote
 
Shida siyo kununua shida mnavyo sema yatapunguza gharama,wakati tunajua miezi simingi yanakufa battery au unajua magari ya hybrid ndo yanaingia leo? Yalikuwapo toka awali👈.
Gari la hybrid betri yake tu niliwahi sikia bei milioni 10. Hiyo ni betri tu.

Wazungu wafanye wafanyavyo, mafuta ndio suluhisho ya yote.

Waarabu wabarikiwe sana, kama ni njama zao wazungu kuwaumiza waarabu wamegonga mwamba.

Tunaomba tu mafuta yashuke bei, atleast 2000 per litre
 
Jamani hii Ndiyo fursa changamoto ni sehemu ya mfanyabiashara ama mtumiaji kwani huwezi kununua betri ya ziada ama charger? Mnapendaz sana kulalamika? Wataalamu wa kulalamika kwenye hili siwaungi mkono
Ishu sio kulalamika. Ilitakiwa kuwekwa miundo mbinu stahiki iendane na huu uzinduzi.

Umewahi jua kero wanayopata watumiaji wa vyombo vinavyotumia gesi? Hebu siku moja pita ubungo maziwa kwenye kituoa cha ujazaji gesi
 
Kutoka Dodoma Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko amezindua matumizi rasmi ya magari ya umeme Kwa Wananchi wanapotaka kuyatumia.

View: https://www.instagram.com/p/C7nwUkRtb0m/?igsh=MTltOXdyenk3cjZieA==
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezindua magari yanayotumia mfumo wa umeme ikiwa ni jitihada za serikali za kuwezesha wananchi kutumia nishati safi nchini. Uzinduzi wa magari hayo umefanyika Alhamisi Mei 30, 2024 jijini Dodoma sanjari na uzinduzi wa Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na kituo cha uzalishaji wa umeme wa jua.

"Niwapongeze wadau wetu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa hatua hii, mtakumbuka kwamba serikali inaendelea kutafuta mbadala wa kuwawezesha wananchi hasa wale walio na uhitaji zaidi wa nishati safi” Amesema Dkt. Biteko. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wadau wanaoshirikiana na Serikali kutafuta uwezekano wa kuwa na nishati safi ya uhakika ili kufikia malengo ya asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ifikapo 2034. Kwa upande wake mwakilishi wa UNDP, Weyinmi Omanuli ameipongeza serikali kwa hatua zinazoendelea kuelekea kuwawezesha wananchi wake katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.

Amesema kuwa kampeni ya Nishati Safi ya kupikia imekuwa kielelezo thabiti cha serikali kuwajali wananchi wake hususani wale wa kipato cha chini. Naye mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Cedric Marel amesema umoja huo una imani kubwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati kuendeleza jitihada za kuwakomboa wananchi kwa kuandaa mazingira wezeshi yanayolenga kuboresha maisha yao. Akitoa salamu za utangulizi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema hatua ya uzinduzi wa magari yanayotumia umeme ni mwendelezo wa mpango wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia. "Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa chini ya Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayolenga kuongeza matumizi ya nishati safi nchini” Amesema Senyamule.​

My Take
Safi sana, ukilalamika bei ya Juu ya Mafuta geukia magari ya umeme au gesi.

Samia amesema by 2034 anataka 80% ya Watanzania watumie Nishati safi.

Kazi za Samia zinaongea huhutaji propaganda.

View: https://twitter.com/EUinTZ/status/1796415222804312126?t=BHF9GAIIOipYbLaHcClY0w&s=19

Huko yalikoanzia mbaona wanaanza kuyapiga na chini.Hayajaleta faida yoyote.
Tanzania hata umeme wa kuonea ni shida huo wa kuchaji betri za gari utatokea wapi.Unaweza ukalala njiani bila sababu
 
Huko yalikoanzia mbaona wanaanza kuyapiga na chini.Hayajaleta faida yoyote.
Tanzania hata umeme wa kuonea ni shida huo wa kuchaji betri za gari utatokea wapi.Unaweza ukalala njiani bila sababu
Hizo gari zitakuwa msaada mkubwa sana kwa hapa mjini. Unakuwa nayo ya kuchaji na ya mafuta kwa ajili ya safari ndefu.

Imagine unapata ya kwenda hata 500km unaweza zunguka hata week 3 hujaichaji. Thats a single charge tu hebu compare kama litre moja ni TZS 3,314/= na unit moja ya umeme ni TZS 350/= huoni kama kuna tofauti ya almost 90% ya bei hizi mbili. Kwa gharama za mafuta zilivyopaa hivi huwezi kukwepa ishu ya gari za umeme. Ni sababu hazijafika tu ila hata Gas watu wataiona ni expensive.
 
Ishu sio kulalamika. Ilitakiwa kuwekwa miundo mbinu stahiki iendane na huu uzinduzi.

Umewahi jua kero wanayopata watumiaji wa vyombo vinavyotumia gesi? Hebu siku moja pita ubungo maziwa kwenye kituoa cha ujazaji gesi
Umeme hauwezi kuwa kero kama wanaojazana vituo vya gesi.

Imagine watu wanaweza kulipia wakafungiwa 3 phase mitaani wakaweka mashine za kusaga. Same kind of installation unaweza wekewa kwako ukawa unachaji gari yako ya umeme kwa fast charger.
 
Hizo gari zitakuwa msaada mkubwa sana kwa hapa mjini. Unakuwa nayo ya kuchaji na ya mafuta kwa ajili ya safari ndefu.

Imagine unapata ya kwenda hata 500km unaweza zunguka hata week 3 hujaichaji. Thats a single charge tu hebu compare kama litre moja ni TZS 3,314/= na unit moja ya umeme ni TZS 350/= huoni kama kuna tofauti ya almost 90% ya bei hizi mbili. Kwa gharama za mafuta zilivyopaa hivi huwezi kukwepa ishu ya gari za umeme. Ni sababu hazijafika tu ila hata Gas watu wataiona ni expensive.
Umeme uko wapi?
 
Ishu sio kulalamika. Ilitakiwa kuwekwa miundo mbinu stahiki iendane na huu uzinduzi.

Umewahi jua kero wanayopata watumiaji wa vyombo vinavyotumia gesi? Hebu siku moja pita ubungo maziwa kwenye kituoa cha ujazaji gesi
Serikali haiwezi kuweka miundombinu hiyo kwasasa kwasababu bado hawajajipanga lakini nijukumu la serikali kuwaunga mkono wananchi wake kwenye harakati mbalimbali zinazoleta mabadiliko kwenye jamii pia nijukumu la sekta binafsi kujenga miundombinu hiyo hata kwa ubia na serikali km ambavyo wameleta hayo magari hata wengine kuanza kuyaunda kwamtizamo wangu hii ingelikuwa ni fursa kwako kibiashara kumbuka binadamu hana ukomo wa kufikiri hata mimi ninaiona fursa ngoja niichangamkie kwa maana fursa haiwezi nifuata
 
Hizo gari zitakuwa msaada mkubwa sana kwa hapa mjini. Unakuwa nayo ya kuchaji na ya mafuta kwa ajili ya safari ndefu.

Imagine unapata ya kwenda hata 500km unaweza zunguka hata week 3 hujaichaji. Thats a single charge tu hebu compare kama litre moja ni TZS 3,314/= na unit moja ya umeme ni TZS 350/= huoni kama kuna tofauti ya almost 90% ya bei hizi mbili. Kwa gharama za mafuta zilivyopaa hivi huwezi kukwepa ishu ya gari za umeme. Ni sababu hazijafika tu ila hata Gas watu wataiona ni expensive.
Services moja ya car electric ni zaidi ya fuel engine!. Afu isitoshe bado atuna mafundi wakutosha wa new generation.
 
Gari la hybrid betri yake tu niliwahi sikia bei milioni 10. Hiyo ni betri tu.

Wazungu wafanye wafanyavyo, mafuta ndio suluhisho ya yote.

Waarabu wabarikiwe sana, kama ni njama zao wazungu kuwaumiza waarabu wamegonga mwamba.

Tunaomba tu mafuta yashuke bei, atleast 2000 per litre
Sasa mabetri ya car electric yanafikia uzito wa 450kg hizo ni betri tu!😁😁😁 afu tuachane na fuel.
 
Services moja ya car electric ni zaidi ya fuel engine!. Afu isitoshe bado atuna mafundi wakutosha wa new generation.
Hio service hadi itokee sio leo unless ule buyu la maana iharibike components. Ile ni kama TV tu ama Feni. Ukinunua brand ya kueleweka unapiga 10-15 years bila kipengele.

Hayana vikorokoro vingi kama magari ya mafuta. Mule humwagi oil wala kubadili filter kila mwezi
 
Hatakuwa na usajili kwenye mfumo wetu, si unaona hata hizi piki piki za umeme hazina usajili.

Ila sasa hivi nadhani zitatakiwa kusajiliwa rasmi. Hichi ni kichaka cha mapato yaliyokuwa tanapotea.
Kichaka cha mapato au upuuzi tu. Kama appliances zinasajiliwa tuanze kusajili mafeni, tv, subwoofer, laptop, washing machine.

Hizo pikipiki na magari lengo ni kupunguza gharama sio viwe kichaka cha dhuluma. Umeme unalipwa na makodi kibao extra. Vikitumia umeme ndio namna vitaingiza mapato.
 
Back
Top Bottom