RASMI: Singida Big Stars tumeinasa saini ya Abdulmajid Mangalo kutoka Biashara United

RASMI: Singida Big Stars tumeinasa saini ya Abdulmajid Mangalo kutoka Biashara United

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Watu wa Soka,

Kuanzia sasa Abdulmajid Mangalo ni
BIG STAR.

Tumemuongeza kikosini Nahodha huyu kutoka klabu ya Biashara United na tutakuwa nae kwa mkataba wa miaka miwili.

Mangalo ni mchezaji anayemudu kucheza nafasi mbalimbali uwanjani hususani beki wa kati, amesaini nasi baada ya kumalizana na Biashara United.

Karibu sana Singida Big Stars "BEKI KISIKI".

MANGALO1.jpg
 
Mchukueni na Mayele wa Utopoloni pale ndio tujue mko siriaz na ligi

Kama unamaanisha Yanga, walishatangaza hawamuuzi Mayele. Hata hivyo, tayari tumeshamsajili beki wa Yanga, Paul Godfrey, maarufu kwa jina la Boxer na tutakuwa nae kwa miaka miwili.
 
Tetesi za chini zinasema pre season mnaenda kuweka kambi marekani. Je ni kweli haya?
 
Hao wachezaji ndio wanaowafaa, sio wale wazuri wazuri ambao mnawasajili halafu wanavunja mkataba kabla hawajatumikia

Ukiondoa Habib Kyombo hakuna mchezaji mwingine aliyeomba kuvunja mkataba. Pia wote tunaowasajili ni wachezaji wazuri wenye uwezo wa kutupatia matokeo tunayoyataka.
 
Habib Kyombo ilikuwaje mkashindwa kulinda mkataba wake?

Mkataba wake haukuwa na tatizo lolote. Alitumia haki yake kuvunja mkataba na ana baraka zetu zote. Pia safu yetu ya ushambuliaji imesheheni, kuondoka kwake sio hasara kwetu hata kidogo ndio sababu tukamruhusu.
 
Back
Top Bottom